
Baada ya tarifa zilizoweza kutolewa na mwana habari wa klabu ya Yanga Ally Kamwe mbele ya vyombo vya habari kua wanaidai TFF na wazamini wakuu wa kombe la shirikisho (CRDB Federation Cup) kiasi cha shiling Milioni 200 za zaawadi za mshindi wa michuano hiyo kwa msimu wa 2023/2024, TFF imetoa taarifa za kukanusha madai hayo.
TFF imekanusha madai hayo na kutoa ufafanuzi kua Yanga iliiomba TFF kukata madeni inayodaiwa kupitia fedha zao za zawaidi tena ilienda mbali kwa kusema maombi hayo yalifanywa kwa barua kutoka klabu ya Yanga.
Kufuatia sakata hilo TFF imeitaka yanga kumwangiza kutuma mtaalamu wa fedha kwenda kuhakiki akiwa na nyaraka za uthubitishi hapo kesho 11/06/2025.