MFUMO wa Maombi ya Kazi Tume ya Utumishi wa Mahakama 2025
MFUMO wa Kutuma Maombi ya Kazi Tume ya Utumishi wa Mahakama,(Judicial Service Commission – Job Application portal) 2025.
Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo huru kilichoundwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kusimamia masuala ya ajira na maendeleo ya watumishi wa Mahakama. Tume hii ina jukumu la kuhakikisha kuwa ajira, mafunzo, kupandishwa vyeo, pamoja na nidhamu ya watumishi wa Mahakama vinafanyika kwa haki, uwazi, na kwa kuzingatia misingi ya utawala bora. Kwa kufanya hivyo, Tume husaidia katika kuimarisha ufanisi wa huduma za kimahakama na kuleta imani kwa wananchi kuhusu mfumo wa utoaji haki nchini.
Majukumu ya Tume hayaishii tu kwenye kusimamia ajira bali pia huchukua hatua za kiutawala katika kushughulikia malalamiko dhidi ya watumishi wa Mahakama, kuhakikisha uwajibikaji na maadili ya kazi yanafuatwa. Pia hufanya kazi kwa karibu na Mahakama ya Tanzania, Ofisi ya Jaji Mkuu na taasisi nyingine za kisheria ili kuhakikisha mfumo wa Mahakama unakuwa na rasilimali watu wenye weledi na maadili. Kwa ujumla, Tume ya Utumishi wa Mahakama ni mhimili muhimu katika kuhakikisha haki inatendeka kwa wakati na kwa usawa.
Jinsi ya Kujisajiri kwenye Mfumo wa Maombi ya Ajira Tume ya Utumishi wa Mahakama
1. Tembelea tovuti rasmi ya tume ya utumishi wa mahaka
2. Bonyeza register kama ndio mara ya kwanza kuingia kwenye mfumo
3. Jaza taarifa muhimu kama vile
- Jina lako kamili
- Email address yako
- Neno siri (Pasword)
Kisha bonyeza Register
, hadi hapo utakua tayari umeingia kwenye mfumo wa Maombi ya kazi Tume ya Utumishi wa Mahakama.
The best way to succeed my successful 💯