Kampuni Za Mabasi Ya Dar To Morogoro | Mabasi ya Moro to Dar
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Mabasi ya Dar to Morogoro, Safari ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ni mojawapo ya safari maarufu nchini Tanzania, ikihusisha umbali wa takriban kilomita 194. Mabasi ni njia maarufu ya usafiri kwa safari hii kutokana na unafuu wake na urahisi wa upatikanaji. Katika makala hii, tutachunguza nauli, ratiba, na huduma zinazotolewa na mabasi kati ya miji hii miwili.
Habari ya waka huu, kama ilivyokua kawaida yetu leo tunakuletea aina ya mabasi yoteyanayofanya safari zake kutoka Dar kwenda Morogoro na Morogoro to dar kila siku. Safari za dar kwenda Morogoro zimekua za kawaida kabisa baina ya wakazi wa mikoa hii miwili, kumekua na safari nyingi zinazo fanywa na wakazi wa mikoa hii kibiashara, kusarimia, kutembea tu na hata kwa wanafunzi, hivyo basi kupelekea nyenzo tofauti tofauti za usafiri kuweza kuanzishwa.

Njia Za Ushafiri Dar to Morogoro
Kulinga na na mwingiliano wa wakazi wa Mikio hii miwili ya jirani kabisa kumekua na aina mbili kuu za usafi zinazounganiasha mikoa hii
1. Njia ya magari, njia hii inahusisha gari ndogo na gari kubwa
2. Njia ya Reli, njia hii inahusisha usafiri wa treni na kwasasa kumekua na ongezeko la usafiri wa treni ya SGR treni ya umeme, Kuhusu usafiri huu BONYEZA hapa kusoma
Usafiri Wa Mabasi Dar To Morogogro
Hapa tutaenda angazi juu ya usafiri wa mabasi yanyofanya safari zake kutoka Dar to Morogoro na Morogoro kwenda Dar es salaam, Kumekua na kampuni kadhaa ambazo zimekua zikitoa huduma zake za usafirishaji wa watu namizigo yao kutoka Dar to morogoro na Morogoro to Dar.
Na asilimia ya wasafiri walio wengi hupenda usafiri huu wa mabsi kwani umeonekana kua usafiri wa uhakika na ni rahisi sana upatikanaji wake pi hata upande wa gharama za nauli ni nafuu kidogo. Usafiri wa Dar kwenda Morogoro hupatikana wakati wowote ule kuanzia saa 11:oo alfajiri hadi saa 10:00 usiku utakapo fika stendi.
Aina Ya Mabasi Yanayofanya Safari Zake Dar to Morogoro
Kuna makampuini ya ainatofauti tofauti yanayofanya safari zake kutoka Dar Kwenda Morogoro na Morogoro Kwenda Dar, hapa chini Tumeweka miongoni mwa kampuni za mabasi hayo
Abood Bus Servise
Hii ni kampuni ya mabasi yenye masikani yake mkoani morogoro inatoa huduma ya usafirishaji abiria kutoka dar to morogoro na morogoro to dar es salaam kila siku.

Bm Coach
BM Coach pia ni miongoni mwa kampini yenye mabasi bora kabisa yanayotoa huduma zake za usafirishaji wa abiria na mizigo yao kila siku kutokea stendi ya Magufuri jijini dar es salaam maeneo ya mbezi kuelekea mkoani Morogoro katika stendi ya Msamvu.

New Force
New force ni kampuni mpya ya mabasi ambayo kwa mara ya kwanza ilianza kufanya safari zake kutok dar kwenda Morogoro. Baada ya miezi kadhaa kupita iliongeza wigo wake wa usafirishaji hadi kufikia kuanza safari zake za mabasi ya Dar to Morogoro na Morogoro to Dar.
Kampuni hii inamabasi mazuri na yenye ubora wa hari ya juu, inatoa huduma bora na za uhakika kwa ushindani wa usafiri wa mabasi ya Dar to Morogoro New force imeweza kufukuzana na makampuni makubwa na makongwe kama vile Abood Bus searves na BM Coach

Happy Nation Bus Service
Ukiachilia mbali makampuni tulioyataja hapo juu pia kunakampuni mashuhuri la mabasi ya dar to morogoro linalofahamika kwa ubora na ufahari wa mabasi yake la Happy Nation, Kampini hii ya mabasi pia ni miongoni mwa makampuni yanayotoa huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo yao kutokea Dar kwenda Morogoro na Morogoro kwenda Dar kila siku.
Wanatoa huduna ya Luxury kwa takribani mabasi yote yafanyayo safari zake kutoka Dar to Morogoro na Morogoro to Dar.

Huduma Za Muhimu Zinazopatika kwenye Mabasi ya Dar to Morogoro
Kulingana na urefu/umbali wa safari kutoka dar kwenda morogoro na morogoro to Dar kampuni hizi za mabasi zimeweza kuboresha huduma zake kwa kutoa huduma mbali mbali kwa wateja wake ndani ya mabasi hayo ili kufanya safari kuwa ya kufurahisha na kuburudisha bila kuwachsha abiria wake.
Mfano au miongoni mwa huduma zitolewazo ndani ya mabasi hayo yawapo safarini ni pamoja na;
Huduma ya TV;
Mabasi haya yamefungea huduma ya runinga ambapo abilia wanapata fursa ya kutazama runinga wakiwa safarimi. Watoa huduma huweka nyimbo za video au tamthiliya ili kuwaburudisha abiria wakati wote wa safari,
Huduma ya Wifi
Mbasi haya hasa yale ya luxury huwa yanatoa pia huduna ya mtandao wa internet kwa njia ya wifi, hii humpa fursa mtumiaji wa simu janja aliyeko ndani ya basi kama abiria kufurahia kuperuzi mtandaoni akiwa safarini, hii pia inamfanya abiria kuto choshwa na safari wakati wote.
Huduma ya Kuchaji Simu
Pia nyuma ya siti za mabasi haya zimewekew vifaa vya kuchajia simu hivyo abiri anapaswa tu kua na kifaa cha kuchajia simu yake waya aina ya USB. Kwa huduma hii abilia hata kua ana hofu ya simu yake kuishiwa au kupungukiwa na chaji pindi awapo safarini.
Huduma ya Vitafunwa
Si kila basi hutoa huduma hii ya vitafunwa na vinywaji, lakini baadhi ya mabasi yanayofanya safari zake kutoka Dar to Morogoro au Morogoro to Dar hasa yale ya daraja la kwanza (Luxury) hutoa huduma hii.
Abiria ndani ya basi hizi hupew vitafunwa kama vile biskuti na vinywaji kam vile maji na soda.
Hivyo basi kama wewe ni msafri wa kutoka dar es salaam kwenda Morogoro au Morogoro kwenda Dar es salaam natumaini umejifunza kitu kutoka katika makala hii.
Kutoka Kwa Mhariri;
1. Mshahara wa Rais wa Tanzania