Ofisi Ya Usalama Wa Taifa
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
BONYEZA HAPA KUJIUNGA NA TELEGRAM CHANNEL YETU
Majukumu ya Ofisi ya Usalama wa Taifa
Kwanza kabisa kama tulivyosema hapo awali kua ofisi ya usalama wa taifa inamilikiwa na idara ya uslama wa taifa TISS ambayo kazi yake kuu ni kusimamia ulama na ulinzi wa taifa kwa kusaidiana na mashirika mengine ya ndani na nje ya mipaka ya taifa la Tanzania. hivyo basi hapa tutaenda kuangazia baadhi ya majukumu ya ofisi ya usalama wa taifa;
1. Kusimamia Taafirifa za Kiuslama
Kazi kuu ya ofisi hii chini ya idara ya usalama kupitia viongozi na maofisa wake ni kuhakikisha taarifa zote za kiuslama zinakusanywa na kufikishwa ofisini na kufanyinywa uchambuzi wa kina na kutolewa majibu.Lengo na madhumuni ya kazi hii ni kuipa serikali ushauli juu ya maswala ya usalama wa nchi na hatua za kuchukua ili kuhakikisha nchi ipo katika usalama wa kutosha.
2. Kulinda Nchi
Kazi ya ofisi ya usalama wa taifa ni pamoja na kuilinda nchi kupitia maofisha wake walioko katika mipaka ili kuhakikisha nchi ipo katika usalama wa kutosha kutoka katika vitisho vya ndani na nje ya nchi. Kuisimamia nchi dhidi ya magaidi na uvamizi.
3. Kuimatisha Ushirikiano
– Ofisi ya usalama wa Taifa, ndiyo idara inayojihusisha na jukumu la kushirikiana kwa katibu na mashirika ya kimataifa ikiwa lengo kuu ni kuhakikisha kuimalika kwa usalama katika mipaka ya Taifa la Tanzania.
– kushirikiana kadiri inavyowezekana na inavyohitajika na vyombo vingine vya dola na mamlaka za umma ndani au nje ya Tanzania vinavyoweza kusaidia Utumishi katika utendaji wa kazi zake
4. kuwashauri Mawaziri
Pale Mkurugenzi Mkuu anaporidhika kwamba ni muhimu kufanya hivyo, kuhusiana na masuala yanayohusu usalama, kwa kadiri mambo hayo yanavyohusiana na idara au nyadhifa wanazozisimamia;
5. Kutoa Taarifa Za Kiuslama
kumfahamisha Rais, na mtu mwingine yeyote au mamlaka ambayo Waziri anaweza kuielekeza, kuhusu eneo lolote jipya la ujasusi, hujuma, ugaidi au upotoshaji ambalo Mkurugenzi Mkuu ameona ni muhimu kulifanyia uchunguzi.
Muundo wa Uongozi
Mkurugenzi Mkuu
Mkurugenzi mkuu wa ofisi ya usalama wa taifa huteuliwa na raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Mkurugenzi huyo huudumu kwa kipindi cha miaka 5 na kwa masharti na masharti ya mshahara, posho, marupurupu ya uzeeni, na vinginevyo, kama Rais atakavyoona inafaa. au kama itakavyotolewa na au chini ya Sheria ya Mafao ya Kustaafu kwa Utumishi wa Umma namba 2.
Maafisa na wafanyakazi wa Idara ya usalama wa Taifa
Hii inajumuifa viongozi, maafisa na wafanyakazi wote ambao wanafanya shuguli za kiutendaji chini ya uongozi wa mkurugenzi wa usalama wa taifa
Hawa ndio hufanya kazi za utekerezaji wa majukumu yote ya kiutendaji ya uslama wa taifa ili kuhakikisha kua swala la ulinzi na usalama wa nchi lipo sawa sawa.
Viapo Vya Usalama Wa Taifa
Mfano Wa Kiapo Cha Ofisi ya Usalama Wa Taifa
Kiapo cha ofisi
Mimi, ____________________ hapa ninaapa/nathibitisha kwamba nitatekeleza kwa uaminifu na bila upendeleo kwa kadiri ya uwezo wangu kazi ninayohitaji kama _________________________ (jina la Ofisi) ya Huduma ya Upelelezi na Usalama ya Tanzania. Basi nisaidie Mungu.
Mfano wa Kiapo cha usalama
Mimi, ______________________________, hapa ninaapa/nathibitisha kwamba, bila mamlaka halali, sitafichua au kumfahamisha mtu yeyote taarifa zozote nilizozipata kwa sababu ya kazi nilizozifanya kwa niaba ya au chini ya uongozi wa Idara ya Upelelezi ya Tanzania. na Huduma ya Usalama au kwa sababu ya ofisi yoyote au ajira niliyonayo kwa mujibu wa Sheria ya TISS
Sheria na Kanuni
Sheria ya Huduma za Ujasusi na Usalama ya Tanzania inaweka misingi ya uendeshaji wa TISS, ikijumuisha mamlaka ya kukusanya taarifa, kuchunguza vitisho, na kutoa tathmini za kiusalama kwa serikali.
Kwa Maelezo zaidi Unaweza soma Makala kupitia linki hapo chini
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Usalama Wa Taifa Tanzania
2. Jinsi ya Kusajiri Kampuni Tanzania
3. Gharama za Usajili Wa Kampuni BRELA
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku