Chuo cha Ualimu Arafah Tanga
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Chuo cha Ualimu Arafah, Habari ya wakati huu mwana Habarika24, karibu katika makala hii fupi ambayo tutaenda kuangazia juu ya chuo cha Ualimu Arafah. Kama wewe ni mwanafunzi unayejiandaa kujiunga na kozi ya Ualimu basi chuo cha Ualimu Arafah kinaweza kua miongoni mwa chaguzi zako.
Hapa katioka mala hii tutaenda kuangazia taarifa za msingi unazohitaji kuzifahamu kuhusu chuo cha ualimu Arafah kama vile kozi zitolewazo na chuo, ada kwa kila kozi, Fomu za kujiunga na chuo pamoja na sifa na vigezo vya kujiunga na chuo cha ualimu cha Arafah.
Chuo cha Ualimu cha Arafah ni miongoni mwa vyuo bora zaidi nchini kwa utoaji wa mafunzo ya ualimu, chuo kinapatikana mkoani Tanga kikiwa kimezungukwa na mazingira bora kwa kujifunzia na kukuza taaluma ya kada ya ualimu. Chuo kinapokea wanfunzi wapya na walimu ambao wako tayari katika ajira kwa lengo la kujiendeleza.
Chuo cha Ualimu cha Arafah kimejikita zaidi kwenye taaluma ya ualimu ambapo kinaendesha kozi katika ngazi ya cheti na diploma ya ualimu.

Chuo cha Ualimu Arafah Tanga
Kozi (programu) Zitolewzao na Chuo cha Ualimu Arafah Tanga
Hapa tutaenda angazia aina ya kozi za ualimu zinazotolewa na chuo cha ualimu Arafah, chuo hiki kimejikita katika utoaji wa kozi za ualimu wa shule za msingi. Miongoni mwa kozi zitolewazo na chuo cha Arafah ni pamoja na;
- Cheti cha Msingi cha Ufundi katika Elimu ya Msingi katika ngazi ya NTA Level 4
- Cheti cha Ufundi katika Elimu ya Msingi katika ngazi ya NTA Level 5
- Diploma ya Kawaida katika Elimu ya Msingi (Huduma) katika ngazi ya NTA Level 6
- Diploma ya Kawaida katika Elimu ya Msingi (Huduma Kabla) katika ngazi ya NTA Level 6
Sifa na Vigezo vya Kujiunga na Kozi Katika Chuo cha Ualimu Arafah Tanga
Ili kuweza kujiunga na chuo cha ualimu Arafah mwombaji anapaswa awe amekidhi baadhi ya Vigezo kama vile;
- Awe amemaliza elimu ya sekondari na kupata angalau alama nne za ufaulu katika masomo husika.
- Awe na GPA isiyo pungua 2.0.
- Awe na ujuzi wa lugha ya Kiingereza
Jinsi ya Kutuma Maombi katika Chuo cha Ualimu Arafah Tanga
Ili kujiunga na kozi ya aiana yoyote katika chuo cha ualimu cha Arafah mwanafunzi anatakiwa kupitia mchakato wa utumaji maombi nja udahili. Hapa chini tutakuonyesha hatua za kufuata ili kutuma maombi yako kikamilifu ya kujiunga na kozi katika chuo cha Ualimu Arafah.
1. Kupata fomu ya maombi- hatua ya kwanza ni kupata fomu ya maombi ambayo inapatikana kwa kuingia kwenye tovuti ya chuo cha ualimu Arafah au kutembelea ofisi za chuo zilizoko mkoani Tanga kilipo chuo
2. Kujaza Fomu ya Maombi- Hatua ya pili baada ya kupata fomu ya maombi ni kuijaza fomu hiyo kwa maelekezo ya fomu kulingana na aina ya kozi unayotaka kuisoma katika chuo cha ualimu cha Arafah.
3. Kulipa Ada ya Usajili – baada ya kujaza fomu ya maombi ya usajili kabla ya kuituma kuituma unatakiwa kulipa ada ya usajili kupitia akaunti ya benki.
4. Rejesha Fomu ya Maombi – Baada ya kuamilisha kujaza fomu ya maombi na kulipia ada ya usajili sasa unaweza kuirudisha fomu hiyo chuoni ili mchakato wa udahili uanze.
Kumb; fomu ya maombi ya usajili inapaswa kurudishwa chuoni kabla ya muda wa usajli kuisha.
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na uongozi wa chuo kupitia mawasiliano tuliyoyaweka hapo chini
Simu namba: 0715120458
P. O. Box 1542, Tanga
AU Tembelea tovuti ya nacte kupitia www.nacte.go.tz/
Hitimisho
Chuo cha ualimu Arafah ni miongoni mwa vyuo bora nchini na kianatoa kozi ambazo kwa kina humuandaa mwanafunzi kuhitimu katika ubora wa hali ya juu katika ngazi ya ualimu wa shule za msingi, pia umuandaa walimu kuweza kumudu aina yoyote ile ya mazingira katika ajira yake.
Mapendekezo ya Mhariri;
2. Chuo cha Ualimu Nazareth Kilichopo Mbinga
3. Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha ADEM Bagamoyo
4. Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Arusha
5. Chuo cha Ualimu cha Waama Lutheran
6. Chuo cha Ualimu cha Moravian Mbeya
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku