TAMISEMI: FORM FIVE SELECTION 2025/2026

_________________________________________________

MATANGAZO YA AJIRA  KILA SIKU BOFYA HAPA

_________________________________________________

NOTES ZA KIDATO CHA 1 HADI 6 BOFYA HAPA

_________________________________________________

MAGROUP MAPYA YA WHATSAAP BOFYA HAPA

_________________________________________________
MATANGO YA AJIRA BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

Gharama za Usajili Wa Kampuni BRELA

Filed in Makala by on September 2, 2024 0 Comments

Gharama za Usajili Wa Kampuni BRELA

Tangazo

Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga

Habari kama ilivyo kawaida yetu tumekua tukikuletea makala za aina mbali mbali na leo katika makala hii tutaenda kukuelezea juu ya gharama za usajili kamuni Brela. Kama inavyojulikana Brela ni wakala anayesimamia usajilo wa biashara na leseni za biashara nchini Tanzania, Hivyo basi Brela ndio mwenye mamla ya upangaji wa gharama za usajili wa kampuni.

Kama Unahitaji kuanzisha kampuni nilazima kusaji kampuni hiyo kaika mamlaka uya usajili na usimamizi Brela kwakua hili swala lipo kisheria kabisa nchini Tanzania.

Gharama za Usajili Wa Kampuni BRELA

Gharama za Usajili Wa Kampuni BRELA

Kuhusu BRELA

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ilianzishwa chini ya Sheria ya Wakala za Serikali Na. 30 ya Mwaka 1997 na kuzinduliwa rasmi tarehe 3 Desemba 1999 chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Majukumu ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ni kama yalivyoainishwa kwenye Waraka wa Uanzishwaji (establishment order) Na. 38 ya Tangazo la Serikali na. 294 la tarehe 08/10/1999

Huduma Zitolewazo Na BRELA

  1. USAJILI WA KAMPUNI
  2. USAJILI WA MAJINA YA BIASHARA
  3. UTOAJI WA HATAZA
  4. UTOAJI WA LESENI ZA BIASHARA KUNDI A
  5. UTOAJI WA LESENI ZA VIWANDA
  6. USAJILI WA ALAMA ZA BIASHARA NA HUDUMA

Gharama za Usajili Wa Kampuni BRELA

Hapa chini tunaenda kukuwekea gharama za usajili wa kampuni Brela;

Ada za Kampuni

1. Kampuni ambayo thamani ya hisa zake halisi ni:
– Zaidi ya Tsh.. 20,000/= lakini si zaidi ya Tsh.. 1,000,000/= Tsh. 95,000 /=
– Zaidi ya Tsh.. 1,000,000/= lakini si zaidi ya Tsh.. 5,000,000/= Tsh. 175,000 /=
– Zaidi ya Tsh..5,000,000/= lakini si zaidi ya Tsh..20,000,000/= Tsh. 260,000 /=
– Zaidi ya Tsh.. 20,000,000/= lakini si zaidi ya Tsh.. 50,000,000/= Tsh. 290,000 /=
– Zaidi ya Tsh..50,000,000/= Tsh. 440,000 /=

2. Usajili wa kampuni ambayo haina mtaji wa hisa ambapo idadi ya washirika ni kama ilivyoelezwa katika Malengo na Katiba ya Kampuni: Tsh. 300,000 /=

3. Ada ya kufungua jalada kwa ajili ya maombi, maana yake Tsh.. 22,000/= kwa kila waraka, yaani Malengo na Katiba ya Kampuni. Tsh. 66,000 /=

4. Gharama ya kila Ushuru wa stempu katika kila nakala ya Malengo na Katiba ya Kampuni ni Tsh. 10,000 /=

5. Gharama za ushuru wa stempu katika Fomu na. 14b Tsh. 1,200 /=

6. Kulinda jina la kampuni ni Tsh. 50,000 /=

7. Kubadilisha jina la kampuni Tsh. 22,000 /=

8. Gharma za upokeaji na/au usajili wa waraka wowote kwa Msajili chini ya Sheria ni Tsh. 22,000 /=

9. Gharama za kuchelewa kufungua faili/usajili wa waraka wowote zinalipwa kwa Msajili (kwa mwezi au sehemu ya siku za mwezi) TSHS 2,500 /=

10. Gharama za kujaza taarifa ya mwaka Tsh. 22,000 /=

11. Gharama za ithibati ya waraka wowote kwa ukurasa ni Tsh. 3,000 /=

12. Gharama za kutafuta jalada lolote/au kupekua kitu chochote ni Tsh. 3,000 /=

13. Gharama kwa ajili ya ripoti ya utafutaji kwa faili ni Tsh. 22,000 /=

14. Ada zinazolipwa na kampuni ambapo Kifungu XII cha Sheria kinahusika
– Gharama za usajili wa nakala yenye ithibati ya mkataba, sheria au malengo na katiba ya kampuni, au muongozo mwingine au kufafanua katiba ya kampuni ni Dola za Kimarekani 750 /=
– Gharama za ujazaji wa waraka wowote unaohitajika kupelekwa kwa Msajili chini ya Kifungu XII cha Sheria hii/mbali na mizania ni Dola za Kimarekani 220 /=
– Gharama kwa ajili ya kufungua jalada la mizania Dola za Kimarekani 220 /=
– Ada ya kuchelewa kufungua jalada/usajili wa waraka wowote inalipwa kwa Msajili (kwa mwezi au sehemu ya siku za mwezi) ni Dola za Kimarekani 25 /=

15. Gharama ya kupata nakala ya Cheti cha Usajili Tsh. 4,000 /=

Majukumu ya BRELA

Hapa chini tumeainisha majukumu ya msingi yanayofanywa na BRELA

  1. Kusajili Kampuni (The Companies Act, Cap. 212);
  2. Kusajili Majina ya Biashara (The Business Names (Registration) Act, Cap. 213 R.E. 2002);
  3. Kusajili Alama za Biashara na Huduma (The Trade and Service Marks Act, Cap. 326 R.E. 2002);
  4. Kutoa Hataza (The Patents (Registration) Act, Cap. 217 R.E. 2002);
  5. Kutoa Leseni za Viwanda (The National Industries (Licensing and Registration) Act, Cap 46 R.E. 2002);
  6. Kutoa Leseni za Biashara Kundi “A” (The Business Licensing Act Cap. 208 R.E. 2002)

Hapo juu tumeweka gharama zote za usajili wa kampuni ikijumuisha gharama za msingi na zile za ziada ili kukamilisha ada za msingi kwenye kusajili kampuni ila gharama hii inaweza kupungua au kuongezeka kutokana na mabadiliko ya gharama za ziada.

Machaguzi ya Mhariri

1. Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Usalama Wa Taifa Tanzania

2. Ada Na Kozi Zitolewazo na Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam

3. Ada na Kozi Zitolewazo Na Chuo Cha Dodoma

4. LATRA: Nauli Mpya Za Mabasi Ya Mikoani

5. Mabasi Dar Kwenda Mbeya

6. Nauli ya Basi Dar Kwenda Dodoma

7. Kampuni Za Mabasi Ya Dar To Morogoro 

MATANGO YA AJIRA BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *