Nafsi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa December 2024
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa anawatangazia Wananchi wote Raia wa Tanzania wenye sifa zinazohitajika kuomba kujaza nafasi wazi baada ya kupokea vibali vyaa ajira Mpya chenye Kumb Na. FA. 97/228/01/09 cha tarehe 22 Juni, 2024 na chenye Kumb. Na. FA.170/360/01A/144 cha tarehe 22 Oktoba, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
1. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III (NAFASI 3)
2. MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA III (NAFASI 2)
3. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (NAFASI 2)
4. DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 4 )
MAELEZO/ MASHARTI YA JUMLA
i) Mwombaji awe Raia wa Tanzania ambaye ana umri si zaidi ya miaka 45 na sio pungufu ya Miaka 18.
ii) Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
iii) Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae ( CV) yenye Anwani inayotumika, namba ya simu na Anuani ya barua pepe (E-mail address) pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
.
iv) Matokeo ya muda (Provisional/Testimonials/Statement of results) havitakubaliwa.
v) Waombajiw ote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
vi) Wombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokua kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
vii) Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
viii) Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na Wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyokatika waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
ix) Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbali mbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
x) Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (NECTA na NACTE).
xi) Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahausika watachukuliwa hatua za kisheria
xii) Barua ya maombi itatakiwa iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.
xiii)MUHIMU: kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa,
S.L.P 12,
MPWAPWA.
xiv) Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https:portal.ajira.go.tz/ (anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
xv) Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
xvi) Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 20 Desemba, 2024
Bonyeza HAPA kupakua Tangazo lote
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Nafasi za Kazi One Plan Solution December 2024
2. Nafasi za Kazi Puma Energy December 2024
3. Nafasi za Kazi Kutoka Minor Hotels December 2024
4. Nafasi Za Kazi Mwanga Hakika Bank December 2024