Nauli ya Basi Dar Kwenda Dodoma
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Habari mwana Habrika24, niwakati mwingine tena tumekutana na katika makala hii tutaenda kuelezea juu ya nauli ya Basi Dar kwenda Dodoma na nauli ya basi Kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam. Kama hufahamu ni makampuni gani za mabasi zizazotoa huduma ya usafirishaji abairia na mizigo kutoka Dar kwenda Dodoma na Dodoma kwenda Dar basi BONYEZA HAPA kusoma.

Nauli ya Basi Dar Kwenda Dodoma
Mambo ya Kuzingatia Kusuhu Nauli Ya Basi Dar kwenda Dodoma
Inapokuja swala la kujadili nauli zitozwazo na makampuni ya usafirishaji ya mabasi kwa wasafiri wa Dar kwenda Dodoma na Dodoma kwenda Dar kunazitu vya msingi vya kuvizingatia ambavyo ndio kwa kiasi kikubwa hutoa tasmini ya msingi ya nauli hizo.
1. Daraja la Basi Husika;
Ubora wa daraja la bais pia hutoa tofauti ya nauli miongoni mwa mabasi yanayofanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, Kuna madaraja matatu ya mabasi, Daraja la juu (VIP), Daraja la kati (Luxury) na Darja la chini (ORDINARY), Utofauti wa kimadaraja pia hutoa utofauti wa bei ya nauli miongoni mwa mabasi husika.
2. Huduma zitilewazo Ndani Ya Basi
Ubora wa huduma zitolewazo ndani ya mabasi pia huchangia ongezeko au upufu wa nauli kutoka basi moja kwenda basi jingine mfano, basi linalotoa huduma ya chakula, vinywaji na hata njia za kuchaji simu haliwezi fanana na basi lisilotoa huduma kama hizo.
Nauli ya Basi Dar Kwenda Dodoma
Hapa chini tutaenda kuangazia nauli halali za mabasi yanayotoa huduma zake kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma na Dodoma kwenda Dar es Salaam
1. Mabasi ya Daraja la juu na kati (Luxury buses)
- Nauli ya basi la daraja la juu na kati (Luxury) ni Tsh. 29,000
2. Mabasi ya Daraja la Kawaida (Ordinary Level)
- Mabasi haya nauli zake huwa ni Tsh. 21,000
Huduma Zinazopatikana Ndani Ya Mabasi
Mbasi haya hutoa huduma tofauti tofauti kwa bairia wake kulingana na daraja la basi husika. Mfano mabasi ya daraja la juu(Luxuly) hutoa huduma kama vile,
- Huduma ya Internet kwa njia ya Wifi
- Huduma ya chakula
- Huduma ya Vinywaji
- Huduma ya kuchaji simu
- Na kunahata mabasi yanahuduma ya Choo ndani
Hivyo basi tunaweza hitimisha kwa kusem kua nauli za mabasi ya kutoka Dar kwenda Dodoma huwekwa au hupangwa kutokana na ubora wa basi husika na huduma zitolewazo na basi hilo.Kwahiyo nauli tulizoziweka hapo si kila wakati zitakua hivyo zinaweza kupungua au kuongezeka kutokana na sababu mbali mbali na kampuni husika ya basi.
Machaguo ya Mhariri;
1. Mabasi ya Dar Kwenda Dodoma Kila siku
2. Nauli Za Mabasi Ya Dar To Morogoro
3. Kampuni Za Mabasi Ya Dar To Morogoro
4. Mshahara wa Rais wa Tanzania
5. Mshahara wa Mbunge Wa Tanzania Na Marupurupu Yake