Tangazo La Kuitwa Kwenye Usaili Chuo cha Sukari cha Taifa (NSI) May 2025

Filed in Usaili by on May 12, 2025 0 Comments

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Chuo cha Sukari cha Taifa (NSI), MDAs & LGAs anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 24-05-2025 hadi 30-05-2025 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo
yafuatayo:-

  • Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
  • Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
  • Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
  • Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka.
  • Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
  • Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
  • Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
  • Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
  • Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTVET au NECTA)
  • Waombaji kazi ambao hawajaona majina yao kwenye tangazo hili wanapaswa kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal na kuona sababu za kutokuitwa kwao ili wasikose fursa wakati mwingine.
  • Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
  • Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili.
  • Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.

 

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp Channel Join Now!