Close Menu
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM

December 13, 2025

NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited

December 13, 2025

NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania

December 13, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Kisiwa24Kisiwa24
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala
Subscribe
Kisiwa24Kisiwa24
Home»Ajira»Tangazo La Kuitwa Kwenye Usaili Benki Kuu Ya Tanzania Majina Ya Nyongeza February 2025
Ajira

Tangazo La Kuitwa Kwenye Usaili Benki Kuu Ya Tanzania Majina Ya Nyongeza February 2025

Kisiwa24By Kisiwa24February 17, 2025No Comments2 Mins Read
Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Reddit Telegram Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Tangazo La Kuitwa Kwenye Usaili Benki Kuu Ya Tanzania Majina Ya Nyongeza February 2025

Naibu Gavana Utawala na Udhibiti wa Ndani wa Benki Kuu ya Tanzania anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili wa kuandika/mchujo (Aptitude Test) unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 15-02-2025 hadi 24-03-2025. Wasailiwa watakaofuzu usaili huu na kwenda katika hatua zinazofuata watatakiwa kushiriki katika usaili wa vitendo au/na mahojiano kwa tarehe iliyoanishwa au kama watakavyotaarifiwa kwa wakati husika.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wa kuandika/mchujo (Aptitude Test) wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.

2. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;

3. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji/shehia anakotoka msailiwa.

4. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na vyeti vingine (kutegemeana na nafasi aliyoomba).

5. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.

6. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.

7. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
8. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTVET au NECTA)

9. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.

10. Wasailiwa wa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.

11. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.

12. MUHIMU: Wasailiwa watakao shindwa kuwasilisha nyaraka zilizokamilika kama zilivyoainishwa katika kipengele na. 2, 3, 4, 8 na 10 hawataruhusiwa kuendelea na usaili.

Bonyeza HAPA kupakua Majina Yote

Mapendekezo ya Mhariri;

1. English Second Language Teacher at EF Teach Online

2. English Second Language Teacher at Micro1 February 2025

3. LtP Content Review Specialist & Language Editor-Consultant at International Rescue Committee February 2025

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
Previous ArticleNafasi za Kazi – English Second Language Teacher at EF Teach Online
Next Article Kikosi cha Yanga SC vs Singida BS Leo 17 Februari 2025
Kisiwa24

Related Posts

Ajira

MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM

December 13, 2025
Ajira

NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited

December 13, 2025
Ajira

NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania

December 13, 2025
Add A Comment
Leave A Reply Cancel Reply

Recent Posts

  • MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM
  • NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited
  • NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania
  • NAFASI za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
  • NAFASI za Kazi Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania

Recent Comments

No comments to show.
Demo
Top Posts

Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2025

July 12, 20251,159 Views

MAJINA Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs

December 6, 2025788 Views

NAFASI za Kazi Za Mkataba Wizara Ya Maliasili Na Utalii

December 6, 2025446 Views
Stay In Touch
  • Facebook
  • YouTube
  • TikTok
  • WhatsApp
  • Twitter
  • Instagram
Latest Reviews

Subscribe to Updates

Get the latest tech news from FooBar about tech, design and biz.

Demo
© 2025 Kiswa24 Blog. Designed by Kisiwa24.

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.