Chuo cha usalama wa Taifa Tanzania,Ghuo cha idara ya usalama wa taifa, Habari ya wakati huu mwana habarika24, karibu tena katika makala hii amabyo tunaenda kukuelezea juu ya chuo cha usalama wa taifa Tanzania. Kama wewe ni miongoni mwa wanohitaji kujiunga na chuo cha idara ya usalama wa taifa basi makala mhii itakupa taarifa kwa kilefu kuufu chuo cha usalama wa taifa.
Usalama wa Taifa
Hii ni taasisi ya kisetikali ambayo inajukumu la kusimamia na kulinda usalama wa nchi wa ndani na nje ya mipaka ya taifa huku ikishirikiana kwa karibu kabisa na mashirika mengine ya kiusalama kimataifa.
Chuo Cha Usalama Wa Taifa
Hii ni taasisi inayojihusisha na utoaji wa mafunzo kwa maafisa na viongozi wanaojianda ili kujiunga na idara ya usalama wa Taifa. Hii ni taasisi muhimu sana kwani ndio taasisi inyo hakikisha kinatoa maafisa bora kabisa ambao jukumu lao kubwa ni kuhakikisha kuwa usala wa nchi unakuwepo mda wote.
Chuo cha usalama wa Taifa hujulikana kama chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC)
Historia ya chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC)
Mipango ya kuanzisha Chuo cha Taifa cha Ulinzi ilianza tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katikati ya miaka ya sitini. Hata hivyo, wazo halisi la kuanzishwa kwa Chuo cha Taifa cha Ulinzi nchini Tanzania lilitolewa miaka ya 1990. Kabla ya kufungua Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, maafisa kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wamekuwa wakihudhuria kozi za Usalama wa Taifa nje ya nchi haswa katika nchi za Kenya, India, Uingereza, Bangladesh, Pakistan, n.k.
Dhana ya kuanzisha Chuo cha Taifa cha Ulinzi imekuwepo kwa zaidi ya miongo mitatu. Mnamo 1998, Makao makuu ya Jeshi yaliunda kamati ambayo ilichunguza uwezekano wa kuanzisha Chuo cha Taifa cha Ulinzi. Kamati ilisisitiza umuhimu wa kuwa na Chuo cha Taifa cha Ulinzi nchini. Hata hivyo, haikuwa rahisi kuanzisha chuo hicho wakati huo kutokana na ufinyu wa fedha na gharama kubwa za uendeshaji wa chuo. Mnamo 2008 wazo la kuanzishwa kwa Chuo cha Taifa cha Ulinzi lilifufuliwa tena. Jeshi la Ukombozi la Watu wa China liliombwa na walikubali kujenga chuo kwa msaada. Tarehe 10 Januari, 2011 kampasi mpya iliyojengwa ilikabidhiwa kwa JWTZ katika hafla kubwa iliyoongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Tarehe 11 Aprili, 2011 Kitivo cha Chuo cha Taifa cha Ulinzi kikijumuisha Mkuu wa Chuo Meja Jenerali (sasa Luteni Jenerali (Mstaafu) na balozi wa URT nchini Zimbabwe, Charles Lawrance Makakala, Wakufunzi Waandamizi Waelekezi watatu na Katibu wa Chuo waliteuliwa kuanza maandalizi ya Kozi ya kwanza ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi. Tarehe 10 Septemba 2012 Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu alizindua rasmi Chuo na kozi yake ya kwanza.

Kozi Zitolewazo na Chuo Cha Taifa Cha Ilinzi
Shahada ya Uzamili na Diploma ya Usalama
Kutayarisha maafisa wakuu waliochaguliwa wa vikosi vya jeshi, huduma za kiraia na wale kutoka nchi washirika kwa kuchukua jukumu la juu katika mwelekeo na usimamizi wa usalama wa kitaifa na mkakati.
Mafunzo ya Kimkakati
Mafunzo ya kimkakati ni mafunzo maalumu yanayotolewa kwa viongozi na maafisa ulama kwalengo la kuwandaa kwa majukumu ya juu ya kiusalama katika nchi.
Uchambuzi wa Usalama wa Kitaifa
Mafunzo haya hutolewa kwa lengo la kuwapa maafisa usalama uwezo wa kupitia na kuifahamu kwa udani hali ya usalama wa nchi iwe ndani au hata nje ya mipaka ya nchi.
Usalama wa Kimataifa
Haya pia ni mafunzo wanayopatiwa maafisa na viongozi wa usalama ili kuwa na uwezo wa kushugulikia maswala ya kimataifa nje ya mipaka ya Tanzania.
Umuhimu Wa Mafunzo ya Usalama wa Taifa
Idara ya Uongozi;
Upande wa uongozi mafunzo haya yanaumuhimu sana kwani huwajenga viongozi kua bora na wenye kufuata sheria kwa maslai ya usalama wa taifa letu.Hapa mafunzo haya huwagusa zaidi maafisa na viongozi wa kiusalama hivyo hujenga uwezo wao katika kuimalisha usalama wa nchi.
Ngazi ya Kimataifa
Katika kiwango cha kimataifa mafunzo haya pia ni muhimu kwa sawala la kiusalama kutoka nje ya mipaka ya nchi yetu kwani huwapa mwongozo viongozi na maafisa walioshiki mafunzo hayo utaalamu wa hali ya juu kuhusu maswala ya kiusalama pale yanapofikia kiwango cha kimataifa, jinsi na namna ya kukabiliana na changamoto zozote zile za kiusalama katika kiwango cha kimataifa.
Mfano ulinzi na usalama wa viongozi wa nchi wanapokua nje ya mipaka ya nchi ya Tanzania.
Ngazi ya Kitaaluma
Pia katika upande wa taaluma mafunzo haya huwafanya maafisa washiriki kuweza kuongeza na kupanua ujuzi wao dhidi ya kukabiliana na maswala mbalimbali yanayo husu usalama wa nchi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Sifa Za Kujiunga Na Chuo cha Usalama Wa Taifa
Ili kujiunga na chuo cha usalama wa taifa na uweze kuajiliwa na kufanya kazi katika idara ya usalama wa taifa nchini Ranzania basi lazima uwe umekidhi baadhi ya sifa na vigezo;
Hapa tunaenda kukuwekea sifa na vigezo unavyotakiwa kuwa navyo ili kupata nafasi za kujiunga na chuo cha ulinzi wa Taifa;
1.Uwe Uraia Wa Tanzania.
Ili uweze kukubariwa kujiunga na chuo cha usalama wa taifa inchi Tanzania basi kigezo cha kwanza huwa ni uraia wa mwombaji, Hivyo basi basi kwa Tanzania lazima uwe RAIA WA TANZANIA.
2. Uwe na Afya Nzuri
Kabla hujajiunga na chuo cha usalama wa taifa lazima upitie vipimo mbali mbali za kiafya kwani lazima uwe na afya nzuri.
3. Uwe na Elimu Kuanzia Kidato Cha Nne
Pia ukitaka kujiunga na chuo hiki lazima uwe na elimu angalau kuanzia kidato cha nne na kuendelea
4. Usiwe na Rekodi ya Uharifu
Kma lengo lako ni kujiunga na chuo cha usalama wa taifa basi hakikisha ya kua hujawahi kua na tabia mbaya amabyo iliperekea kukupa rekodi ya aina yoyote ile ya kiharifu.
5. Usiwe na Tatoo yoyote.
Unapo taka kujiunga na chuo cha mafunzo ya usalama wa taifa basi hakikisha ya kua mwili wako haujawahi kuchorwa tatoo ya aina yoyote ile.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. LATRA: Nauli Mpya Za Mabasi Ya Mikoani
3. TIRA MIS Uthibitishaji wa Uhai wa Bima Ya Gari.
4. Jinsi ya Kuangalia Salio NBC Bank
5. JINSI ya Kupata TIN Number Online
6. Jinsi ya Kusajiri Kampuni Tanzania
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku