Kampuni ya Ndege Tanzania kinapenda kuwataarifu wote walioomba kazi katika kada mbalimbali
kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 5 Julai, 2025 hadi tarehe 10 Julai, 2025.
Wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
- Usaili utafanyika tarehe 5 Julai, 2025 hadi tarehe 10 Julai, 2025 kama ilivyooneshwa
kwenye tangazo hili; - Muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;
- Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
- Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkaazi, Kitambulisho cha
Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Taifa, Hati ya Kusafiria au Leseni ya
udereva; - Wasailiwa wanatakiwa kufika na vyeti vyao halisi, kuanzia cheti cha Kuzaliwa, Kidato cha
IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea
kutegemeana na sifa za Mwombaji; - Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”,
hati za matokeo za Kidato cha IV na VI (Form IV and Form VI result slips) HAZITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI - Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;
(viii) Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili; - Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa
hawakukidhi vigezo; - Wasailiwa wenye tofauti ya majina katika vyeti vya elimu, taaluma na cheti cha kuzaliwa
wahakikishe wanakuwa na kiapo cha kubadilisha majina kilichosajiliwa (DEED POLL); - Wasailiwa waliozaliwa nje ya Tanzania wahakikishe wanawasilisha uthibitisho wa uraia
kutoka Ofisi za Uhamiaji.
MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Air Tanzania
Ili kuweza kutizama orodha kamili ya majina ya walioitwa kwenye usaili kampuni ya Air Tanzania bonyeza linki hapo chini
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA TANGAZO