Jinsi ya Kujiunga na Mfuko wa Uwekezaji wa UTT AMIS, Jinsi ya Kujiunga na Akaunti ya UTT AMIS Tanzania, Jinsi ya kujiunga na UTT AMIS, UTT AMIS, Hii ni kampuni inayojihusisha na uwekezaji wa masoko ya fedha kupitia njia mbalimbali, uwekezaji wa fedha kati kampuni hii huleta faida wakati wa uuzaji wa vipande utavyonunua na kuwekeza kupitia akaunti yako ya UTT AMIS.
Jinsi ya Kujiunga na UTT AMIS
Ili kuanza kuwekeza pesa zako kwenye kampuni ya UTT AMIS itakupasa uweze kufungua akaunti. Kufungua akaunti ya UTT AMIS ni rahisi kabisa kwani unaweza kufanya hivyo kupitia simu yako ya mkononi
A) Kufungua Akaunti ya Kupitia SimImvest
Ili kufungua akaunti yako ya UTTAMIS kwa kutumia mfumo wa SimImvest tafadhari fuata hatua zifuatazo;
1. Ingia kwenye simu yako na Upinge *150*82#
2. Chagua lugha uitakayo
3. Kisha Fungua Akaunti Mpya
4. Akaunti Binafsi
5. Kisha jaza jina la muwekezaji na tarehe ukifuata mfumo wa DDMMYY
6. Kisha chagua Umiliki Binafsi
7. Kisha ingiza Jina la Mfuko, kulingana na mfuko unaohitaji kuwekeza.
8. Kisha utapokea ujumbe wa maelekezo.
9. Hadi hapo utakua tayari umesha fungua Akaunti ya uwekezaji kwenye kampuni ya UTT AMIS
B) Kujaza Fomu Ya Maombi
Baada ya kukamilisha ufunguaji wa akaunti yako na kuchagu mfuko unaotaka kuwekeza sasa itakupasa kujaza fomu ya maombi ya uwekezaji. Unaweza kuzipata form za kujiunga na UTT AMIS uwekezaji katika maeneo yafuatayo
- Tovuti ya UTT AMIS; [email protected], kisha tuma form yako katika email ya [email protected]
- Tawi lolote la CRDB
- Ofisi za UTT AMIS zilizo karibu
C) Fanya Mawasilisho ya Fomu ya Maombi
Baada ya kupata fomu ya maombi na kuijaza kikamilifu kulingana na maezo ya kwenye fomu sasa itabidi uitume form kwa uthibitisho. tuma form yako katika email ya [email protected]. Hakikisha unapoituma fomu uiambatanishe na
- picha( passport size, pamoja)
- Pamoja na copy ya kitambulisho chako
D) Subili Majibu ya Kufunguliwa Kwa Akaunti Yako ya UTT AMIS
Ukisha tuma fomu yako na kupokelewa utasubili majibu ya kufunguliwa kwa akaunti yako na baada ya kufunguliwa kwa akaunti yako sasa utaweza kuanza uwekezaji wako kwa kununua vipande kulingana na mfuko uliouchagua wakati wa kufungua akaunti yako kupitia huduma ya SimImvest.
Faida za Kujiunga na UTT AMIS
- Urahisi wa Kuwekeza:
- Uwazi na Uwezo wa Kufuata Maendeleo
- Faida Shindani
Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea tovuti rasmi ya UTT AMIS kupitia linki – https://uttamis.co.tz/
Kwa kufuata hatua hizo hapo juu sasa utakua umeshajiunga na mfuko wa uwekezaji wa UTT AMIS na kuanza kufanya uwekezaji wako kwa njia rahisi kabisa zitakazoweza kukuwezesha kununua vipande vya mfuko wa UTT AMIS kulinga na jinsi ulivyo jisajili na mfuko uliouchagua.
Mapendekezo ya Mhariri;
Mwongozo wa Bei ya Vipande vya UTT AMIS 2025
Jinsi ya Kununua Vipande Vya Uwekezaji Vya UTT AMIS