Mabasi ya Dar es Salaam Kwenda Mwanza
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Mabasi ya Dar es Salaam Kwenda Mwanza, Habari ya wakati huu mwana Habarika 24, Karibu katika makala hii fupi ambayo itaenda kukuelezea juu ya usafiri wa mabasi yanayofanya safari zake kati ya mkoa wa Dar es Salaam na Mwanza Kila siku
Kama wewe ni msafiri unayetaka kufanya safari yako kutoka mkoa wa Dar es Salaam kwenda Mwanza au Mwanza kwenda Dar es Salaam kwa usafiri wa basi inakupasa usome makala haya ili kutambua aina ya kampuni za mabasi zinazofanya safari zake baina ya mikoa hii miwili.
Njia za Usafiri kati ya Dar es Salaam na Mwanza
Mkoa wa Dar es Salaam na Mwanza inaunganishwa na nja mbi za usafiri nazo ni;
- Usafiri wa Anga (ndege)
- Usafiri wa Aridhini (Gari)
Hapa katika makala haya tuanenda kujadili makampuni ambayo yanatoa usafiri kwa njia ya aridhi kwa kutumia mabasi. Hivyo basi ili kutambua ni makampuni gani ya mabasi yanayo toa huduma zake kati ya mkoa wa Dar es Salaam na Mwanza tafadhari soma makala hii hadi mwisho
Mabasi ya Dar es Salaam Kwenda Mwanza
Super sami
Super Sami ni moja ya kampuni bora za usafirishaji abiria na mizigo yao baina ya mkoa wa Dar es Salaam na Mwanza. Kampuni hii inamabasi ya aina tatu katika kutoa huduma zake, ina mabasi ya kawaida, semi luxury na Luxury (VIP). huduma kwenye mabasi haya ni bora na yenye kuwafanya wateja wafurahie safari yao wawapo safarini.
-Huduma kwenye mabasi haya hutofautiana kulingana na daraja la basi. Mfano mabasi ya Luxury hutoa huduma za ziada kwa wasafiri kama vile vinywaji na vitafunwa, huduma ya internet na hata huduma ya kuchaji simu. Lakini mabasi ya daraja la kawaida hayana huduma hizo za ziada.
Zuberi bus
Hii inaweza kua ndio miongoni mwa kampuni kongwe katika nyanja ya usafirishaji wa watu namizigo yao nchini, Kutokana na kuibika kwa makampuni mapya na yenyekutumia mabasi ya hadhi ya juu kampuni hii ya Zuberi Pia imeingia kwenye ushindani huo na kufanya mabadiliko ya mabasi yake kwa kuingiza mabasi mpya na ya kisasa.
Kama unatazamia kufanya safari kwa njia ya basi kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza au Mwanza kwenda dar basi Zuberi bus iwe ni sehemu ya machaguo yako kwani kampuni hii inauzoefu wa kutosha katika swala la usafirishaji kwa njia ya mabasi.
-Kama livyo kwa makampuni mengine pia mabasi ya kampuni ya Zuberi yako katika mgawanyo wa madaraja na mabasi ya Luxury yanatoa huduma mbali mbali mbali wakati wa safari kama vile huduma ya kuangalia runinga, internet, vinywaji na vitafunwa pia hata huduma ya kuchaji simu yote hayo ni kumfanya abiria asichishwe na safari.
Princes Muro
Kama unahitaji kusafiri kwa raha basi kampuni ya Princes Muro ndio chaguo lako kwani kampuni hii inamabasi makubwa na yenye nafasi ya kutosha kua na viti vya kukufanya utulie uwapo safarini licha ya kua kampuni iliyokua na mabasi ya daraja la chini apo awali, lakini ushindani wa kimakampuni imeifanya kampuni ya Princes Muro pia kuendana na ushindani huo kwa kuleta mabasi ya kisasa nyenye mwonekano mzuri wa nje hadi ndani.
– Kampuni hii inaumiliki wa mabasi ya daraja la kawaida na yale ya semi luxury, katika mabasi ya Semi Luxury msafiri utapewa huduma za ziada kama vile vinywaji na vitafunwa, huduma ya internet na hata huduma ya kuchaji simu.
Happy Nation Express
Tunapozungumzia usafiri wa basi kutoka Dar kwenda Mwanza na Mwanza kwenda Dar basi Kampuni ya Happy Nation ndi chaguo la kwanza, Mabsi ya kampuni hii ni bora na ya kistarehe hasa kwa mabasi ya daraja la Luxury. Utulivu wa basi na huduma bora kutok kwa wahudumu utakufanya ufurahiye safari yako muda wote.
Hii ndio kampuni yenye mabasi mazuri inawezekana kuliko kampuni nyingine yoyote nchini Tanzania, kwa wale wanaopenda kusafiri kifahari basi mabasi ya Happy Nation garaja la kwanza ndio inaweza kua chaguo sahahi kwako.
Mohamed Trans Limited
Mohamed Trans ni miongoni mwa kampuni zinazotoa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo yao kutoka dar kwenda Mwanza na Mwanza kwenda Dar. Kimwonekano mabasi haya ni ya kawaida sana lakini ndio kampuni inayomiliki mabasi bora zaidi na yakuaminika kwani mabasi yake yananguvu na imara zaidi. Kwa wale wanaopenda kusafiri na usafiri wa uhakika bila kujari mwonekano wa nje wa basi hii ndio kampuni sahihi kwao kwani uhakika wa safairi ni asilkimia 90.
– Kama wewe ni msafri kwa kuangalia mwonekano wa mabasi, basi tambua kabisa usiweke akilini chaguzi y mabasi ya kampuni hii kwani inamabasi ya mwonekano wa kawaida sana lakini ndio imala na yenye kasi zaidi.
Isamilo express
Ukitoa kampuni za mabasi tuizozitaja hapo juu huwezi kuacha kuitaja kampuni ya Isamilo kwa umaarufu wake wa kua na mabasi ya luxury na nenye wendo wa kasi. Kampuni hii kutokanaa na changamoto za kiusafiri toka makampuni mengine nayo inazidi kujiimalisha kwa kuleta mabasi ya kisasa na kifahari zaidi, nje ya kamp[uni ya Happy Nations pia hii ni kampuni yenye basi za kifahari kwa wasafiri wanaohitaji kusafiri kifahari.
-Mabasi ya Luxury kwenye kampuni hii yanatoa huduma za ziada kama ilivyo kwa kampuni nyingine. Haimaanishi ya kua kampuni hii inamiliki mabasi ya kifaari daraja la juu peke yake la asha pia inamabasi ya semi luxury na daraja la kawaida pia.
Nje ya kampuni za mabasi tulizozitaja hapo juu pia kunakampuni nyingine za mabasi kama vile,
- Lucky Star
- Princes Shabaha
- Green Star Express
- Kambas
- Princes Munaa
- Najmunisa
- Simiyu Express
- Igembensabo
- Master City Limited
- Best line
Kampuni zote hapo juu zinashidana katika kila hali kuhakikisha zinatoa huduma bora kwa wasarifi katika mikoa hii ya dar na mwanza, hivyo kampuni yoyote ile utakayo ichagua itafaa kwa safari yako kwani hakuna kampuni kati ya hizo hapo juu inayotoa huduma duni kwa wateja wake.
Huduma Zinazopatikana Katika Mabasi ya Dar To Mwanza
Mbasi ya jutoka Dar kwenda Mwanza hasa yale ya daraja la juu VIP hutoa huduma mbali mbali za ziada yawapo safarini, Miongoni mwa huduma hizo ni pamoja na;
- Huduma ya vinywaji na vitafunwa
- Huduma ya kutazama Runinga
- Huduma ya Kuchaji simu
- Huduma ya Internet
- Kwa basi nyingine huenda mbali na kutoa huduma ya choo.
Mambo ya Kuzingatia Katika Kuchagua Mabasi;
Hapa tutaenda kutaja mambo ya jumla ya kuzingatia unapotaka kuchagua basi la kusafiria lakini kila mtu ana mabo yake anayo yazingatia.
- huduma bora za watumishi wa basi
- Vitu vya kukuliwaza wakati wa safari
- Hali nzuri ya basi
- Ubora wa basi
Hitimisho
Kama wewe ni msafiri na hujui ni kampuni gani ya basi unaweza kuchagua ili kufanya safiri yako iwe kutoka Dar kwend Mwanza au Mwanza kwenda Dar basi naamini maelezo yetu hapo juu yatakua yamekupa mwangaza hata kidogo.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Jinsi Ya Kujiunga na Vifurushi vya Halotel
2. Bei Mpya ya Kifurushi cha Azam Lite
3. Mfano wa Mkataba wa Kazi ya Ulinzi
4. Jinsi Ya Kujiunga na Vifurushi vya TTCL
5. Muundo wa Mkataba wa Kazi ya Kuuza Duka
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku