JINSI ya Kutumia Kadi Ya GUSA AzamPesa,FAHAMU kuhusu Azam Pesa pamoja na Makato yake, Karibu katika makala hii itayokupa mengi kuhusu AzamPesa kama vile Jinsi ya kutumia AzamPesa, jinsi ya kujiunga na AzamPesa, Huduma zitolewazo na AzamPesa,Makato ya Azampesa Na Jinsi ya kudownload AzamPesa App

JINSI ya Kutumia Kdi Ya GUSA AzamPesa
Kuhusu AZAM Pesa
Azam Pesa ni huduma mpya ya kifedha nchini Tanzania,HUDUMA ZA KIFALME, Bei za kizawa
Huduma mpya ya kifedha ya kutuma na kupokea pesa pamoja na kufanya malipo kupitia simu. Ni huduma ya uhakika na yenye gharama nafuu.
Kampuni kubwa na iliyoenea katika nchi ya Tanzania pamoja na nchi jirani ‘Bakhresa Group’ imeleta sokoni huduma mpya ya kifedha ijulikanayo kama ‘Azam Pesa’.
Huduma hii ni kama zilivyo huduma nyinginezo za M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa, Halopesa and the like.
Ili kuielewa zaidi huduma hii, nitaenda katika mtindo wa Maswali na kisha majibu.
Huduna Zitolewazo na Azam Pesa
kutuma au kutoa pesa
AzamPesa ni njia rahisi ya kuaminika ya kutuma au kutoa pesa.
Unaweza kutuma pesa kwenda mtandao wowote ule. Kwani kila mmoja anaweza kujisajili na AzamPesa kwa laini ya mtandao huo huo alionao.
Punde tuu baada ya kukamilisha usajili wako wa AzamPesa. Utakua na uwezo wa Kutuma na Kutoa Pesa kwa gharama nafuu sana.
Huduma yetu imetengenezwa kuwa huduma iliyo rahisi kutumia na inayomuwezesha mteja kulinda na kusimamia fedha zake kwa uhuru.
Jinsi ya Kutuma Pesa na AzamPesa
- Piga *150*08#
- Chagua 1 Tuma Pesa
- Tuma kwenda namba ya AzamPesa
- Weka namba ya simu ya mpokeaji
- Weka kiasi
- Weka namba ya siri
AU
- Fungua App ya AzamPesa
- Bofya Tuma Pesa
- Weka namba ya mpokeaji iliyosajiliwa na AzamPesa
- Weka Kiasi
- Bofya Endelea kisha Hakiki taarifa
- Bofya TUMA
- Weka PIN, kisha Thibitisha
Jinsi ya Kutoa Pesa na AzamPesa
- Piga *150*08#
- Chagua 3 Kutoa Pesa
- Weka namba ya Wakala
- Weka kiasi
- Weka namba ya siri kukamilisha muamala
AU
- Fungua App ya AzamPesa
- Bofya Toa Pesa
- Weka namba ya wakala ya AzamPesa
- Weka Kiasi
- Bofya Endelea kisha Hakiki taarifa
- Bofya TOA
- Weka PIN, kisha Thibitisha
Kukunua Muda Wa Naongezi
Azam Pesa inampa mtumiaji uhuru wa kununua muda wa maongezi kwa ajiri ya simu yake. Huduma ya kukunua muda wa maongezi ni kwa mitandao yote yani Vodacom, Tigo, Airtel, Halotel hata TTCL.
Jinsi ya Kununua muda wa Maongezi na AzamPesa
Hatua za kununua muda wa maongezi kweneye simu yako kwa kutumia AzamPesa
- Piga *150*08#
- Chagua 2 Muda wa Maongezi
- Chagua Mtandao wa Simu
- Weka Namba ya simu
- Weka Kiasi
- Weka namba ya Siri kukamilisha
AU
- Fungua App ya AzamPesa
- Bofya Muda wa Maongezi
- Chagua Mtandao wa Simu
- Weka namba ya simu
- Weka Kiasi
- Bofya Endelea
- Hakiki taarifa kisha Bofya Muda wa maongezi
- Weka namba ya SIRI kisha Thibitisha
Kulipa Bill Mbali Mbali
AzaPesa Inampa mtumiaji wake nafasi ya kufanya malipo ya bili mbali mbali kama Maji, umeme, ving’amuzi, malipo ya bidhaa (kwa MasterCard QR) kwa unafuu na haraka zaidi.
Malipo unayoweza kufanya kwa kutumia AzamPesa ni kama vile:
- Kununua Luku
- Kulipia Bili ya Maji
- Malipo ya Serikali (GEPG)
- Malipo ya Ving’amuzi
- Tiketi za ndege
- Malipo ya Huduma za Intaneti
- UTT
Jinsi ya Kulipia Bili Mbali Mbali na AzamPesa
Hatua za Kufuata ili kulipia bili kwa kutumia AzamPesa
- Piga *150*08#
- Chagua 4 Lipia Bili
- Chagua Kampuni
- Fuata maelekezo rahisi kukamilisha malipo yako
AU
- Fungua App ya AzamPesa
- Bofya Lipa Bili
- Bofya kuchagua Kampuni
- Ingiza Kumbukumbu Namba
- Ingiza Kiasi
- Bofya Endelea, kisha Hakiki taarifa za malipo yako
- Bofya Tuma
- Ingiza PIN, kisha Thibitisha
Kutumia Huduma Za Kibenki
AzamPesa pia inampa furusa mtumiaji wa benki nafasi ya kuweza kutumia huduma za kibenki kupitia simu yake ya mkononi.
Ukiwa na AzamPesa Unaweza kuhamisha Pesa kutoka kwenye akaunti yako ya Benki kwenda AzamPesa na kuhamisha Pesa Kutoka AzamPesa kwenda kwenye akaunti ya benki.
Ili kutumia huduma za kibenki kupitia AzamPesa mteja anatakiwa kuunganisha namba yake ya simu na akaunti yake ya benki.
Jinsi ya Kutumia Huduma Za Kibenki Na AzamPesa
Hatua za Kufuata Ili Kutumia Huduma za Kibenki Kupitia AzamPesa
- Piga *150*08#
- Chagua 6 Huduma za Benki
- Chagua 1 AzamPesa kwenda Benki AU 2 Benki kwenda AzamPesa
- Chagua Benki na ufuate maelekezo
AU
- Fungua App ya AzamPesa
- Bofya Hamisha kwenda Benki
- Weka Akaunti Namba
- Weka Kiasi
- Hakiki taarifa zako, kisha Bofya Thibitisha Tuma
- Weka PIN yako ya AzamPesa, kisha Thibitisha
Kwa maelezo zaidi tembelea tawi lolote la benki unayotumia lililo karibu nawe.
Kufanya Malipo Ya Serikali
Mtumiaji wa AzamPesa anaweza kufanya malipo yote ya Serikali kiurahisi kabisa kupitia simu yake bila shida ya aina yoyote ile
Aina za malipo ya serikali yanayoweza kufanywa na AzamPesa ni pamoja na
- Kununua Luku
- Kulipia Bili za maji
- Kulipia Faini za polisi
- Kulipia TRA
- Kulipia TARURA
- Kulipa Ardhi
- Kulipia LGA
Jinsi ya Kufanya Malipo Ya Seikali Kwa Kutumia AzamPesa
- Piga *150*08#
- Chagua 4 Lipia Bili
- Chagua 2 Malipo ya Serikali
- Weka Kumbukumbu namba
- Weka kiasi unachotaka kulipa
- Hakikisha taarifa zako za malipo kisha Weka namba ya siri kufanya malipo
AU
- Fungua App ya AzamPesa
- Bofya Malipo ya Serikali
- Weka Kumbukumbu Namba
- Weka Kiasi
- Hakiki taarifa za malipo yako, kisha Bofya Fanya malipo
- Weka PIN yako ya AzamPesa, kisha Thibitisha
Kulipia Huduma za Azam
AzamPesa inampa pia nafasi mtumiajiwa huduma za Azam kuweza kulipia bidhaa zake kwa urahisi zadi. Mtumiaji wa AzamPesa anaweza kulipia na kununua bidhaa mbali mbali za Azam kama vile kulipia Azam TV, AzamFerry na Sarafu.
Jinsi ya Kulipia Huduma Za Azam Kupitia AzamPesa
Ili kulipia huduma za Azam kwa kutumia AzamPesa tafadhari unaweza kufuata hatua zifuatazo;
Ili kUlipia AZAM TV
- Piga *150*08#
- Chagua 4 Lipia Bili
- Chagua 4 Azam Tv
- Chagua muda wa kifurushi unachotaka kulipia
- Chagua kiwango cha kifurushi unachotaka kulipia
- Andika namba ya kadi yako ya king’amuzi
- Weka namba ya siri kukamilisha malipo
AU
- Fungua App ya AzamPesa
- Bofya Huduma za Azam
- Bofya AzamTV Vifurushi
- Chagua muda wa kifurushi unachotaka kulipia
- Chagua kiwango cha kifurushi unachotaka kulipia
- Andika namba ya kadi yako ya king’amuzi
- Nunua sasa
- Hakiki taarifa, kisha Bofya Nunua Kifurushi
- Weka namba ya siri kukamilisha malipo
Kulipia AZAM FERRY
- Piga *150*08#
- Chagua 7 Akaunti yangu
- Chagua 6 kuona malipo yaliyosubirishwa
- Chagua malipo unayotaka kulipia
- Hakiki taarifa
- Weka namba ya siri kukamilisha malipo
AU
- Fungua App ya AzamPesa
- Bofya Akaunti Yangu
- Bofya Malipo yaliyosubirishwa
- Weka namba ya siri kuona listi
- Chagua malipo, kisha Bofya Lipa
- Hakiki taarifa, kisha Bofya Fanya Malipo
- Weka namba ya siri kukamilisha malipo
Kulipia Huduma za SARAFU
- Piga *150*08#
- Chagua 7 Akaunti yangu
- Chagua 6 kuona malipo yaliyosubirishwa
- Chagua malipo unayotaka kulipia
- Hakiki taarifa
- Weka namba ya siri kukamilisha malipo
AU
- Fungua App ya AzamPesa
- Bofya Akaunti Yangu
- Bofya Malipo yaliyosubirishwa
- Weka namba ya siri kuona listi
- Chagua malipo, kisha Bofya Lipa
- Hakiki taarifa, kisha Bofya Fanya Malipo
- Weka namba ya siri kukamilisha
Makato ya AzamPesa
Hapa tutaenda kukuonyesha gharama za makato ya huduma za AzamPesa kama vile
- Kutuma pesa kwenda AzamPesa
- Kutuma Pesa Kwnda mitndao mingine
- Kutuma pesa Benki
- Kutoa pesa
Jinsi ya Kujisajili na AzamPesa
Kuna njia kuu mbili za kuweza kujisajili na huduma ya AzamPesa na kuweza kutumia huduma zake
- Kujisajiri kwa njia ya App
- Kujisajili kupitia wakala wa Usajili
Kujisajili kwa Njia ya App
Kama unafikilia kuweza kutumia huduma za Azampesa basi unaweza kupakua App ya Azampesa kutoka Playstore au App Store na kuweza kujisajjili mwenyewe.
Kujisajili mwenyewe kwa App ya AzamPesa ni rahisi na haraka. Unachohitaji kufanya ni kuweka namba yako ya Simu na namba ya NIDA. Kisha kujibu maswali marahisi kuthibitisha NIDA yako.
Hatua Za Kufuata Ili Kujisajili na AzamPesa Kwa App
Kunahatua kadhaa za kufuata ili uweze kujisajili kwa kupitia app ya AzamPesa. Hapa chini ni hatua za kufuata,
Hatua ya 1
- Hatua ya kwanza kabisa ni kupakua App ya AzamPesa kwenye Google Play Store au iOS App Store
Hatua ya 2
- Baada ya kupakua sasa utatakiwa kubofya palipoandikwa USAJILI BINAFSI chini ya Ingia
Hatua ya 3
- Kisha page nyingine itafunguka na itakupasa kujaza namba yako ya simu na namba yako ya NIDA
Hatua ya 4
- Baada ya kuweka namba ya simu neno siri OTP litatumwa kwenye namba uliyoweka na itakupasa kuiingiza kwenye app
Hatua ya 5
- Kisha thibitisha namba yako ya NIDA kwa kujibu maswali marahisi
Hatua ya 6
- Hadi kufikia hapa utakua umejisajili na sasa unaweza kuingia kwenye App na kutumia huduma ya AzamPesa
Jinsi ya Kujisajili Kupitia Wakala Wa Usajili
Masawali Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kuhusu AzamPesa
Je, Azam wameanzisha mtandao wao wa simu?
Hapana. Azam bado hawajaanzisha mtandao wao kama zilivyo kampuni kadhaa za mawasiliano hapa nchini.
Bali AzamPesa wameingia makubaliano na baadhi ya mitandao kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa huduma kupitia line za mitandao hiyo.
Mpaka sasa AzamPesa wameshakubaliana na Tigo, Airtel na Zantel. Hivyo huduma hii inapatikana katika line za mitandao tajwa.
Je, huduma hi inahusika na nini?
Kama ilivyo huduma zingine, huduma hii inahusika na;
1.Kutuma Pesa
2.Kutoa Pesa
3.Kulipia bili
4.Kulipia bidhaa za Azam
Je, huduma hii imeanza kufanya kazi?
Ndiyo, huduma hii imeshaanza kufanya kazi kwa wateja wote waliosajiliwa.
Je, najiungaje na huduma hii?
Fika katika duka la wakala na uweze kusajiliwa. Kinachohitajika ni namba yako ya simu pamoja na namba yako ya NIDA. Ndani ya dakika mbili tayari utakuwa umeshasajiliwa kuwa mteja wa AzamPesa.
Ada za Wateja wa Azam Pesa ni za kishindani na nafuu zaidi nchini. Ukiwa na AzamPesa utaweza kupata thamani zaidi ya pesa.
Je, huduma naweza kupata vifurushi ‘bundles’ maalum vya Azam?
Hapana. Kama ambavyo nilikwishaeleza hapo juu kwamba Azam bado hawajaanzisha mtandao wao hivyo swala la vifurushi linabakia kuwa maamuzi ya mtandao husika.
Je, huduma hii naipata wapi?
Huduma hii inapatikana katika mikoa yote Tanzania. Ijapokuwa bado haijatapakaa kila mahali lakini upatikanaji wake katika maeneo mengi ya miji ni uhakika.