Nafasi ya Simba Sc Kwenye Ligi Kuu Ya NBC 2024/2025, Msimamo wa Simba SC ligi kuu ya NBC 2024/2025, Habari ya wakati huu mwanamichezo wa Habarika24, karibu katika makala hii fupi itakayoenda kukupa mwenendo wa klabu yako pendwa ya wekundu wa msimbazi Simba SC Kwenye ligi kuu ya NBC kwa msimu huu mpya wa 2024/2025.
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Klabu ya Simba inayofahamika kama wekundu wa msimbazi ni moja miongoni mwa klabu bora zaid nchini Tanzania ukiacha zile za Yanga na Azam, Simba SC ni miongoni mwa klabu zinazishiriki ligi kuu ya NBC kwa msimu huu mpya wa 2024/2025. Na ikiwa wewe ni moja ya maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu na klabu ya Simba basi huna budi kufuatilia mwenendo wa klabu yako kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC.
Hapa sisi kama chombo cha kukuhabarisha tupo tayari kukuletea taarifa zote za muhimu kuhusu msimamo wa Simba SC kwenye ligi kuu ya NBC,

Nafasi ya Simba SC Kwenye Ligi Kuu Ya NBC 2024/2025
Msimu mpya wa ligi kuu ya NBC tayari umesha anza kupamba moto huku klabu ya Simba ikizidi kujiimalisha kwa kuendelea kukusanya pointi na kujiweka kileleni mbele ya maasimu wao wakuu Yanga SC na Azam FC
- Hadi sasa klabu ya Simba imecheza michezo 11, imeshinda michezo 9, imedroo mchezo 1 na kufungwa mchezo 1
- Iko katika nafasi ya kwanza kwa jumla ya point 28
Simba iko mbele kwa pointi 1 kwa klabu ya Yanga iliyoko nafasi ya 2 kwa pointi 27 sawa na Azam FC iliyoko katika nafasi 3 ikiwa imecheza michezo 12.
Matokeo Ya Simba SC Ligi Kuu ya NBC 2024/2025
1. November 22, 2024
Pamba Jiji 0 – 1 Simba SC
2. November 6, 2024
Simba SC 4 – 0 KMC FC
3. November 1, 2024
Mashujaa FC 0 – 1 Simba SC
4. October 25, 2024
Simba SC 3 – 0 Namungo FC
5. October 22, 2024
Tanzania Prisons 0 – 1 Simba SC
6. October 19, 2024
Simba SC 0 – 1 Young Africans
7. October 4, 2024
Simba SC 2 – 2 Coastal Union
8. September 29, 2024
Dodoma Jiji 0 – 1 Simba SC
9. September 26, 2024
Azam FC 0 – 2 Simba SC
10. August 25, 2024
Simba SC 4 – 0 Fountain Gate
11. August 18, 2024
Simba SC 3 – 0 Tabora United
Michuano Mingine Inayoshiriki Klabu ya Simba 2024/2025
Simba nje ya kushiriki katika ligi kuu ya NBC lakini pia inashiriki michuano ya kombe la shirikisho Barani Afrika. Katika hatua hii ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika (CAF Confideretion Cup) Simba imepangwa katika kundi ikiwa na timu kama vile CS Sfaxien (Tunisia),CS Constantine (Algeria) na FC Bravos do Maquis (Angola)
– Hadi sasa Simba imecheza mchezo mmoja wa hatua ya makundi kiwa nyumbani kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa na kuibuka na ushindi wa magoli 1 kwa bila dhidi ya FC Bravos do Maquis
– Simba katika msimamo wa kundi A inashika nafasi ya 2 ikiwa na jumla ya pointi 3
Matokea ya Mechi za Simba Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025
- 27/11/2024Simba SC 1 – 0 FC Bravos do Maquis
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Nafasi ya Yanga Ligi Kuu Ya NBC 2024/2025
2. Jezi Mpya Za Simba SC Kimataifa Msimu Wa 2024/2025
3. Ratiba ya Simba SC Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025