TAMISEMI: FORM FIVE SELECTION 2025/2026

_________________________________________________

MATANGAZO YA AJIRA  KILA SIKU BOFYA HAPA

_________________________________________________

NOTES ZA KIDATO CHA 1 HADI 6 BOFYA HAPA

_________________________________________________

MAGROUP MAPYA YA WHATSAAP BOFYA HAPA

_________________________________________________
MATANGO YA AJIRA BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

NAFASI za Kazi Dereva Daraja la II Makambako Town Council

Filed in Nafasi Za Kazi Tanzania 2025 by on June 19, 2025 0 Comments

Halmashauri ya Mji Makambako imepokea kibali cha Ajira mpya chenye Kumb. Na. FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29/04/2025 kwa nafasi ya Dereva Daraja la II, Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II na Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi kama ilivyoorodheshwa katika tangazo hili.

NAFASI za Kazi Dereva Daraja la II Makambako Town Council

DEREVA DARAJA LA II – NAFASI- 6

KAZI/ MAJUKUMU YA DEREVA

i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
vi. Kufanya usafi wa gari; na
vii. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
viii. Pamoja na kazi zingine utakazopangiwa na Mwajiri wako.

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya
uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1)
bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata
madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari

(Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine
kinachotambuliwa na Serikali.

MSHAHARA

Ngazi ya Mshahara ni TGS B1

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 01 Julai, 2025,

MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya Elimu, Anuani ya barua hiyo ielekeze kwa:-
Mkurugenzi wa Mji,
Halmashauri ya Mji Makambako,
S. L. P 405,
MAKAMBAKO.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira kupitia anwani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa (‘Recruitment Portal’)

 

Kwa Matangazo ya AJIRA Mpya kila siku BONYEZA HAPA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!