Close Menu
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

MAJINA Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs

December 6, 2025

NAFASI za Kazi Za Mkataba Wizara Ya Maliasili Na Utalii

December 6, 2025

NAFASI za Kazi Kutoka Vodacom Tanzania

December 6, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Kisiwa24Kisiwa24
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala
Subscribe
Kisiwa24Kisiwa24
Home»Ajira»NAFASI Mpya 5476 za Mafunzo ya Ufundi Stadi Katika Fani Mbalimbali
Ajira

NAFASI Mpya 5476 za Mafunzo ya Ufundi Stadi Katika Fani Mbalimbali

Kisiwa24blogBy Kisiwa24blogDecember 6, 2025No Comments3 Mins Read
Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Reddit Telegram Email
NAFASI Mpya 5476 za Mafunzo ya Ufundi Stadi Katika Fani Mbalimbali
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano inatekeleza Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi inayolenga kuwezesha nguvu kazi ya Taifa kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili kumudu ushindani katika soko la ajira.

Ofisi imeingia makubaliano na vyuo 46 vinavyotoa mafunzo ya ufundi stadi ambavyo vimesajiliwa na Mamlaka husika kutoa mafunzo katika fani mbalimbali zikijumuisha ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo, ufundi bomba, uashi, useremala, uchomeleaji na uungaji vyuma, upakaji rangi na maandishi ya alama, upishi, utengenezaji wa vipuri vya mitambo, ufundi magari na mitambo, umeme wa majumbani na viwandani, umeme wa magari, huduma za hoteli na utalii, ukataji madini na ufundi vyuma.

Ofisi hiyo inapenda kuwatangazia vijana wa kitanzania wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 wanaopenda kujiunga na mafunzo katika mojawapo ya fani zilizoorodheshwa hapo juu wafike katika Vyuo vya Ufundi Stadi vya Mikoa na Wilaya vilivyopitishwa na Serikali ili kuchukua fomu ya kuomba kujiunga na mafunzo.

Serikali itafadhili ada ya mafunzo kwa asilimia 100. Mwanafunzi/ Mzazi/ Mlezi atagharamia gharama nyingine zikijumuisha nauli ya kwenda chuoni na kurudi nyumbani.

Mafunzo yataanza tarehe 26 Januari, 2026 na yatakua ya kutwa.

Mwombaji anashauriwa kuomba mafunzo haya katika chuo kilicho katika Mkoa anaoishi.

Orodha ya Vyuo imeambatanishwa hapa chini kwenye PDF.

Vituo vilivyokubalika na Serikali kutoa mafunzo hayo na fani zake
vimeambatishwa pia.

Maombi yawasilishwe kuanzia tarehe 05 hadi 19 Desemba, 2025 yakiambatana na nyaraka zifuatazo:

  • Barua ya maombi ya mafunzo.
    Nakala ya Cheti cha kuzaliwa.
  • Nakala ya Cheti cha elimu uliyohitimu.
  • Kitambulisho cha uraia kadi ya mpiga kura (Kwa wenye miaka 18 na kuendelea).
  • Barua ya utambulisho kutoka Ofisi ya Serikali ya Mtaa/Kijiji anakoishi mwombaji na
  • Picha nne za pasipoti (ziandikwe majina matatu ya mwombaji kwa nyuma).

Sifa za kujiunga na mafunzo haya ni:

  • Elimu ya msingi au zaidi kwa fani za ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo, ufundi bomba, ujenzi, useremala, uchomeleaji na uungaji vyuma, upakaji rangi na maandishi ya alama.
  • Elimu ya kidato cha nne na kuendelea kwa fani nyingine zilizobaki zikijumuisha fani ya utengenezaji wa vipuri vya mitambo, ufundi magari, umeme wa majumbani na viwandani, umeme wa magari na umeme wa jua (solar).
  • Awe Mtanzania.
  • Awe na umri kati ya miaka 15-35 na
  • Awe mwenye afya njema.

Vijana Wenye Ulemavu wanasisitizwa kuomba fursa hizi na watapewa kipaumbela katika nafasi za mafunzo haya.

Maombi yachukuliwe na kuwasilishwa kwenye vyuo vilivyo katika mkoa wako ambavyo vimekubaliwa na Serikali kutoa mafunzo haya.

Watakaokidhi vigezo na sifa tu ndio watakaochanguliwa.

Imetolewa na;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA WAZIRI MKUU
KAZI, AJIRA NA MAHUSIANO.
DODOMA

VYUO VILIVYOPENDEKEZWA KUTOA MAFUNZO YA UANAGENZI AWAMU YA NANE – MWAKA WA FEDHA 2025/26.

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA TANGAZO

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
Previous ArticleNafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
Next Article NAFASI za Kazi Kutoka Vodacom Tanzania
Kisiwa24blog
  • Website
  • Tumblr

Related Posts

Ajira

MAJINA Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs

December 6, 2025
Ajira

NAFASI za Kazi Za Mkataba Wizara Ya Maliasili Na Utalii

December 6, 2025
Ajira

NAFASI za Kazi Kutoka Vodacom Tanzania

December 6, 2025
Add A Comment
Leave A Reply Cancel Reply

Recent Posts

  • MAJINA Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs
  • NAFASI za Kazi Za Mkataba Wizara Ya Maliasili Na Utalii
  • NAFASI za Kazi Kutoka Vodacom Tanzania
  • NAFASI Mpya 5476 za Mafunzo ya Ufundi Stadi Katika Fani Mbalimbali
  • Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ngara

Recent Comments

No comments to show.
Demo
Top Posts

Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

December 3, 2025286 Views

MAJINA Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs

December 6, 2025277 Views

NAFASI za Kazi Za Mkataba Wizara Ya Maliasili Na Utalii

December 6, 2025271 Views
Stay In Touch
  • Facebook
  • YouTube
  • TikTok
  • WhatsApp
  • Twitter
  • Instagram
Latest Reviews

Subscribe to Updates

Get the latest tech news from FooBar about tech, design and biz.

Demo
© 2025 Kiswa24 Blog. Designed by Kisiwa24.

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.