Jinsi ya kubadilisha kifurushi cha DSTV
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Habari ya wakati huu mwana Habarika24, Karibu katika makala hii ambayo itaenda kutoa elimu kwa mtumiaji wa kisimbuzi cha DSTV juu ya jinsi ya kubadilisha kifurushi cha DSTV, kutoka kifurshi unachotumia sasa na kwenda kifurushi kingine.
DSTV ni moja miongoni mwa kampuni pendwa zaidi nchini Tanzania kwenye upande wa kampuni zinazotoa huduma ya vipindi vyao bomba . DSTV inapendwa zaidi hasa na wapenzi wa mpira hasa kwa ligi za nje ya nchi hasa ligi kuu ya EPL.
Hivyo basi kama wewe ni mtumiaji wa kisimbuzi cha DST na unataka kuhama kutoka kifurushi ulichopo kwenda kifurushi kingine cha DSTV na kibaya hujui ni Jinsi ya kubadilisha kifurushi cha DSTV basi makala hii ni muhimu sana kwako.

Jinsi ya kubadilisha kifurushi cha DSTV
Vifurushi vya DSTV
Kwanza kabisa kabla ya kufahamu namna ya kubadilisha vifurshi vya DST ni vyema kwa kifupi sana tukavitambua vifurushi vinavyopatikana katika kisimbuzi cha DSTV. Vifurushi vya DSTV vinatofautiana kutoka kifurushi kimoja hadi kingine kulingana na idadi ya chaneli utofauti wa idadi ya chaneli ndio unaoleta tofauti ya gharama za malipo kutoka kifurushi kimoja hadi kingine.
Hapa chini tunakuwekea aina ya vifurushi vya DSTV na idadi ya chaneli kwa kila kifurushi
1. DSTV BOMBA PACKAGE – Ina channel 65+ bora
2. DSTV FAMILY PACKAGE – Ina channel 70+ bora
3. DSTV COMPACT PACKAGE – Ina channel 85+ bora
4. DSTV COMPACT PLUS PACKAGE – Ina channel 90+ bora
5. DSTV PREMIUM PACKAGE – Ina channel 120+ bora
Kwa maelezo zaidi na kujua bei ya vifurushi vya DST BONYEZA HAPA
Jinsi ya kubadilisha kifurushi cha DSTV
Baada ya kuvitambua vifurushi vinavyopatikana katika kisimbuzi cha DSTV sas tunaweza kuangalia ni hatua vipi za kufuata ili uweze kubadili kifurushi unachokitumia sasa kwenda kifurushi kingine. ni rahisi sana cha kufanya ni kufuata maelekezo hapa chini.
1.Tembelea Tovuti ya DST
Njia ya kwanza ya kubadili kifurushi chao cha DST ni kutembela tovuti ya DSTV. Ili kufanya hivyo nenda google na andika DSTV Tanznai kisha ingia kwenye linki ya kwanza au bonyeza linki hii kwenda moja kwa moja kwenye wavuti ya DSTV https://www.dstv.com/en-tz
– Baada ya ukrasa wa DSTV kufunguka sasa shuka chini hadi utakapoona neno OUR PACKAGE kisha angalia kifurushi unachotaka kuhamia
– Mara baada ya kukiona kifurushi bonyeza kwenye maneno yalioandikwa MORE INFO na taarifa nyungine zitajifungua
– Kisha bonyeza palipoandikwa GET kupata kifurushi hicho.
– Mara baada ya kubonyeza hapo ukrasa mpya utafunguka na kisha bonyeza palipoandikwa BUY NOW ilikununua kifurushi hicho kipya ambacho kitakua tofauti na kile cha mwanzo.
2. Kuwasiliana na Huduma Kwa Wateja DSTV
Njia nyingine ya kuweza kubadili kifushi chako cha DSTV ni kupitia njia ya mawasiliano ya huduma kwa mteja ya DSTV. Kuwasiliana na mtoa huduma wa DSTV tafadhari unaweza tumia njia hizi hapa chini
Unaweza piga simu kupitia namba;
- -+255 22 219 9600
- +255 78 410 4700,
- +255 76 898 8800
Au unaweza wasiliana nao kwa Email: [email protected]
Baada ya kupiga simu na mtoa huduma wa DSTV kupokea utampa maelezo ya kadi ya kisimbuzi chako cha DSTV na kisha kumwambia shida yako ya kuma kifurushi na yeye atakusaidia kwa kukupa maelekezo ya kufanya ili kuhamisha kifurushi cha kisimbuzi chako.
3. Kutumia Code ya Simu
Pia licha ya njia hizo hapo juu unaweza pia kutumia njia ya kupi code za DSTV. Code za DSTV ni *150*53# mara baada ya kupiga code hizo tafadhari fuata maelekezo yanayotokea kwenye screen ya simu yako ili kuweza kubadili kifurushi chako cha DSTV unachotumia kwa sasa kwenda kifurushi kingine.
Hitimosho ya Jinsi ya kubadilisha kifurushi cha DSTV
Kama tulivyosema hapo awali DSTV ni moja ya makampuni pendwa zaidi nchini Tanzania kutokana na huduma zake bora na urushaji wa chaneli pendwa zaidi na watanzania walio wengi hasa zile za mpira. Hivyo basi kama ujaridhishwa na kifurushi unachokitumia kwa sasa unaweza kufuata moja ya njia tulizozielezea hapo juu ili kubadilisha kwenda kifurushi kingine.
Hata hivyo sisi Habariak24 tunapenda kukushauri wewe mtumiaji wa DSTV kutumia njia ya kupiga simu huduma kwa wateja wa DSTV kwan njia hii itaweza kukurahisishia utatuzi wa changamoto yako moja kwa moja kutoka kwa watoa huduma wenyewe na hata kama unatatizo jingine kuhusu DSTV yako ni rahisi kuwaelezea.
Mapendekezo Ya Mhariri;
1. Jinsi ya kubadilisha kifurushi cha Azam TV
2. Jinsi ya Kusajiri Kampuni Tanzania
3. JINSI ya Kupata TIN Number Online
4. jinsi ya Kujisajili na Huduma za NBC Mobile Banking
5. Jinsi ya Kutoa Pesa Kwenye Akaunti ya NBC Bank
6. TIRA MIS Uthibitishaji wa Uhai wa Bima Ya Gari
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku