NAFASI 15 za Kazi Dereva Daraja La II Arusha City Council
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Jiji la Arusha kuomba nafasi za kazi
zilizotajwa hapo chini baada ya kupokea kibali chenye Kumb. Na. FA/97/228/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili, 2025 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala.
DEREVA DARAJA LA II – NAFASI (15)
MAJUKUMU YA KAZI
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
iii. Kufanya matengenezo madogo ya gari.
iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
vi. Kufanya usafi wa gari; na
vii. Kufanya kazi nyingine atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua
mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo
ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali yaani TGS B1
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 25 Juni, 2025.
MUHIMU: Kumbuka kutuma barua yako iliyosainiwa pamoja na vyeti kwenda kwa;
Mkurugenzi
Halmashauri ya Jiji la Arusha
S. L. P 3013
20 Barabara ya Boma
23101 ARUSHA
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kieletroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal)