Jinsi Ya Kupata Leseni Ya Udereva, Leseni ya udereva Tanzania, Aina ya leseni ya udereva Tanzania,Habari mwana kisiwa24 blog karibu katika makala hii fupi itakayoenda kukupa mwongozo juu ya jinsi ya kupata leseni ya udereva Tanzania.
Kama ulisha wahi kufikilia kuendesha gari lako binafsi ndani ya nchi ya Tanzania au kuwa dereva wa kampuni flani kitu cha kwanza kitakacho kuijia akilini ni kua na leseni ya udereva amabayo itakupa uhuru wa udereva wako pindi uwapo barabarani.
Leseni ya Udereva Ni Nini
Leseni ya udereva ni nyaraka au kibari kitolewacho kwa mtu aliyekidhi vigezo vya uendeshaji wa gari nchini Tanzania. Leseni ya Udereva hutumika kuonyesha umahili wa mwendesha gari kulingana na daraja la gereva husika. Ili uweze kuendesha gari kwa uhuru nchini Tanzania lazima uwe na leseni ya udereva.
Hivyo basi makala hii yenye mwongozo wa namna gani unavyoweza kupata leseni ya udereva imeanadaliwa ili kukupa maarifa kwa wewe unayefikilia kuwa dereva nchini Tanzania kuweza kupata leseni yako ya udereva.
Namna Ya Kupata Leseni Ya Udereva
Kuwa na leseni ya udereva kwa dereva anayetaka kuendesha gari nchini Tanzania ni miongoni mwa hatua muhimu sana katika safari ya kuadereva huru na bora. Kwa kuzingatia umuhimu wa kua na leseni ya udereva kwa madereva Tanzania tumeamua kukuletea mwongoz utakaokuonyesha jinsi ya kuweza kupata leseni ya udereva nchini Tanzania.
Madaraja ya Lesini za Udereva
Kabla ya kuangalia hatua za jinsi ya kupata lesini ya udereva hatuna budi kutazama kwanza aina za leeni za udereva zinazopatikana nchini Tanzania. Tanzania ina aina kuu 8 za leseni. Hapa chini tumekuwekea aina zote 8 za leseni za udereva kwa kifupi, kwa maelezo ya kina juu ya aina za leseni za udereva Tanzania bonyeza HAPA.
- Daraja A: Pikipiki (za ukubwa tofauti)
- Daraja B: Magari ya binafsi
- Daraja C: Magari ya abiria (daladala, mabasi)
- Daraja D: Magari ya mizigo
- Daraja E: Magari yote (isipokuwa ya abiria na pikipiki)
- Daraja F: Mitambo maalum (forklifts, graders)
- Daraja G: Mitambo ya kilimo na migodi (tractors)
- Daraja H: Leseni ya kujifunza (provisional)
Mahitaji ya Msingi Kabla ya Kuanza Mchakato wa Kupata Leseni ya Udereva
Kabla ya kuanza mchakato wa kupata leseni ya udereva, ni muhimu kuhakikisha unatimiza mahitaji ya msingi. Kwanza, lazima uwe na umri wa miaka 18 au zaidi. Pili, unahitaji kuwa na uwezo wa kusoma na kuandika, hasa kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza. Pia, ni muhimu kuwa na afya nzuri na uwezo wa kuona vizuri.
Hatua za Kufuata Ili Kupata Leseni ya Udereva Tanzania
1. Kujiunga na Shule ya Udereva
Hatua ya kwanza ni kujiunga na shule ya udereva iliyosajiliwa rasmi na kutambuliwa na TRA. Hapa utapata mafunzo ya nadharia na vitendo. Mafunzo haya yanachukua kipindi cha miezi 2-3, kutegemea na ratiba yako.
Wakati wa mafunzo, utajifunza:
- Sheria na kanuni za barabarani
- Ishara na alama za barabarani
- Sehemu mbalimbali za gari na matengenezo ya msingi
- Mbinu za udereva salama
- Jinsi ya kukabiliana na dharura barabarani
2. Omba Leseni ya Kujifunza
Baada ya kuanza mafunzo ya udereva kutoka chuo kinachotambulika na TRA itakupasa kuomba leseni ya kujifunzia kutoka TRA.
3. Fanya Mtihani wa Udereva
Hatua hii inahusisha kupima uwelewa wako wa mafunzo ya udeleza uliuoyapitia wakati ulipokua shuleni. Mtihani wa udereva umegawanyika katika makundi mawili
- Mtihani wa Nadharia
- Mtihani wa vItendo
A) Fanya Mtihihani wa Nadharia
Baada ya kukamilisha mafunzo, utahitaji kufanya mtihani wa nadharia katika ofisi za TRA (Tanzania Revenue Authority). Mtihani huu unafanyika kwa kompyuta na unahitaji kufaulu kwa asilimia 80 au zaidi. Mtihani hujumuisha maswali kuhusu:
- Sheria za barabarani
- Ishara za barabarani
- Usalama barabarani
- Huduma ya kwanza
B) Mtihani wa Vitendo
Ukifaulu mtihani wa nadharia, hatua inayofuata ni kufanya mtihani wa vitendo. Mtihani huu unafanyika chini ya usimamizi wa afisa wa TRA na unajumuisha:
- Kuendesha gari kwenye barabara ya kawaida
- Kuegesha gari
- Kuendesha gari kwenye mteremko
- Kufuata ishara zote za barabarani
- Kuonyesha uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali za barabarani
4. Kukusanya Nyaraka Muhimu
Ukifaulu mitihani yote, utahitaji kukusanya nyaraka zifuatazo:
- Picha mbili za passport size
- Nakala ya kitambulisho cha Taifa au passport
- Cheti cha afya kutoka hospitali iliyothibitishwa
- Stakabadhi ya malipo ya ada husika
- Fomu ya maombi iliyojazwa kikamilifu
5. Fanya Malipo ya Ada ya Leseni
Utahitaji kulipa ada mbalimbali, zikiwemo:
- Ada ya usajili
- Ada ya mtihani wa nadharia
- Ada ya mtihani wa vitendo
- Ada ya leseni yenyewe
6. Pata Leseni yako
Baada ya kukamilisha hatua zote hapo juu utasubili muda kidogo na TRA itashugulikia ombi la leseni yako na pindi leseni yako itakapokua tayari utatumiwa na TRA kupitia sanduku la posta uliloliweka kwenye formu ya maombi ya leseni au unaweza kuifuata mwenyewe kwenye ofisi za TRA.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Jinsi ya Kujisajili na Kutumia App ya Startimes ON
2. Jinsi ya Kujisajili na Kutumia AzamTV MAX App