Jinsi Ya Kutumia Kadi Ya Mwendokasi, Habari mwana Dar es Salaam, karibu katika makala hii ambayo itaenda kukupa maelekezo ya kuhusu kadi ya malipo ya usafiri wa mwendokasi. Wakala Wa Mabasi Yaendayo Haraka Mkoa Wa Dar es Salaam (DART) imeanzisha kadijanja itakayotumika kufanya malipo ya usafiri wa mbasi ya mwendokasi ikiwa na lengo la kurahisisha huduma za kiusafiri ndani ya DART.
Fahamu Kuhusu Wakala Wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART)
Wakala Wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa mujibu wa Tangazo la serikali No. 120 la tarehe 25 Mei 2007 chini ya sheria No. 30 ya Wakala za Serikali ya mwaka 1997 na marekebisho yake. Jukumu kuu la DART ni kuanzisha na kuendesha mfumo wa Usafiri wa Mabasi Yaendayo katika mkoa wa Dar es Salaam.
Jinsi ya Kupata Kadi ya Mwendokasi
Kama wewe ni mtumiaji wa usafiriwa mabasi ya mwendokasi ili kupata kadi hii ya mwendokasi itakupasa uweze kutembelea vituo vya mwendokasi vilivyopo jijini Dar es Salaam na kulipia kiasi cha Tsh 500.

Kiwango Cha Kuweka Fedha Kwenye Kadi ya Mwendokasi
Dadi hii huwekwa fedha ambayo ndio hutumika katika kufanya malipo ya nauli zako pindi unapotaka kutumia usafiri wa mwendokasi. Hapa tunakuwekea kiwango cha chini na cha juu cha kuweka pesa katika kadi yako ya mwendo kasi.
- Kiwango Cha chini Cha kuweka Pesa ni Tsh 1,000
- Kiwango cha juu cha kuweka pesa ni Tsh. 90,000
Hivyo kumbe unapotaka kuweka pesa lazima iwe kunzia shilingi elfu 1 na unaweza kuweka hadi shilingi elfu tisini za kitanzania.
– Unapoitaji kuongeza salio katika kadin yako unaweza kufanya hivyo kupitia simu yako kwa mitandao ya simu kama vile
- Tigo – Bonyeza
- Airtel – Bonyeza
- Vodacom – Bonyeza
- Halotel – Bonyeza
Lakini pia unaweza kuweka pesa katika kadi yako ya mwendo kasi kwa njia zifuatazo
- Benki
- Wendokasi App
- Kwa kutembelea vituo vya Mwendokasi
Jinsi ya Kutumia kadi ya Meondokasi
Hapa chini tunaenda kuangazia sasa jinsi ya kuweza kutumia kadi ya usafiri wa mabasi yaendayo kasi katika jiji la Dar es Salaam (Mabasi ya Mwendokasi).Ili kuweza kutumia kadi hii tafadhari fuata hatua zifuatazo;
- Ukifika kituoni chukua kadi yako na weka kwenye geti la kufanyia malipo kwa njia ya kadi hadi utakapoona mshale wa rangi ya kijani utakaoruhusu kuendelea, baada ya mshaele huo kuonekana hapo utakua tayari umefanya malipo na kuendelea na safri yako na salio la nauli litakuwa limekatwa moja kwa moja kutoka kwenye kadi yako ya mwendokasi.
Mambo ya muhimu kuhusu Kadi ya Mwendokasi
- Kadi ya mwendokasi haitumiki kufanya malipo ya ainayoyote ile zaidi ya malipo ya safari za mwendokasi.
- Mara baada ya kuweka kadi kwenye geti la kufanya malipo la mwendokasi na kuthibitishwa basi salio litakatwa kwenye kadi hapo hapo.
- Hata pale Kadi ya Mwendokasi inapotumika pasipo uwepo wa mtandao, salio lililopo katika Kadi litatolewa pasipo kuchelewa sehemu itakapokuwepo kadi hiyo.
Mambo ya Kuzingatia Uwapo Ndani ya Kituo Cha Mwendokasi
- Pindi uwapo katika Kituo cha Mabasi Yaendayo Haraka, subiri basi lisimame katika jukwaa la kupandia.
- Hkikisha unapo panda basi unaingia ndani kabisa na sio kukaa mlangoni
- Kama wewe si abiria mwenye mahitaji maalumu tafadhari usikae kwenye viti vya watu wa mahitaji maalumu kama vile walemavu, wajawazito na wazee.
- Ondoa wazo la kugombania mabasi kwani yako mengi sana
Jinsi Ya Kurudisha Kadi ya Mwendokasi Iliyopotea Au Kuharibika
Kama umepatwa na changamoto ya kuharibu kadi yako ya mwendokasi au kupoteza basi usijiali fanya yafuatayo ili kuirudisha,
- Tembela kituo cha mabasi ya mwendokasi ukiwa na Taarifa zote zilizotumika kusajiria kadi iliyopotea au kuharibika
- Lipia kiasi cha Tsh. 500 ili kuomba kurudishwa kwa kadi
- Baada ya kukamirisha taratibu za kurudisha kadi subili siku 7 za kazi kiasi kilichokuwepo kwenye kadi ya awali kuhamishiwa kwenye kadi mpya
- Sasa unaweza kutumia kadi yako mpya ikiwa na taarifa zako zote za kadi iliyo pita.
Hitimisho
Wakala ya Mabasi Yaendayo Haraka (DART) imethibitisha kua maendeleo ya teknolojia yanayokua kwa kasi yanaweza kua na manufaa ya kutosha hata katika sekta ya usafiri kwani huduma hii ya kutumia kadi ya malipo ya usafiri wa mwendokasi yamekua na umuhimu mkubwa sana kama vile kuokoa muda, kuto kutembea na pesa.