Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo (SUA) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa
kuendeshwa kuanzia tarehe 20-11-2025 hadi 21-11-2025 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji
kazi watakaofaulu usaili huo. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo
yafuatayo:-
1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo
usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
2. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask).
Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.
• Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga
kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au
barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji anachotoka.
4. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI,
Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za nafasi
husika.
5. Wasailiwa watakaowasilisha ‘Testimonials, Provisional Results, Statement of results’, hati za matokeo
za kidato cha IV na VI (‘form IV and form VI results slips’) HAVITAKUBALIWA NA
HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
6. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi
vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
7. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi. Aidha kila msailiwa anapaswa kuhudhuria
usaili akiwa na mavazi nadhifu na yenye staha kulingana na Waraka wa mavazi.
8. Kwa wasailiwa waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na
Mamlaka husika (kama TCU, NACTVET au NECTA). Wasailiwa wa kada zinazohitaji ‘GPA’ waliosoma
nje ya Tanzania wawasilishe cheti cha ukokotozi wa GPA kutoka TCU.
9. Wasailiwa ambao hawajaona majina yao kwenye tangazo hili wanapaswa kuingia kwenye akaunti zao
za ‘Ajira Portal’ na kuona sababu za kutokuitwa kwao ili wasikose fursa wakati mwingine.
10. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba
ya usaili. Aidha wasailiwa watakaofanya usaili wa mchujo kwa njia ya Mtandao wanapaswa kukumbuka
barua pepe (email address) na nywila (password) zao wanazotumia katika mfumo wa Ajira Portal.
11. Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo
cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
Walioitwa Kwenye Usaili Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) November 2025
Bonyeza Hapa Kudownload PDF ya Majina
