Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kinapenda kuwataarifu waombaji kazi mbalimbali
waliofanya usaili tarehe 5 Desemba, 2025 kuwa, majina ya waombaji kazi waliofaulu usaili
huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili.
Waombaji waliofaulu usaili watatakiwa kukamilisha taratibu mbalimbali za ajira kwa kufika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jengo la Utawala, Ofisi ya Masjala, Chumba Na.
315 siku ya Jumatatu, tarehe 15 Desemba, 2025 kuanzia saa tatu kamili asubuhi,
wakiwa na nyaraka zilizoainishwa katika tangazo hili ili ziweze kuhakikiwa kabla ya
kupewa barua za ajira.
Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili, watambue kuwa hawakupata
nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine pindi nafasi za kazi
zitakapotangazwa.
Nyaraka za kuwasilisha ni kama ifuatavyo:
- Vyeti halisi (Original Certificates and Transcripts) na nakala mbili za vyeti hivyo
ambazo zimethibitishwa na Mamlaka za kisheria (certified by - Advocate/Magistrate) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea;
- Cheti cha kuzaliwa;
- Nakala ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA); na
- Picha ndogo nne za rangi (four coloured passport size photographs)
MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM
Bonyeza Hapa Kudownload PDF ya Tangazo

