Close Menu

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

    What's Hot

    Winstrol: Ein Blick auf das beliebte Anabolikum

    November 13, 2025

    Hy-Vee Employee Gateway: Huddle Access Manual and Advantages Entry

    November 13, 2025

    Free casino 1xslots 50 free spins Blackjack Video game: Zero Join, Zero Download, Use Cellular!

    November 13, 2025
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Kisiwa24
    • Home
    • Ajira
    • Makala
    • Michezo
    • Usaili
    • Kuitwa Kazini
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Kisiwa24
    Home»Makala»Jinsi ya Kujisajili na Kutumia App ya Startimes ON
    Makala

    Jinsi ya Kujisajili na Kutumia App ya Startimes ON

    Kisiwa24By Kisiwa24May 8, 2025No Comments10 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Jinsi ya Kujisajili na Kutumia App ya Startimes ON
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

    Jinsi ya Kujisajili na Kutumia App ya Startimes ON,jinsi ya kupakua Startimes On, App ya Startimes On, Jinsi ya kujisajili na Startimes On app,Startime On App Huduma kwa Wateja.Habari mwana Startimes katibu kwneye makala hii fupi amabayo itaenda kukupa mwangaza juu ya namna gani ya kudownload, kujisajili na kuweza kutumia App ya Startimes On app iliyotolewa na kampuni ya Startimes.

    Jinsi ya Kujisajili na Kutumia App ya Startimes ON

    Kuhusu Startimes

    Hii ni moja kati ya kampuni maarufu zaidi Afrika kwa urushaji wwa channel na matangazo ya euninga. Startimes imekua kampuni pendwa zaidi batani Afrika hasa Tanzania kulingana na urushaji wa vipindi vyenye maudhui bora zaidi. Uwepo wa channele zenye vipindi vilivyotafsiriwa kwa lugha ya kiswahili umeipa nafasi ya juu zaidi kwa watumiaji wa lidha ya kiswahili. Channel kama

    1. Star swahili
    2. Tv 3
    3. Mambo Tv

    Pia channel za Tanzania kama TBC 1, TBC 2, SAFARI CHANNEL, STAR TV, ITV, CHANNEL TEN, WASAFI TV CLOUDS TV na nyingine nyingi kumeifanya Startimes kua chaguo nambali moja kwa watumiaji wa lugha ya kiswahili.

    Startimes On App ni Nini?

    Hii ni Application iliyoanzaishwa na kampuni ya Startimes kwa lengo la kutoa huduma ya challen zinazorushwa kwenye runinga kupitia simu janja za mkononi. Mtumiaji wa Startimes On App anaweza kufurahia maudhui mbali mbali kama yale ya kwenye runinga kupitia startimes hata kama hana kisimbuzi cha Startimes.

    Jinsi ya Kujisajili na Kutumia Startimes On App

    Unaweza kufurahia channel zirushwazo na kampuni ya Startimes bure hata kama huna kisimbuzi cha Startimes kupitia kujisajili kwenye Startimes On App.

    Katika makala hii tutaenda kukupa mwongozo wa jinsi ya kujisajili na kutumia  Startimes On App kupitia simu yako ya mkononi, ila kumbuka ya kua huduma hii inapatika kwa watumiaji wa simu janja pekee (Smartphone)

    Jinsi ya Kudownload Startimes On App

    Hatua ya kwanza kabisa ili kuweza kutumia App ya Startimes On ni kupakua na kuinstall App ya Startimes On kwenye simu yako.

    App ya Startimes On inapatikana kwneye Play Store, App Store na hata kwenye mfuomo wa APK unaweza kwenda Google na kudownload APK file na kuinstall kwenye simu yako.

    • Kwa watumiaji wa Play Store bonyeza HAPA kupakua
    • Kwa watumiaji wa App Store bonyeza HAPA kupakua

    Jinsi ya Kujisajili kwenye Startimes On App

    Ukisha download na kuinstall App ya Startimes On kwenye simu janja yako sasa hatua inayofuata ni kuweza kujisajili. Ili uweze kujisaji unahitaji vitu vikuu vitatu

    • Email
    • Namba ya Simu
    • Neno Siri

    Kisha fungua App na ufuate hatua zifuatazo

    1. Ukiwa ndani ya App ya Startimes On nenda kweneye eneo la akaunti

    2. App itakupa machaguo mawili amabyo ni “Sign In na Sign Up” kwakua wewe ni mtumiaji wa mara ya kwanza changua Sign Up

    3. Utapewa njia 3 za kuweza kujisajili njia ya Email, Namba ya simu na facebook akaunti.

    4. Chagua njia unayopenda kujisajili nayo.

    5. Kisha fuata maelekezo yanayofuata ili kuweza kujisajili.

    Njinsi ya Kuingia (login) kwenye Startimes On App

    Baada ya kukamilisha zoezi la kujisajili sasa utaweza kulogin kwenye akaunti yako ya Startimes On App. Ili kuingia kwenye akaunti yako ya Startimes On App tafadhari unaweza kufata hatua zifuatazo

    1. Chini ya App ya Startimes On kuna menu ya Ap[p nenda palipoandikwa ME na upabonyeze

    2. Pakisha funguka nenda juu kabisa mahari palipo andikwa SIGN IN na upabonyeze

    3. Kisha ingiza login detail zako kama ulivyoweka wakati unasajili akaunti na bonyeza sign in

    4 Kisha utakua umeingia kwenye akaount yako na unaweza kufurahia channel za Startimes On App bure.

    Vifurushi Vinavyopatikana Kwenye App ya  Startimes ON

    Startimes On App inampa mtumiaji fursa za aina tatu ambazo ni

    1. Kuangalia Channel za Startimes kwa kulipia vifurushi vya kwenye App
    2. Kutazama channel za Startimes kwa kuunganisha na kisimbuzi chake
    3. Kuangalia channel za bure zilizopo kwenye Startimes bila kufanya malipo yoyote yale

    A) Vifurushi vya Startimes On App

    Ukiwa na startimes On App unaweza kufanya malipo ya vifurushi zinavyopatikana kwa matumizi ya APP peke yake. Ili kuweza kulipia vifufushi vya startimes On kwenye APP embu fuata hatua zifuatazo;

    1. Fungua App ya Startimes On na ulogin kwenye akaunti yako
    2. Kisha nenda kwenye MENU chini ya App na bonyeza palipoandikwa ME
    3. Juu kabisa utaona maneno yalioandikwa ” My star Times On Plan” mbele ya maneno hayo kunaneo ” MORE” bonyeza kwenye hilo neno
    4. Page mpya itafunguka na kisha nenda kwneye “ALL”
    5. Ukisha bonyeza neno ALL  utaona vifurushi vyote vya Startimes On App.

    Kwenye Startimes On App kunavifurushi vya aina 4 amabavyo mtumiaji anweza kulipia kwa siku, wiki,mwezi, miezi 3 na Mwaka

    Kifurushi cha Max VIP

    Kifurushi hiki kinampa mtumiaji wa startimes On App kuweza kutumia channel zote za kulipia zitolewzao na Startimes isipokua channel ya Mambo Tv

    • Malipo ya Siku  Tsh 2,200
    • Malipo ya Wiki Tsh 5,600
    • Malipo ya Mwezi Tsh 12,000
    • Malipo ya Miezi 3 Tsh 23,000
    • malipo ya Mwaka Tsh 69,000
    Kifurushi cha Poa Max

    Kifurushi hiki kinakupa uwezo wa kutazama channel ya Mambo Tv

    • Malipo ya Siku  Tsh 1,000
    • Malipo ya Wiki Tsh3,000
    • Malipo ya Mwezi Tsh 6,000
    • Malipo ya Miezi 3 Tsh 13,000
    • malipo ya Mwaka Tsh 39,000
    Kifurushi cha Cold-Blooded Boss

    Hiki ni kifurushi kinachokupa wasaha wa kutazama tamthiliya ya “Cold-Blooded Boss Love Me” pekee  pindi utakaponunua kifurushi utaweza kutazama Tamthiliya hii hadi itakapo malizika.

    • Gharama za kifurushi hiki ni Tsh 2,000 hadi tarehe 2/08/2025
    Kifurushi cha Stand-In Husband

    Pia Hiki ni kifurushi kinachokupa wasaha wa kutazama tamthiliya ya “Oop, Yuo Are A Stand-In Husband” pekee  pindi utakaponunua kifurushi utaweza kutazama Tamthiliya hii hadi itakapo malizika.

    • Gharama za kifurushi hiki ni Tsh 2,000 hadi tarehe 2/08/2025

    B) Kuangalia Channel za Startimes On App kwa Kulink Kisimbuzi chako

    Wateja ambao tayari wanavisimbuzi vya Startimes wanaweza kufurahia vifueushi walivyovilipia kwenye visimbuzi vyao kupitia App ya Startimes On wakati wowote. Ili kuweza kuunganisha kisimbuzi chako na App ya Startimes On tafadhari fuata hatua zifuatazo;

    1. Ingia kwenye App ya Startimes On kisha login kwenye akaunti yako

    2. Nenda upande wa MENU ya App chini na ubonyeze palipo andikwwa ME

    3. Kisha tafuta na ubonyeze palipoandikwa Startimes Decoder Service

    4. Kisha bonyeza palipoandikwa Click Here To Link Your Decoder

    5. Ingiza namba za kisimbuzi chako na kisha ubonyeze linki

    6. Hadi hapo utakua umeunganisha kisimbuzi chako na App yako ya Startimes On na utaweza kufurahia channel za kifurushi kilicholipiwa kwenye kisimbuzi chako kupitia Strimes On App.

    C) Kutazma channel Bure kwenye Startimes On App

    Fursa ya mwisho ni uwezo wa mtumiaji wa App ya Startimes On kuweza kutizama baadhi ya channel bure kabisa bila kulipia gharama za aina yoyoyte.

    Ilio kuweza kutazama channel za startimes bute kabisa kupitia Startimes On App  fuata hatua zifuatazo

    1.  Fungua App ya startimes kwenye simu janja yako, hii haiitaji hata kua na akaunti kwenye Startimes On App

    2. Nenda chini ya App utaona menu, kisha bonyeza neno ” LIVE TV”

    3. Hapa orodha ya channel zote za tv zitaonyeshwa za kulipia na zile za bure

    4. Ili kutizama channe za bure tafuta channel zilizoandikwa “TRIAL”

    5. Channel zote zenye neno trial unaweza kutazma bure kabisa bita kulipia chochote ukiwa na Startimes On App.

    6. Furahia maudhui ya bure ya tv ukiwa na startimes On App.

    Jinsi ya Kujisajili na Kutumia App ya Startimes ON

    MATANGAZO YA AJIRA BOFYA HAPA

    Jinsi ya Kufanya Malipo ya Vifurushi vya Startimes ON App

    jinsi ya kulipia vifurushi vya Startimes On App unaweza kutumioa njia mbili amabzo ni

    • Kupitia mitandao ya Simu
    • Kupitia eWallet kwa mteja mwenye akaunti ya Startimes On

    Ili kufanya malipo ndani ya App ya Startimes fuata hatua zifuatazo

    Malipo kwa Njia ya Mitandao ya Simu

    App ya Startimes On inaruhusu malipo kwa njia ya mitandao ya simu ya M-pesa na Tigo Pesa (Mix by Yas)

    1. Ingia kwenye app ya startimes On kisha nenda kwenye menu na ubonyeze neno ME
    2. Juu kabisa ya App bonyeza palipoandikwa MORE ili kufungua vifurushi vyote
    3. Chagua kifurushi unachokitaka na kibonyeze
    4. Kisha chagua muda wa malipo unaotaka kulipia mfano Siku, Wiki, Mwezi, Miezi 3 au Mwaka
    5. Kisha shuka chini na uchague njia ya malipo kwa mtandao wa simu kama ni M-Pesa au Tigo Pesa (MIX By Yas)
    6. Baada ya kuchagua mtandao wa kufanya malipo shuka chini na ubonyeza palipoandikwa BUY
    7. Page mpya itafunguka  na utaingiza namba ya simu ya mtandao uliouchagua. Kumbuka namba ya simu utakayoiingiza iwe na kiwango cha fedha zaidi kidogo na kile nunachotaka kulipia ili kuruhusu makato ya uhamisho wa fedha (transaction fee)
    8. Kisha bonyeza neno NEXT na susbili
    9. Ujumbe utakumwa kwenye simu yako na kamiliasha malipo
    10. Hadi hapo utakua uimefanya malipo ya kifurushi chako cha Starimes On Ap na unaweza kufurahia channel zipatikanazo nadi ya App ya Starimes On.

    Malipo kwa Njia ya Akaunti ya eWallet

    Njia ya 2 ya Kufanya malipo ya kifurushi chako ndani ya Startimes On ni kutumia akaunti ya eWallet, njia hii ni kwa wateja amabao wamrfungua akaunti ndani ya app ya Startimes On

    Ili kununua kifurushi ukipendacho kupitia akaunti ya eWallet itakupasa kwanza kuweka pesa kwenye eWallet yako kupitia mitandao ya simu kama vile

    • Tigo-Pesa
    • M-Pesa
    • Airtel Money
    • EzyPesa
    • HalPesa

    Ili kuongeza pesa kwneye akaunti yako ya eWallet kwa kutumia mitandao ya simu nenda kwenye neno RECHARGE kisha bonyeza mtandao unaotaka kufanya malipo ya eWallet yako kisha maelekezo ya kufuata yatatokea kwenye skrini ya simu yako ili kukamilisha uhamisho wa pesa kwenda kwenye akaunti yako ya eWallet ya Startimes On App

    Baada ya kuhamisha fedha kwenye akaunti yako ya eWallet sasa unaweza kulipia kifurushi ukitakacho cha Startimes On App na kuanza kufurahia channel zilizopo kwenye App ya Startimes On.

    NB;

    Kumbuka njia ya malipo ya mtandao unayoitumia lazi simu iwe hweani ili kuweza kupokea ujumbe wa kukamilisha mailipo nje ya hapo hauta fanikiwa kuweza kufanya malipo ya kifurushi chako ndani ya startimes On App.

    Faida na Hasara za Kutumuia Startimes On APP

    Kwa watumiaji wa App ya Stimes On kunafaida na hasara zake embu katika kategoria hii embu tuangazie faida na hasara za kutumia App ya Startimes On.

    Faida za Kutumia App ya Startimes On

    1. Kutazama channel bure bila kulipia gharama ya aina yoyote ile

    2. Kufuruahia channel za startimes mahari popote na wakati wowote

    3. Urahisi wa kulipia vifurushi kwa njia ya mtandao na eWallet

    4. Huna haja ya kufungua akaunti kwenye app  ya Startimes ON

    5. Unaweza kufurahia kifurushi cha kisimbuzi chako kupitia app ya startimes On kwa kuunganisha kisimbuzi chako na App yako

    Hasara za Kutumia Startimes On App

    Licha ya kuwepo kwa faida nyingi za kutumia Startimes On App lakini pia hakuna kitu kisichokua na hasara, zifuataoz ni hasara za kutuma App ya Startimes On

    1. Matumizi ya fedha za ziada kwa tumia bando –  licha ya kuunganisha kisimbuzi chako na app ya startimes On au kununua kifurushi ndani ya startimes On App bado itakubidi uwe na internet data ili kuweza kutachama channel ndani ya App ya Startimes
    2. Matumizi mabaya ya muda, kwakua startimes on app iko ndani ya simu yako unaweza kujikuta mda wote unatazama vipindi vya vinavyoppatikana ndani ya statimes TV hata wakati wa kufanya kazi nyingine
    3. Matumizi ya Chaji ya Simu- App ya startimes inapokua on kwa mda mrefu pia huongeza matumiz ya chaji ya simu yako.

    Startimes ON App Huduma kwa wateja

    Kama unachangamoto kwenye utumizi wa app ya startimes On usiwe na shaka unaweza kuwasiliana nao kwa mawasiliano tuliyoyaweka hapa chini mawasiliano haya yanapatikana 24/7

    Namba ya Simu

    • 0764 700 800
    • 0677 700 800

     

    Hitimisho;

    Startimes On App ni moja ya app bora zaidi kuwahi kutokea kwenye ulimwengu wa kampuni za urushaji wa matangazo ya channel za television nchini Tanzania, huduma zake ni nafuu zaidi naunaweza kulipa kuanzia kifurushi cha siku, wiki, mwezi, miezi 3 au hata mwaka pia unaweza kuunga decoder yako na App yako cha zidi ni kua App imedhibikiwa katika matuymizi ya data kwani unaweza kutumia kiwango cha chini cha mb hadi Mb 100 kwa lisaa.

    Mapendekezo ya Mhariri;

    1. Jinsi Ya Kulipia Vifurushi Vya King’amuzi Cha Startimes

    2. Jinsi ya kubadilisha kifurushi cha Startimes

     

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Kisiwa24
    • Website

    Related Posts

    Jinsi ya kupika Pilau kwenye Rice Cooker

    October 9, 2025

    Jinsi ya Kuwasha Rice Cooker

    October 9, 2025

    Jinsi ya kupika Maharage kwenye Rice cooker

    October 8, 2025
    Leave A Reply Cancel Reply

    Demo
    Top Posts

    PDF ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Magereza 2025/2026

    September 30, 2025629 Views

    Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2025

    July 12, 2025616 Views

    Matokeo ya Darasa la Saba Mkoa wa Dodoma 2024/2025

    October 16, 2024225 Views
    Stay In Touch
    • Facebook
    • YouTube
    • TikTok
    • WhatsApp
    • Twitter
    • Instagram
    Latest Reviews

    Subscribe to Updates

    Get the latest tech news from FooBar about tech, design and biz.

    Demo
    Covid-19 Statistics

    [rb_covid countries_code=’CN’ countries_label=’China’ columns=1]

    Most Popular

    PDF ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Magereza 2025/2026

    September 30, 2025629 Views

    Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2025

    July 12, 2025616 Views

    Matokeo ya Darasa la Saba Mkoa wa Dodoma 2024/2025

    October 16, 2024225 Views
    Our Picks

    Winstrol: Ein Blick auf das beliebte Anabolikum

    November 13, 2025

    Hy-Vee Employee Gateway: Huddle Access Manual and Advantages Entry

    November 13, 2025

    Free casino 1xslots 50 free spins Blackjack Video game: Zero Join, Zero Download, Use Cellular!

    November 13, 2025

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest
    • Home
    • Buy Now
    © 2025 ThemeSphere. Designed by ThemeSphere.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.