Majina Wailioitwa Kwenye Usaili Taasisi Mbalimbali December 2024
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI),, Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 03-12-2024 hadi 10-12-2024 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.
Mambo Muhimu ya Kuzingatiwa na Wasiliwa
Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili ni muhimu sana kuzingatia mambo yafuatayo ili kuweza kujihakikishia ya kua unafanya usaili kama ulivyopangwa na kujhakikishia nafasi yako ya kupata kazi;
1. Siku ya Kufanyika kwa Usaili
- Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
2.Uvaaji wa Barkoa Kwa Wasaili
- kila msailiwa anaitarajia kuudhulia usaili anatakiwa kufika eneo la usaili akiwa amevaa barakoa kama njia ya kujikinga na magonjwa ambukiziKila (Mask)
3. Ubebaji wa Kitambulisho
Kila msailiwa atakayefika kituo cha usaili ni lazima awe na kitambulisho kinacho tambulika kwa ajili ya utambuzi wa msailiwa, kama vile Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka.
5.Vyeti
Wasailiwa wote pindi wanapofkwenda katika kituo cha usaili ni lazima wabebe vyeti vyao halisi kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
7.Gharama Wakati wa Usaili
- Gharama zote zitakazokuwepo wakati wa usaili basi msailiwa tajitegemea kwa gharama hizo kama vile Chakula, Usafiri na Malazi.
8 .Waombaji Waliosoma Nje ya Tanzania
- Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
9. Waombaji Wasio Ona Majina yao Katika Tangazo Hili
- Kwa waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
11. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
12. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili.
8. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.