Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Arusha Technical College
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Arusha Technical College, Habari ya wakati huu mwana Habarika24, karibu katika makala hii fupi ambayo tutaenda kukupa maelekezo juu ya Ada,fomu, kozi na sifa za kujiunga na chuo cha Arusha Technical Collage. Kama unatarajia kujiunga na chuo cha Ausha tech Collage basi hunabudi kusoma makala hii hadi mwisho kwani itakupa mwangaza wa mambo ya msingi kama vile ada za kozi mbali mbali katika chuo cha Arusha Technical Collage, fomu ya kujiunga na sifa na vigezo vya kujiunga na chuo.
Kuhusu Arusha Technical Collage
Chuo cha Arusha Technical Collage kilianzishwa mwaka 1978 kwa ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ujerumani inayojulikana pia kwa jina la FRG-Federal Republic of Germany “West Germany”, kwa jina la Chuo cha Ufundi Arusha (TCA). Wilaya ya Kati ya Biashara ya Jiji la Arusha ambalo ni kitovu cha Kaskazini mwa Tanzania cha kilimo, biashara, biashara na utalii. Jiji la Arusha pia ni Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na ni kitovu cha Afrika kati ya Cape Town na Cairo. Imezungukwa. na milima maarufu kama vile Mlima Kilimanjaro na Mlima Meru. Aidha, ni mlango wa makimbilio makubwa ya wanyamapori duniani ikiwemo Ngorongoro Crater, Serengeti na Tarangire. Yote haya hufanya eneo la Chuo kuwa mahali pazuri pa kusoma. Sehemu ya majukumu ya ATC wakati wa kuanzishwa kwake ilikuwa kutoa mafunzo kwa mafundi kwa miaka mitatu hadi ngazi ya Cheti cha Ufundi Kamili (FTC) katika fani za Uhandisi wa Magari, Uhandisi Ujenzi, Uhandisi Umeme, Uhandisi Usafirishaji na Uhandisi Mitambo. Mnamo Machi 2007, jina lilibadilishwa na kuwa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kupitia Agizo la Uanzishwaji wa Chuo cha Ufundi Arusha Namba 78 kama ilivyowezeshwa na Sheria ya NACTE namba 9 ya 1997. taasisi ya elimu ya juu.
Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Arusha Technical College
Kozi Zinazotolewa na Chuo Cha Arusha Technical Collage
Chuo cha Arusha Technical Collage kinatoa kozi mbali mbali katika ngazi za diploma na digrii hapa chini tunaenda kukuwekea kozi kwa kila ngazi ya elimu
Kozi za Diploma (Astashahada) Zitolewazo na Chuo cha Arusha Technical Collage
- Diploma ya Uhandisi Ujenzi
- Diploma ya Uhandisi Umeme wa Maji
- Diploma ya Uhandisi wa Mitambo ya Mafuta na Gesi
- Diploma ya Uhandisi Mawasiliano
- Diploma ya Tehama
- Diploma ya Uhandisi Magari
Kozi za Digrii (Shahada) Zitolewazo na Chuo cha Arusha Technical Collage
- Shahada ya Uhandisi wa Umeme na Kiotomatiki
- Shahada ya Uhandisi wa Nishati Mbadala
- Shahada ya Sayansi ya Kompyuta
- Shahada ya Uhandisi wa Mitambo
- Shahada ya Uhandisi wa Maabara na Teknolojia ya Viwanda
Ada za Chuo cha Arusha Technical Collage katika Kozi Mbali Mbali
Hapa tunaenda kukupa maelezo ya kina juu ya ada za kozi zinazotolewa katika chuo cha Arusha technial Collage,
Ada ya Kozi ya Diploma (Astashahada)
- Ada kwa mwaka ni kati ya Tsh 1,200,000 – 1,500,000
Ada ya Kozi ya Digrii (Shahada)
- Ada kwa mwaka ni kati ya Tsh 1,500,000 – 2,000,000
Fomu ya Kujiunga Na Chuo Cha Ufundi Cha Arusha Technical Collage
Fomu za kujiunga na chuo cha ufundi cha Arusha Technical Collage zinapatika moja kwa moja kwenye wavuti kuu ya chuo, Ili kupata fomu ya maombi tafadhari fuata hatua zifuatazo hapa chini;
1. Kwanza tembelea tovuti ya chuo cha ufundi cha Arusha Technical Collage kupitia linki hii – https://www.atc.ac.tz/
2. Ndani ya tovuti nenda kwenye menu iliyoandikwa ICT service kisha tafuta electronic Payment (GePG)
3. Bonyeza hapo ili kupata namba ya malipo ili kufanya malipo(hakikisha umesha jisajili katika mfumowa tovuti ya chuo)
4. Baada ya kupata namba ya malipo fanya malipo kupitia simu au banki, malipo ya fomu ni Tsh 20,000 tu.
Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Ufundi Cha Arusha Technical Collage
Ili kujiunga na kozi zitolewazo na chuo cha ufundi cha Arusha Technical Collage lazima mwanafunzi aweze kukizi sifa na vigezo vya kozi ya ngazo husika.Hapa tutaenda kukuonyesha sifa kwa kila ngazi na kozi zake;
Sifa za Kujiunga na Kozi za Diploma katika Chuo Cha Ufundi Cha Arusha
1. Awe amehitimu kidato cha Nne na alama za ufaulu wa angalau D nne ikiwemo Hisabati na Sayansi
2. Awe amehitimu kidato cha Sita na alama za ufaulu wa angalau E mbili katika masomo ya sayansi
Sifa Za Kujiunga na Kozi za Digrii katika Chuo Cha Ufundi Cha Arusha
1. Awe amehitimu kidato cha Sita na alama za ufaulu wa angalau D mbili katika masomo ya sayansi.
2. Awe ana stashahada ya Ufundi kutoka chuo kinachotambulika na NACTE.
Hitimisho
Chuo cha ufundi cha Arusha Technical Collage ni chuo bora cha ufundi na kinatoa kozi katika ngazi za diploma (Astashahada) na digrii (Shahada). Ili kujiunga na kozi zinazotolewa katika chuo hiki lazima mwanafunzi aweze kukidhi sifa na vigezo kulingana na kozi husika kwa kujaza fomu kutoka katika tovuti ya chuo na kulipia ada ya fomu ya Tsh 20,00.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Dar es Salaam
2. Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Temeke
3. Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Mwanza
4. Ada, Fomu, Kozi na Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Utalii Arusha
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku