
Mamlaka ya Serikali Mtandao
Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-Government Authority – e-GA) ni taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa lengo la kuratibu, kusimamia na kuendeleza matumizi ya TEHAMA katika taasisi za serikali ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Kupitia mamlaka hii, serikali inalenga kuhakikisha kwamba taasisi zote za umma zinatumia mifumo ya kidigitali inayowasiliana kwa ufanisi, inayojali usalama wa taarifa, na inayopunguza gharama za uendeshaji. e-GA pia ina jukumu la kutoa miongozo, viwango na usaidizi wa kitaalamu kwa taasisi mbalimbali za umma kuhusu matumizi bora ya teknolojia ya habari na mawasiliano.
Kwa kutumia huduma na miundombinu ya kisasa kama vile Government e-Payment Gateway (GePG), Government Mailing System (GMS), na Data Center, e-GA imefanikiwa kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi serikalini. Aidha, mamlaka hii inahakikisha kuwa mifumo ya serikali inalindwa dhidi ya mashambulizi ya kimtandao kupitia huduma zake za usimamizi wa usalama wa taarifa. Kwa ujumla, e-GA ni mhimili muhimu katika safari ya Tanzania kuelekea serikali ya kidigitali, yenye uwezo wa kutoa huduma bora, za haraka na zinazozingatia mahitaji ya wananchi wa karne ya 21.
NAFASI 11 za Kazi Mamlaka ya Serikali Mtandao July 2025
Ili luweza kusoma nafasi zilizopo, vigezo na njia ya kutuma maombi tafadhari bonyeza linki hapo chini
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA TANGAZO