WALIO CHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2025

_________________________________________________

MATANGAZO YA AJIRA  KILA SIKU BOFYA HAPA

_________________________________________________

NOTES ZA KIDATO CHA 1 HADI 6 BOFYA HAPA

_________________________________________________

MAGROUP MAPYA YA WHATSAAP BOFYA HAPA

_________________________________________________
MATANGO YA AJIRA BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

Majina Walioitwa Kwenye Usaili Chuo MUST May 2025

Filed in Usaili by on May 17, 2025 0 Comments

Makamu Mkuu wa Chuo kwa niaba ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 22-05-2025 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
2. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
3. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
4. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
5. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI, Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
6. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
7. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
8. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
9. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
10. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya
tangazo husika.
11. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
12. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili

Majina Walioitwa Kwenye Usaili Chuo MUST May 2025

MATANGO YA AJIRA BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA
MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *