Jinsi ya Kukopa Salio Airtel, Habari ya wakati huu mfuatiliaji wa blog ya Habarika24, katika makala haya tunaenda kukuelekeza jinsi ya kukopa salio katika mtandao wa simu wa Airtel. Kama wewe ni mtumiaji wa laini ya airtel na ungependa kukopa salio na hufahamu ni hatua zipi za kufuata ili uweze kukopa salio pindi unapoishiwa na muda wa maongezi, dakika au hata mesiji basi makala hii itakua na umuhimu mkubwa sana kwako. Cha kufanya soma makala hii hadi mwisho,

Mtandao wa Airtel
Airtel ni mtandao unaotoa huduma za mawasiliano katika nchi tofauti tofauti na huduma mbali mbali za kidijitali. Kwa Tanzania Airtel inatoa huduma mbali mbali kwa asilimia kubwa sana ya watanzania, mfano wa huduma zitolewazo na kampuni ya mawasiliano ya Airtel ni kama vile;
- Huduma ya mawasiliano ya simu
- Huduma ya Kutuma na kupokea pesa kupitia Airtel Money
- Huduma ya kutuma mseji
- Huduma ya Internet
- Huduma ya kulipia bili na maripo ya serikali
Jinsi ya Kukopa Salio Airtel
Mtandao wa airtel inatoa salio kwa wateja wake kupitia ofa ya Daka salio, huduma hii inatoa kiwango kidogo cha salio kwa wateja wake ili kuwawezesha pale pindi wanapokua na tatizo la salio katika simu zao.
Umuhimu wa Kukopa Salio Airtel
Huduma ya kukopa salio Airtel ya Daka Salio inaumuhimu mkubwa sa na kwa watumiaji wa mtandao wa airtel, Miongoni mwa faida za kukopa salio Airtel ni pamoja na;
- Kutatua changamoto za kutokua na salio kwa wakati husika
- Itasaidia kununua vifurushi vya Airtel kama vya meseji na dk
- Itasaida kutoa taarifa ya dharula au kuomba salio kwa mtu mwingine
Hivyo basi huduma ya daka salio ya kukopa salio kwenye mtandao wa airtel ni ya muhimu sana kwa wateja wa mtandao huo. Na wewe kama ni mmoja wa watumiaji wa airtel basi ni muhimu sana kuifahamu huduma hii kwani ni huduma ya ukombozi pindi unapoishiwa na salio.
Vigezo Na Masharti ya Kukopa Salio Airtel
Kama unahitaji kukopa salio katika mtandao wa airtel unatakiwa kufikia baadhi ya vigezo na masharti kadhaa. Hapa tumeweka masharti na vigezo unavyotakiwa kuwanavyo ili kupata huduma ya daka salio kutoka mtandao wa airtel;
- Kwanza kabisa unatakiwa kua umetumia laini ya Airtel ndani ya siku 90
- Mkopo huu hutolewa kwa wateja wa malipo ya kabla
- Mkopo huu hutolewa kwa liba ya 15%
- Mlipo ya mko hufanywa kwa mtumiaji kuongeza salio katika laini yake.
- Mkopo huu unapaswa kurudishwa ndani ya siku 7 (wiki moja)
Masharti na vigezo hapo juu vimewekwa na kampuni ya mawasiliano ya airtel na kuondolewa au kudadirishwa kwa vigezo na masharti hayo yanaweza kubadilishwa au kutolewa wakati wowote na kampuni ya airtel yenyewe.
Kama wewe ni mteja mpya katika utumiaji wa mtandao wa airtel na ungependa kujua jinsi ya kukopa salio Airtel basi hapa kwenye makala hii nitaenda kukuonyesha hatua za kufuata au menu ya kupiga ili kukopa salio katika mtandao huu.
- ingia kwenye simu yako kisha piga *149*44#
- Kisha fuata maelekezo kukopa salio
Njia hii ni rahisi zaidi kwa watumiaji wa mtandao wa airtel pindi wanapoishiwa na salio na kuitaji msaada wa haraka zaidi.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Jinsi ya Kukopa Salio Tigo Haraka na Rahisi
2. Orodha ya Shule za Sekondari Mkoani Lindi
3. LATRA: Nauli Mpya Za Mabasi Ya Mikoani
4. Gharama za Usajili Wa Kampuni BRELA