BONYEZA HAPA KUTAZAMA MAJINA YA WALIOITWA USAILI JESHI LA POLISI
Mkuu wa Jeshi la Polisi anawatangazia vijana walioomba ajira ya Jeshi la Polisi kupitia mfumo wa Ajira (TANZANIA POLICE FORCE – RECRUITMENT PORTAL) kuwa usaili utafanyika kuanzia tarehe 28/4/2025 saa 07:00 Asubuhi hadi tarehe 11/5/2025 kote nchini.
Kwa wasailiwa wenye elimu ya Shahada, Stashahada na Astashahada usaili utafanyika jijini Dar es Salaam katika uwanja wa gwaride uliopo Kambi ya Polisi (Police Barracks) barabara ya Kilwa nyuma ya kituo cha Polisi Kilwa
Road.
Kwa wasailiwa wenye elimu ya kidato cha Nne na cha Sita usaili utafanyika kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa waliyoichagua wakati wa kutuma maombi.
Kwa wasailiwa wa Zanzibar wenye elimu ya Shahada, Stashahada, Astashahada, Kidato cha sita na Nne, usaili utafanyika Zanzibar ambapo kwa walioko mikoa ya Unguja, usaili utafanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani) na Mikoa ya Pemba usaili utafanyika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba (Chakechake).
Kila msailiwa atalazimika kufika eneo la usaili akiwa na vyeti halisi vya taaluma (Academic certificates), cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha Taifa cha NIDA au namba ya NIDA pamoja na nguo na viatu vya michezo.
Msailiwa atakayefika kwenye usaili baada ya tarehe 28/04/2025 hatapokelewa. Aidha, orodha ya waliochaguliwa kufanya usaili imeambatishwa pamoja na tangazo hili.