jinsi ya Kujisajili na Huduma za NBC Mobile Banking
Habari za wakati mwingine tena mwana Habarika24. Karibu tena katika makala hii ambayo itaenda kukupa maelekezo ya kina juu ya jinsi gani utakavyoweza kujiunga na huduma ya NBC Mobile banking kupitia simu yako ya mkononi.
NBC Benki ni miongoni mwa mabenki makubwa sana na yanayotoa huduma katika nchi ya Tanzania na pia benki ya NBC inajihusisha pia na uendeshaji wa Ligi ya NBC Tanzania. Banki ya NBC inatoa huduma mbali mbali kwa wateja wake ikiwemo huduma ya kuhifadhi pesa na kutoa pesa.

jinsi ya Kujisajili na Huduma za NBC Mobile Banking
Kuhusu NBC Mobile Banking
NBC Mobile banking ni huduma ya mtandao wa simu inayotolewa na benki ya NBC kwa lengo la kuwarahisishia wateja wke upatikanaji wa huduma za benki hiyo kama vile nji ya kutoa pesa na kuangalia salio la kwenye akaunti ikiwepo pia kulipia bili mbali mbali.
Njinsi ya Kujiunga na NBC Mobile Banking
Ili kujiunga na huduma ya NBC mobile banking tafadhari jalibu kufuata maelekezo hapa chini;
1. Pakua App ya NBC Mobile Banking
Kwanza kabisa itakupasa uweze kuinstall application ya NBC Mobile banking, kupitia simu yako tafadhari nenda playstore na utafute app ya “NBC Mobile Banking” na kisha istall kwenye simu yako
2. Tembelea Tawi la NBC Benki
Kisha nenda kwenye tawi lolote lile la banki ya NBC kujisajili na sim banking, huduma hii ya kuijisaji na NBC Mobile banking ni bure kabisa haiukuitaji wewe uweze kulipia gharama ya aina yoyote ile.
3. Thibitisha Taarifa
Mara baada ya kukamilisha usajili wako basi utapokea mesi kutoka NBC benki ambayo itakua na maelezo kamili ya usajili wa namba yako kwenye mfumo wa NBC Mobile Banking
4. Ingia Kweye Menu ya NBC Simu Bank
Mara baada ya kuthibitisha matumizi ya akaunti yako sasa utakua tayari umejiunga na huduma ya simu benki sasa itakupasa kupiga *150*55# ili kupata menyu na ufuate maagizo ili kuanza kutumia huduma ya simu benki ya NBC.
Faida za Kutumia NBC Mobile Banking
- Lipa bili kwa orodha pana ya watoza bili
- Tazama salio la akaunti yako na taarifa ndogo
- Hamisha fedha kwa akaunti zako zilizounganishwa na akaunti nyingine za NBC
- Tuma pesa kwa simu za mkononi (MPESA, TIGOPESA, AIRTEL MONEY, na EZYPESA)
- Nunua muda wa maongezi kwa nambari yoyote ya simu ya mkononi
- Hifadhi akaunti au nambari za simu za wale unaowatumia pesa au kulipa bili mara kwa mara
- Badilisha PIN yako mara nyingi unavyotaka
- Chagua lugha unayopendelea
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Kozi za Diploma na Ada Za Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA)
2. Ada na Kozi Zitolewazo Na Chuo Kikuu Cha Sokoine SUA
3. Orodha ya Shule za Sekondari Mkoa wa Njombe
4. Orodha ya Shule za Sekondari Mkoa wa Rukwa
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku