WALIO CHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2025

_________________________________________________

MATANGAZO YA AJIRA  KILA SIKU BOFYA HAPA

_________________________________________________

NOTES ZA KIDATO CHA 1 HADI 6 BOFYA HAPA

_________________________________________________

MAGROUP MAPYA YA WHATSAAP BOFYA HAPA

_________________________________________________
MATANGO YA AJIRA BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

Majina Walioitwa Kwe Usaili Utumishi 19 May 2025

Filed in Usaili by on May 19, 2025 0 Comments

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Tume ya Ushindani (FCC), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Chuo cha Maji (WI), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Makumbusho ya Taifa la Tanzania (NMT), Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), MDAs & LGAs, Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Chuo cha Sukari cha Taifa (NSI) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 24-05-2025 hadi 28-06-2025 hatimaye
kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.

2. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)

3. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;

4. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka.

5. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.

6. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.

7. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.8. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.

9. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTVET au NECTA)

10. Waombaji kazi ambao hawajaona majina yao kwenye tangazo hili wanapaswa kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal na kuona sababu za kutokuitwa kwao ili wasikose fursa wakati mwingine.

11. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti
vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.

12. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili.

13. Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi

Majina Walioitwa Kwe Usaili Utumishi 19 May 2025

MATANGO YA AJIRA BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA
MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *