Mfano wa Barua Rasmi | Muundo wa barua Rasmi
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Mfano wa barua rasmi au barua ya kikazi, Habari ya wakati huu mpenzi wa blog yako pendwa ya Habarika24, katibu katika makala hii fupi ambayo itaenda kukupa maezo na mfo juu ya barua rasmi au baru aya kikazi.
Barua Rasmi
Hii ni aina ya barua ambayo huandikwa kwa lengo maalumu hasa mawala ya kiofisi . Mmabo yanayo bebwa na barua rasmi ni kama vile;
- Barua za kuomba kazi au vitu mbali mbali
- Kutoa taarifa za mikutano ya kiofisi
- Kuagiza vifaa mbali mbali vya kiofisi
Aina za Barua Rasmi
Kuna aina nyingi za barua rasmi lakini barua zote hizo zinaweza kugawanywa katika makundi makuu 3 kulingana na dhumuni harisi la barua husika. Makundi hayo ni pamoja na
- Barua za taarifa
- Barua za maombi mbalimbali
- Barua za upokeaji vifaa.
Mtindo wa barua Rasmi
Mtindo wa barua rasmi ni tofauti kabosa na baru nyingine kama zile za kirafiki kwani barua hizi humfunga mwandishi kwa kua humtaka mwandishi kuandika barua hii kwa ufupi zaidi huku ndienda moja kwa moja kwenye lengo la barua kwa kutumia lugha nyepesi na sentensi fupi fupi zinazo fuata sheria na kanuni za uandishi

Muundo wa barua Rasmi
Hapa chini tutaenda kuangalia mambo yaliyomo katika uandhishi wa barua resmi
1. Anwani ya mwandishi
Hii huandikwa juu kabisa mwa barua upande wa kulia mwa karatasi,
2. Tarehe
Bada ya anuani ya mwandichi basi chini ya anauani hiyo ndipo uandikwa tarehe, hii hutoa taarifa juu ya siki gani baria ndio iliandikwa.
3. Kumbukumbu namba
Hii ni namba ambayo huwa kama kitambulisho cha barua; mara nyingi huwa na tarakimu pamoja na herufi, kwa mfano: MFF HG 01
4. Anwani ya mwandikiwa
Anuani ya mwandikiwa hukaa upande wa kushoto mwa karatasi baada ya kumbu kumbu namba na huanza kwa kutaja cheo cha unayemwandikia
5. Mwanzo wa barua
Hii huandikwa chini y anuani ya mwandikiwa kama salamu kwa neno “ndugu” kisha kutaja jina au cheo cha mwandikiwa
6. Kichwa cha barua
Kishwa cha barua hutaja kwa ufupi zaidi lengo au dhumuni la barua, kishwa cha barua hudokeza kwa ufupi sana nini kusudi la msingi la barua hiyo
7. Kiini Cha Barua
Hap ndio hutolewa maelezo ya kina juu ya lengo na kusudi la barua kwa kuzingatia kichwa cha barua. Mwandishi anapaswa kutumia sentesi fupi fupi katika kuelezea lengo na kusudi la barua kwa kuzingatia lugha nyepesi na inayoeleweka.
8. Mwisho wa barua
Hapa mwandishi wa barua hutumia maeno mazuri ya kuhitimisha barua yake mfano wa maneo yanayotumika ni pamoja na
- Wako mtiifu
- Wako katika kazi
- Wako katika kujenga taifa
- Wako mwanachama
9. Saini au jina la mwandishi
Baada ya hitimisho la barua mwandishi wa barua anatakiwa kuweka saini au kutaja jina lake
10. Cheo cha mwandishi
Hapa mwandishi humalizia kwa kutaja cheo chake, mfano wa cheo ni kama vile
- Mwombaji,
- Mwalimu wa darasa,
- Mwanafunzi,
- Kiranja mkuu,
- Waziri wa elimu,
- Mjumbe wa tawi
Hitimisho
Mwandishi wa barua rasmi anapaswa kuzingatia mtindo na muundo wa barua kwani hicho ndio kielelezo cha utambulisho wa barua hii. Mambo ya msingi ya kuzingatia ni kama vile matumiji ya lugha,Matumizi ya sentensi fupi zenye kufuata kanuni za kiuandishi, kujikita kwenye lengo la batua na matumizi ya lugh nyepesi,
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Dar es Salaam
3. Bei ya iPhone 16 Pro Max Tanzania 2024
4. Bei ya iPhone 16 ProTanzania 2024
5. Viwango Vipya Vya Mishahara ya Walimu Serikalini
6. EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania 2024
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku