Nauli ya Boti Dar es Salaam Kwenda Zanzibar
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Nauli ya Boti Dar es Salaam Kwenda Zanzibar, Habari ya waki mwingine tena mwana habarika24, karibu katika mfurulizo wa makala zetu na leo katika makala hii tutaenda angazia nauli ya boti Dar es Salaam kwenda Zanzibar. Kama wewe ni msafiri au unahitaji kusafiri kuelekea zanjiabar ukitokea Dar es Salaam basi ni vizuri ukazifahamu nauli za usafiri wa boti.
Zanzibar ni miongozni mwa visiwa vyenye vivutio vizuri sana huku vikipambwa ba utamaduni uliyukuka na madhari nzuri ya kibiashara. Ifahamike ya kua Zanzibar ni sehemu ya Tanzania baada ya kutokea kwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Njia za Usafiri Dar es Salaam Kwenda Zanzibar
Ili mtu afanye safari kutok dar kwenda Zanzibar au Zanzibar kwenda Dar lazima atumie njia zifuatazo za kiusafiri.Hapa chini tumekuwekea njia za usafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar na Zanzibar kwenda Dar es Salaam.
1. Njia ya Maji – Kusafiri kwa kutumia Boti
2. Njia ya Anga – Kusafiri kwa kutumia ndege
Zanzibar na mkoa wa Dar es Salaam vimetenganishwa bna bahari ya hindi hivyo hakuana usafiri wa nchi kavu mtu akitaka kusafiri kati ya maeneo hayo mawili lazima atumia usafiri tuliouandika hapo juu.
Hivyo basi katika makala haya tutaenda jadili juu ya usafiri wa majini hasa kwa kutumia boti na nauli zake.
Sabau Ya Kusafiri kati ya Dar es Salaam na Zanzibar
Kuna faida na sababu nyingi sana zinazowafanya watu wafanye safari kati ya mkoa wa Dar es Saalaam na Zanzibar na hapa chini ni miongoni mwa sababu zinazopelekea safari hizo;
1. Sabau za Kibiashara
– Maeneo haya yote ni tajiri kwa fursa za kibiashara hivyo watu wanaoishi katika maeneo haya huingiliana kwa lengo la kufanya biashara. Mfano watu husafri kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzabar kwa lengo la kwenda kununua bidhaa hasa zile za kielektroni. Kutokana na mwingiliano wa bahari Zanzibar imekua kitovu cha bidhaa kwa Mkoa wa dar es salaam
-Pia kwa wakazi wa Zanzibar wamekua wakisafiri kwenda Dar es Salaam kwa lengo la kupeleka bidhaa zao kutafuta soko.
2. Sababu za Kiutalii
Pia watu wamekua akisafiri baina ya sehemu hizi mbili kwa lengo la kufanya utalii, Zanzabar ni kivutio kii cha utarii wakazi wa Tanzania bara na wageni kutoka nje ya Taanzania wamekua wakienda Zanzibar kufanya utalii kupitia Dar es Salaam
3. Sababuza kimapumziko na Burudani
Wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam wamekua wakifanya safari zao kwenda Zanzabar mwishini mwa wiki kwa lengo la mapumziko na kupata burukiko baada ya mihangaiko ya kikazi ya wiki nzima. Familia nyingi hufunga safari za kwenda Zanzibar ili kufanya mapumziko.
4. Kusalimia Famialia
Kumekua na mwingiliano mkubwa wa kiutendaji baina ya Tanzania bara na Zanzibara na hii ni kutokana na Muungano ulioleta nchi moja hivyo kufanya watu wa Zanzibar kufanya kazi Tanzania bara na watu wa Tanzania bara kufanya Kazi Zanzibar. Kutokana na hilo limepelekea kuwepo kwa safari za watu kutoka Tanzania bara kwenda Zanzibar na Zanzibar kwenda Tanzia bara, pale wanapokua katika wakati wa likizo.

Nauli ya Boti Dar es Salaam Kwenda Zanzibar
Usafiri wa Boti Dar es Salaam Kwenda Zanzibar
Safari ya njia ya maji kutoka Dar kwenda Zanzibar imerahisiswa na kampuni za boti ambazo ndio zinazotoa huduma ya kusafirisha abilia baina ya naeneo hayo mawili. Hapa chini Tumekuwekea baadh ya kampuni hizo za usafirishaji abilia kwa njia ya boti,
- Azam Marine
- Zanzibar Fast Ferries
- Sea Star Ferry
- Kilimanjaro Fast Ferries
Hapa tunaenda kuangazia nauli za boti kutok Dar es Salaam kwenda Zanzibar, Nauli hizi hutofautiana kulingana na daraja katika boti, Kuna iana tatu za madaraja katika Boti zinazo fanya safari zake kati ya Dar na Zanziba
- Daraja la Uchumi
- Daraja la Kwanza
- Daraja la VIP
Sasa tutazame nauli kwa kila daraja;
Tiketi ya Uchumi
Hili na daraja la watu wa kawaida ambao wanataka kusafiri kw bei nafuu, Huduma za kawaida na hakuna huduma maalumu katika daraja hili kulingana na nauli yake.
- Nauli ya daraja hili ni kati ya Tsh 30,000 – 35,000
Tiketi ya Daraja la Kwanza
Hili ni daraja la wadhifa wa kati hutoa huduma bora kwa wasafiri pia huduma za ziada kama vile vinywji na vitafunwa hutolewa katika daraja hili. Daraja hili huwafaa hasa wale wanaopenda kusafiri bila kubugudhiwa yani kwa furahaa.
- Nauli katika daraja hili ni kati ya Tsh 50,000 – 60,000
Tiketi ya Daraja la VIP
Hili nio daraja bora zaidi katika boti na hujumuisha wale wanaopenda kusafiri katika hali ya kifahari. Katika daraja hili kunahuduma za kila aina ikiwemo chakula, vinywaji na hata sehemu za mapumziko kwa wasafiri.
- Nauli katika daraja hili ni kati ya Tsh 80,000 na zaidi.
Ratiba za Safari za Boti Kutoka Dar es Salaam Kwenda Zanzibar
Kama tulivyosema hapo awali makala hii itajikita zaidi kwenye kuangalia nauliza boti Dar es Salamm kwenda Zanzibar laki haina budi pia kama tukikupa mchanganuo wa ratiba za usafiri huo wa boti.
Kwenye swala la muda wa kuanza safari upande wa boti sio sawa na ule wa mabasi ya mikoani kwani hapa swala la kluanza safari kwa kila kampuni inayomiliki boti hutofautiana lakini ratiba ya jumaya kuanza sali iko kama ifuatavyo;
– Kuna boti zinazo anza safari zake Saa 12:00 asubuhi
– Nyingene Saa 4:30 asubuhi
– Nyingine Saa 10:00 jioni
– Na nyingineSaa 12:00 jioni
Kira boti ina muda wake wa kundoka kulingana na latiba ya kampuni husika hivyo basi muda wa kuondoka kwa boti huandikwa kwenye tiketi ya abiria na cha zaidi abiria hushauliwa kuwahi kufika bandarini nusu saa kabla ya boti kuanza safari zake.
Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kuanza Safari;
Tunza Tiketi Yako
Abiria mara baada ya kukata tiketi yako unashauriwa kuitunza kwa umakini kwani ndiyo dhamana ya ya safari yako, Pindi utakapo ipoteza italeta changamoto maana ufuatiliaji wa uhalali wa malipo ya tiketi unaweza kuchukua mda ukajikuta umechwa na Boti yako.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Vifurushi vya Starrtimes Na Bei Zake
2. Kitambulisho cha Usalama wa Taifa
3. Jinsi ya kubadilisha kifurushi cha Startimes
4. Vifurushi vya DSTV Na Bei Zake
5. Jinsi ya Kusajiri Kampuni Tanzania
6. JINSI ya Kupata TIN Number Online
7. jinsi ya Kujisajili na Huduma za NBC Mobile Banking
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku