Ada za Masomo ya Udereva Chuo cha NIT, ada ya udereva chuo cha NIT, Habari ya wakati huu mwanakisiwa24, karibu katika makala hii itakayoenda kukupa mwongozo wa ada za kozi ya udereva katika chuo cha NIT.
Je unafikilia kusoma kozi ya udereva katika chuo bora zaidi nchini Tanzania, basi ni muhimu pia kabla ya kutaka kujiunga na chuo cha NIT katika kozi ya udereva ukafahamu gharama za kozi hizo zitozwazo na chuo cha NIT.
Hapa katika makala hii tutaenda kukupa mwongozo wa jumla juu ya;
- Kozi za udereva zitolewazo na chuo cha NIT
- Garama za ada kwa kila kozi
- garama za ziada
Ada Mpya za Kozi ya Udereva Chuo cha NIT 2025
Tunapotaka kuzungumzia gharama za ada za kusomea udereva kutoka chuo cha NIT lazima kwanza tufahamu ni kozi zipi za udereva zinazotolewa na chuo cha NIT.
Kozi za Udereva Zitolewazo na Chuo cha NIT
Chuo cha NIT kinatoa mafunzo ya udereva katika ngazi kuu 2 ambazo ni
1. Mfafunzo ya Msingi ya Udereva
Hapa mwanafunzi hupewa mafunzo ya msingi kwenye fani ya udereva kama vile jinsi ya kuendesha na kulidhibiti gari lakini pia hupewa mafunzo juu ya matumizi ya barabara kama vile kuzijua na kutafsiri alama za barabarani
Kozi hii ni ya muhimu sana kwa mtu anayefikilia kuanza safari yake ya udereva na kiujumla gharama za kujifunza kozi hii ni dogo ukilinganisha na umuhimu wa mafunzo yanayotolewa katika kozi hii.
2. Kozi ya Udereva ya Juu
Baada ya mafunzo ya msingi, mwanafunzi wa udereva huamia katika kozi ya udeteva ya juu. Kozi hii huwa na mafunzo makubwa zaidi katika fani ya udereva baada ya mwanafunzi kupata mafunzo ya msingi.
Ada za Kozi ya Udereva Chuo cha NIT
Chuo cha NIT ni nmiongoni mwa vyuo bora zaidi Tanzania kwa utoaji wa kozi za udereva. Chuo hiki kinatoa kozi mbalimbali za udereva kwa muda tofauti tofauti. Kozi hizi pia zinatofautiana katika gharama za ufundishwaji.
Hapa chini ni mwongozo wa ada za kozi ya udereva Chuo cha NIT
Kozi ya Msingi ya Udereva (Basic Driving Course)
- Ada yake ni Tsh – 200,000
- Muda wa Kozi – Siku 11
Kozi ya Udereva wa Magari Makubwa (Heavy Goods Vehicle)
- Ada yake ni Tsh – 515,000
- Muda wa Kozi – Siku 15
Kozi ya Madereva wa VIP (Advanced Drivers Grade II – VIP)
- Ada yake ni Tsh – 400,000
- Muda wa Kozi – Wiki 4
Kozi ya Udereva wa Gari za Abiria (Passenger Service Vehicle)
- Ada yake ni Tsh – 200,000
- Muda wa Kozi – Siku 11
Kozi ya Udereva Maalum (Senior Driver Course)
- Ada yake ni Tsh – 450,000
- Muda wa Kozi – Wiki 6
Kozi ya Waendeshaji wa Forklift (Forklift Operator’s Training)
- Ada yake ni Tsh – 400,000
- Muda wa Kozi – Siku 5
Gharama za Ziada za Kozi ya Udereva Chuo Cha NIT
Nje ya ada za msingi za kozi za udereva kutoka chuo cha NIT pia kuna gharama za ziada ambazo mwombaji wa kozi ya udereva katika chuo cha NIT itampasa kulipa, gharama hizo ni pamoja na
Ada ya Maombi:
- Tshs 10,000
- Ada hii huwa hairejeshwi baada ya kufanyiwa malipo.Kwa muombaji wa nafasi ya kozi ya udereva ili kufanya malipo ya ada ya maombi fuata maelekezo yanayopatikana kwenye tovuti rasmi ya chuo- www.nit.ac.tz.
Ada ya Awali ya Mtihani:
- Tshs 20,000
- Ada hii hulipwa kwa waombaji wa kozi za PSV, HGV, INDUSTRIAL, na VIP.
- Ili kujiunga na kozi hizi Waombaji wanatakiwa kufaulu mtihani wa majaribio.
Ada ya Maombi ya MBA
- Tshs 30,000( Tanzania) na
- USD 25 kwa waombaji wa Nje
- Ada hii hutozwa kwa kozi za Master of Business Administration katika Usimamizi wa Usafirishaji na Usafiri.
Mwongozo wa Malipo ya Ada
Malipo haya ya Ada na gharama za ziada kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kozi yoyote ile ya udereva kama tulivyoainisha hapo juu wanapaswa kuzilipa mapema zidi kabla ya muhura kuanza. Malipo ya ada na kozi hufanyika kupitia mfumo wa kiserikali wa GePG kupitia namba ya malipo ya chuo (University Control Number) ambayo mwanafunzi ataipata chuoni.
Gharama Za Malazi na Makazi
Gharama zilizo orodheshwa hapo juu ni gharama za malipo ya kozi, kwa upande wa Malazi na Makazi Chuo cha NIT hakijushughulishi hivyo mwanafunzi atajitegemea kwa upande wa malazi na makazi.
Kwa maelezo Zaidi Unaweza Wasiliana na Uongozi wa Chuo
Simu: +255 22 2400148/9
Fax: +255 22 2443140
Simu ya Mkononi:
- +255 684 757 774
- +255 762 202 215
- +255 713 794 870
- +255 782 422 199
Barua pepe: [email protected]
Au unaweza kutembela tovuti rasmi ya chuo kupitia linki – www.nit.ac.tz.
Hitimisho;
Chuo cha NIT kimekua kitovu cha uzalishaji wa madereva wapya kila kukicha wenye taaluma na kwa wale madereva mwenye uzoefu hutumia chuo hiki ili kuongeza maalifa.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Mwongozo wa Bei ya Leseni ya Udereva Tanzania
2. Mwongozo wa Jinsi Ya Kupata Leseni Ya Udereva Tanzania