Timu Zilizofuzu Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2025
Habari mwanamichezo wa Kisiwa24 Blog karibu katika blog yako pendwa na katika kurasa hii ya kimichezo tutaenda kukuonyesha orodha ya vilabu vilivyofanikiwa kuwea kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika kwa msimu wa 2024/2025.
Hatua ya Makundi Klabu bingwa Afrika
Baada ya hatua ya mtoano kumalizika na timu kutoka mataifa 16 kuweza kufanikiwa kuingia katika hatua ya makundi shirikisho la mpira wa miguu Afrika CAF liliweza kupanga magundi ya michuano hiyo na mnamo November 26, 2024 michuano hiyo iliweza kuanza kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali
Jumla ya timu 16 ziliweza kupambania nafasi ya kuweza kusonga mble katika michuano hiyo iliyoweza kuendeshwa kwa mizunguko sita huku kila kundi likiwa na jumla ya timu 4. Timu kwenye kila kundi katika hatua hii iliweza kucheza michezo 6 huku michezo 3 ikiwa ya nyumbani na michezo 3 ya ugenini.
Timu Zilizofuzu Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2025
CAF iliweza kupanga jumla ya makundi 4 ambapo kila kundi liliundwa kwa timu 4 na kulingana na taratibu za michuano hii ya CAF champions League kila kundi litatoa timu 2 kuingia katika hatua inyofuata ya robo fainali.
Hapa chini tutaenda kukuonyesha timu zilizoweza kufuzu hatua ya robo fainali CAF Champions League 2025 kwa kuzingatia makundi yalieyoweza kupangwa
1. Timu zilizofudhu Robo Fainali CAF Champions League Kundi A
Kundi A limeundwa na timu 4 ambazo ni;
- Al-Hilal
- MC Alger
- Young Africans
- TP Mazembe
Hadi sasa kunajumla ya michezo 5 ambayoimesha chezwa na timu ya Al-Hilal tayariimesha fuzu kuelekea katika hatua ya robo fainali ya michuano ya CAF Champions League kwani hadi sasa imejikusanyia jumla ya pointi 10 ikisubili mchezo wa mwisho ambao hata ikifungwa na mshindani wake akishinda atabaki katika nafasi ya 2.
Timu zilizobakia katika kinyang’anyilo cha kufuzu hatua ya robo fainali katika kundi hili ni klabu ya MC Alger na klabu ya Yanga. kulingana na msimamo wa kundi hili klabu ya Yanga iko katika nafasi ya 3 ikiwa na pointi 7, huku klabu ya MC Alger kiwa katika nafasi ya 2 ikiwa na pointi 8.
Mchezo wa mzunguko wa mwishi utazikutanisha Yanga vs MC Alger jijini Dar es Salaam , mchezo huu ndio utakao toa majibu ya klabu gani itaenda kuungana na Al Hilal kuelekea robo fainali.
Msimamo wa Kundi A Baada ya Roundi ya 5
Rank | Club | MP | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
1 | Al-Hilal | 5 | 3 | 1 | 1 | 6 | 3 | 3 | 10 |
2 | MC Alger | 5 | 2 | 2 | 1 | 4 | 2 | 2 | 8 |
3 | Young Africans | 5 | 2 | 1 | 2 | 5 | 6 | -1 | 7 |
4 | TP Mazembe | 5 | 0 | 2 | 3 | 3 | 7 | -4 | 2 |
2. Timu zilizofudhu Robo Fainali CAF Champions League Kundi B
Kundi B ilimeindwa na timu zifuatazo;
- AS FAR
- Mamelodi Sundowns
- Raja CA
- Maniema Union
Katika kundi hili pia jumla ya michezo 5 imesha fanyika kwa kila timu na hadi sasa AS FAR imesha jikatia tiketi ya kuweza kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hii ya CAF Champions League kwa msimu wa 2025 ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi 9 katika michezo 5 ikisubili mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Timu ya pili itakayoenda kujiunga na AS FAR kwenye hatua ya robo fainali itatengemea na matokeo ya mchezo wa roundi ya mwisho kwa ni Mamelodi Sundowns ina jumla ya pointi 8 ikiwa katika nafasi ya 2 na Raja CA inajumla ya pointi 5 ikiwa katika nafasi ya 3. Kama Mamelodi Sundowns itashinda mche au kutoa sare mchezo wake wa mwisho itakua imefuzu kwenda robo fainali pia kwa upande wa Raja CA ikishinda mchezo wake wa mwisho kwa ushindi wa goli zaidi ya 3 na Mamelodi Sundowns kupoteza mchezo wake basi itakua imefudhu hatua ya robo fainali kwa utofauti wa magoli.
Msimamo wa Kundi B Baada ya Roundi ya 5
Rank | Club | MP | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
1 | AS FAR | 5 | 2 | 3 | 0 | 7 | 3 | 4 | 9 |
2 | Mamelodi Sundowns | 5 | 2 | 2 | 1 | 4 | 3 | 1 | 8 |
3 | Raja CA | 5 | 1 | 2 | 2 | 3 | 5 | -2 | 5 |
4 | Maniema Union | 5 | 0 | 3 | 2 | 3 | 6 | -3 | 3 |
3. Timu zilizofudhu Robo Fainali CAF Champions League Kundi C
Katika kundi C pia kulikua na jumla ya timu 4 ambazo hadi sasa zimecheza jumla ya michezo mitano.
- Orlando Pirates
- Al Ahly
- CR Belouizdad
- Stade d’Abidjan
Hadi kufikia sasa kwenye kunci C tayari timu mbili zimesha fuzu kwenda robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika timu hizo ni
- Orlando Pirates – ikiwa na jumla ya pointi 11 kwenye nafasi ya 1 ya msimamo wa kundi
- Al Ahly – Ikiwa na pointi 10 katika nafasi ya 2 kwenye msimamo wa kundi
Katika nafasi ya tatu ya msimamo wa kundi C inashikwa CR Belouizudad ikiwa na pointi 6. Mchezo wa mwishi Orlando Piretes itaminyana na Al Ahly huku wote 2 wakiwa tayari wamesha fuzu kuelekea hatua ya robo fainali.
Msimamo wa Kundi B Baada ya Roundi ya 5
Rank | Club | MP | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
1 | Orlando Pirates | 5 | 3 | 2 | 0 | 8 | 3 | 5 | 11 |
2 | Al Ahly | 5 | 3 | 1 | 1 | 13 | 5 | 8 | 10 |
3 | CR Belouizdad | 5 | 2 | 0 | 3 | 5 | 10 | -5 | 6 |
4 | Stade d’Abidjan | 5 | 0 | 1 | 4 | 4 | 12 | -8 | 1 |
4. Timu zilizofudhu Robo Fainali CAF Champions League Kundi D
Kundi D pia kama ilivyokua kwneye makundi mengine lilikua na jumla ya timu nne amabazo ni;
- ES Tunis
- Pyramids
- Sagrada Esperança
- Djoliba
Katika kundi D tayari timu 2 zimesha pata tiketi ya kuweza kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya CAF Champions League huku timu mbili zikiwa tari zimeaga mashindano zikisubili tu kumalizia roundi ya 6 ya michuano hiyo. Timu zilizoweza kufuzu hatua inayofuata ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika 2025 kutoka kundi D ni pamoja na.
- ES Tunis – Iliyoko katika nafasi ya 1 ikiwa na pointi 10 na magoli ya utofauti 6
- Pyramids – Ikiwa katika nafasi ya 2 ikiwa na pointi 10 na magoli ya utofauti 4
Upande wa timu zilizobakia kwa nafasi ya 3 inashikiliwa na Sagrada Esperanca ikiwa na pointi 5 na katika nafasi ya 4 iko Djoliba ikiwa na pointi 2.
Msimamo wa Kundi B Baada ya Roundi ya 5
Rank | Club | MP | W | D | LL | GF | GA | GD | Pts |
1 | ES Tunis | 5 | 3 | 1 | 1 | 8 | 2 | 6 | 10 |
2 | Pyramids | 5 | 3 | 1 | 1 | 8 | 4 | 4 | 10 |
3 | Sagrada Esperança | 5 | 1 | 2 | 2 | 2 | 6 | -4 | 5 |
4 | Djoliba | 5 | 0 | 2 | 3 | 0 | 6 | -6 | 2 |
Orodha ya Timu Zilizoweza Kufudhu Hatua ya Robo Fainali CAF Champions League
Hapa chini ni jumla ya timu ambazo tayari zimesha weza kufuzu kwenda hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika hadi sasa
1. Al-Hilal
2. AS FAR
3. Orlando Pirates
4. Al Ahly
5.ES Tunis
6. Pyramids
Hitimisho
Hadi kufikia wakati huu ni jumla ya michezo 5 amabyo imesha chezwa na katika kila kundi tayari kunatimu ambazo zimeshaweza kufuzu kwenda hatua ya robo fainali ya michuano hii ya CAF Champions League kwa msimu wa 2025.
Kwenye kundi C na D tayari timu 2 zimesha fuzu bado kundi A na kundi bi linasubilia uwamuzi wa mchezo wa roundi ya 6 ili kupata timu ya 2 kwa kila kundi.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. RATIBA ya Mechi za Simba Mwezi Januari 2025
2. RATIBA ya Mechi za Yanga Mwezi Januari 2025
3. Ratiba ya Mechi Za Leo Ligi Mbalimbali