Katika ulimwengu wa kisasa wa michezo ya kubahatisha mtandaoni, kubet imekuwa moja ya shughuli maarufu zinazovutia watu wengi duniani na hapa nyumbani Tanzania. Lakini pamoja na umaarufu huu, watu wengi bado hawajui aina tofauti za betting (kubet) pamoja na maana ya kila aina ya bet wanazokutana nazo. Katika makala hii, tutaelezea kwa kina option mbalimbali za kubet na tafsiri zake kwa Kiswahili ili kukusaidia kufanya maamuzi sahihi unapobashiri.
1X2 – Mshindi wa Mechi
Hii ni moja ya chaguzi maarufu kabisa katika kubet. Inajulikana pia kama Full Time Result.
1: Timu ya nyumbani (home) kushinda
X: Mechi kuisha kwa sare
2: Timu ya ugenini (away) kushinda
Mfano: Kama unabeti 1, unaamini timu ya nyumbani itashinda. Ikiwa timu hiyo itashinda, unapata ushindi.
Double Chance (1X, X2, 12)
Chaguo hili linakupa nafasi mbili za kushinda katika tukio moja.
1X: Timu ya nyumbani kushinda au sare
X2: Timu ya ugenini kushinda au sare
12: Either timu ya nyumbani au ugenini ishinde (hakuna sare)
Hili ni chaguo bora kwa wabetaji wanaotaka kupunguza hatari ya kupoteza.
Over/Under (Zaidi/Chini ya Mabao)
Hapa unabeti kuhusu idadi ya jumla ya mabao yatakayofungwa na timu zote mbili.
Over 2.5: Mabao 3 au zaidi yafungwe
Under 2.5: Mabao 2 au chini yafungwe
Over/Under zinaweza kuwa pia 0.5, 1.5, 3.5 n.k., kulingana na bookmaker.
Both Teams to Score (BTTS)
Katika chaguo hili, unaweka bet ikiwa timu zote mbili zitafunga goli au la.
Yes: Timu zote mbili zitafunga
No: Timu moja au zote hazitafunga
Hii ni bet inayopendwa sana kwenye mechi ambazo zinahusisha timu zenye safu kali za ushambuliaji.
Correct Score – Matokeo Sahihi
Hii ni moja ya option ngumu zaidi lakini yenye malipo makubwa.
Mfano: Unabeti matokeo yatakuwa 2-1, basi timu ya nyumbani lazima ishinde kwa magoli hayo haswa.
Ni bet hatari lakini inaweza kulipa vizuri ukiwa na uelewa mzuri wa form ya timu.
Half Time/Full Time (HT/FT)
Hapa unatabiri matokeo ya kipindi cha kwanza na ya mwisho wa mechi.
Mfano:
HT/FT 1/1: Timu ya nyumbani kushinda kipindi cha kwanza na mechi nzima
HT/FT X/2: Sare kipindi cha kwanza, timu ya ugenini ishinde mwisho
Ni chaguo la kipekee kwa wale wanaopenda kuchanganua mwenendo wa timu.
Handicap (Asia Handicap / European Handicap)
Handicap betting inahusisha kumpa timu moja faida au hasara kabla ya mechi kuanza.
Mfano:
+1 Handicap kwa timu A: Timu A inaanza na bao moja mbele
-1 Handicap kwa timu B: Timu B inaanza ikiwa imepunguzwa bao moja
Katika Asian Handicap, hakuna sare, hivyo odds huwa tofauti kidogo.
Draw No Bet (DNB)
Hii ni chaguo la kubet ambapo sare haizingatiwi. Ikiwa mechi itaisha kwa sare, unarudishiwa hela yako.
Bet yako inashinda kama timu uliyobetia inashinda
Ikiwa ni sare, unapata refund
Ni njia nzuri ya kupunguza risk ikiwa huamini kama timu moja inaweza kushinda wazi.
Outright Winner – Mshindi wa Mashindano
Hii inatumika kwenye mashindano kama vile:
Kombe la Dunia
EPL
UEFA Champions League
Unabeti timu gani itashinda mashindano yote, si tu mechi moja.
Anytime Goalscorer – Mfungaji Wakati Wowote
Unabeti mchezaji fulani atafunga bao wakati wowote kwenye mechi.
Mfano: Ukibetia Haaland kuwa ata-score, lazima afunge bao moja au zaidi ndani ya dakika 90.
Odds za chaguo hili hubadilika kulingana na fomu ya mchezaji.
First/Last Goalscorer – Mfungaji wa Kwanza/Mwisho
First Goalscorer: Mchezaji kufunga goli la kwanza kwenye mechi
Last Goalscorer: Mchezaji kufunga goli la mwisho
Ni chaguo hatari lakini lenye odds nzuri sana.
Multibet – Kubet Mechi Nyingi kwa Wakati Mmoja
Hii ni pale unapochanganya bets nyingi kwenye tiketi moja.
Mfano: Unabeti 1X kwa mechi ya Arsenal, Over 2.5 kwa Chelsea, na BTTS kwa Man United. Ili ushinde, chaguo zote lazima zifanikiwe.
Multibets huongeza odds lakini pia huongeza hatari ya kupoteza.
Live Betting – Kubet Wakati Mechi Inaendelea
Kubet moja kwa moja wakati mechi inaendelea hukuwezesha kutumia hali halisi ya mchezo.
Odds hubadilika kila dakika kulingana na matukio ya mechi.
Ni chaguo linalohitaji umakini na uamuzi wa haraka.
Cash Out – Kutoa Faida au Kupunguza Hasara
Cash out hukuruhusu kuvuna ushindi wako kabla mechi haijaisha, au kupunguza hasara kama hali ya mechi haielekei vizuri.
Ni zana muhimu kwa wabashiri wa kisasa.
Soma Pia;
1. Historia ya Yanga SC Kushuka Daraja