Tahasusi za Kidato cha Tano zimegawanywa katika makundi makuu kulingana na mwelekeo wa taaluma na mahitaji ya soko la ajira.
1. Tahasusi za Sayansi (Science Combinations)
-
PCM – Fizikia, Kemia, Hisabati
-
PCB – Fizikia, Kemia, Baiolojia
-
CBG – Kemia, Baiolojia, Jiografia
-
CBN – Kemia, Baiolojia, Lishe (Nutrition)
-
PGM – Fizikia, Jiografia, Hisabati
-
PGMc – Fizikia, Jiografia, Kompyuta
-
CBM – Kemia, Baiolojia, Hisabati
-
PMCs – Fizikia, Hisabati, Sayansi ya Kompyuta
-
CBCh – Kemia, Baiolojia, Kichina
2. Tahasusi za Biashara (Business Combinations)
-
EGM – Uchumi, Jiografia, Hisabati
-
ECA – Uchumi, Biashara, Uhasibu
-
HGE – Historia, Jiografia, Uchumi
-
EBuAc – Uchumi, Masomo ya Biashara, Uhasibu
-
BuAcM – Masomo ya Biashara, Uhasibu, Hisabati
-
ECsM – Uchumi, Sayansi ya Kompyuta, Hisabati
3. Tahasusi za Sanaa na Lugha (Arts & Language Combinations)
-
HGL – Historia, Jiografia, Kiingereza
-
HGK – Historia, Jiografia, Kiswahili
-
HKL – Historia, Kiswahili, Kiingereza
-
HGCh – Historia, Jiografia, Kichina
-
HGF – Historia, Jiografia, Kifaransa
-
KLF – Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa
-
KArCh – Kiswahili, Kiarabu, Kichina
-
LFAr – Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu
4. Tahasusi za Michezo (Sports Combinations)
-
Michezo, Elimu ya Mwili na Lishe
-
Michezo, Elimu ya Mwili na Baiolojia
-
Michezo, Elimu ya Mwili na Jiografia
Umuhimu wa Tahasusi Mpya
Tahasusi hizi ni sehemu ya juhudi za serikali:
-
Kuimarisha ubunifu na ujuzi wa karne ya 21
-
Kulinganisha elimu na mahitaji ya soko la ajira
-
Kuwapa wanafunzi uhuru wa kuchagua mwelekeo wa taaluma kulingana na vipaji na malengo yao
Taarifa Muhimu kwa Wanafunzi
-
Wanafunzi wa Kidato cha Nne 2024 waliruhusiwa kubadili tahasusi kupitia mfumo wa SELFOM hadi tarehe 30 Aprili 2025.
-
Hatua hii ililenga kuwasaidia wanafunzi kupanga upya mwelekeo wa kitaaluma kulingana na ufaulu na ndoto za baadaye.
Maelezo Zaidi
Kwa taarifa kamili na sahihi zaidi, tembelea:
-
Tovuti rasmi ya TAMISEMI (SELFOM):
https://selform.tamisemi.go.tz/tahasusi

