Jinsi ya Kutoa Pesa Kwenye Akaunti ya NBC Bank
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
BONYEZA HAPA KUJIUNGA NA TELEGRAM CHANNEL YETU
Habari mwana Habarika24, karibu tena kwenye makala nyingi ambayo itaenda kukupa maelekezo juu ya Jinsi ya kutoa pesa kwenye akaunti ya NBC bank, Kama tunavyojua Bank ya NBC kama zilivyo banki nyngine inanjia mbali mbali za za kumfanya mteja wake aweze kutoa pesa alizozihifazi kwenye banki hiyo.
Banki ya NBC ni miongoni mwa mabenki makubwa zaidi Tanzania na inatoa huduma ya kutunza pesa kwa wateja wengi sana, nje ya huduma za kibenki lakini pia banki ya NBC hufadhiri mpira wa miguu katika Ligi kuu ya NBC Tanzania bara.Nje ya kutoa pesa kutoka katika banki ya NBC pia wewe mtumiaji wa banki ya NBC ni lazima pia utambue njia mbali mbali za kuweza katazama salio lililopo kwenye akaunti yako ya NBC, ili kutazama salio lako tafadhari bonyeza hapa.

Njia za Kutoa Pesa Kwenye Akaunti ya NBC
Kama tulivyosema ao awali kua benki ya NBC kama zilivoy kua benki nyingine pia inanjia mbali mbali ambazo mteja wake anaweza kuzitumia ili kuweza kutoa pesa katika akaunti yake ya NBC. Hapa chini tunaenda kukuonyesha njia tofauti tofauti unazoweza kuzitumia ili kuweza kutoa pesa zilizopo kwenye akaunti yako.
- Njia ya Tawi la Benki
- Njia ya Simu Banking
- Njia ya ATM
- Njia ya Wakala
Hapa tutaenda kukutolea maelezo kwenye njia 4 tofauti tofauti ambazo unaweza zitumia ili kuweza kutoa pesa kwenye akaunti yako ya NBC.
Njia ya Tawini
Mteja wa NBC anaweza kutoa pesa zilizoko kwenye akaunti yake ya NBC kwa kutembela tawi la benki hiyo ya NBC akiwa na Kitambulisho chake za Taifa, Kitambulisho cha Mpigakula au kadi ya benki ya NBC. Baada ya kufika tawini utajaza formu ya kuomba kutolea pesa kisha utaenda dirishani na kupewa kiasi cha pesa kama ulivyoandika kwenye form ya kuombea kutoa pesa.
Njia ya Simu Banking
Njia hii inaweza tumika kwa namna mbili tofauti
a) Unaweza tumia nji hii kwa kuhamisa pesa kutoka kwenye akaunti yako ya NBC na kupeleka kwenye mtandao wa simu unaoutumia, utafanya hivyo kwa kupiga namba *150*55# kisha fuata maelekezo yote ili kuweza kuhamisha pesa kwenye akaunti yako na kuzipeleka kwenye simu kadi yako.
b) Njia ya pili ni kumtembele wakala wa NBC ukiwa na simu yako na kutoa pesa kwenye akaunti yako ukitumia njia ya simu benki kwa kupia *150*55# kisha ufuate maelekezo yote na uweze kuhamisha pesa iliyoko kwenye akaunti yako na kwenda kwa wakala.
Njia ya ATM
Njia nyingine ya mteja wa benki ya NBC kuweza kutoa pesa kutoka kwenye akaunti yake ni kutumia njia ya ATM, njia hii hutumika pale mteja wa NBC atakapoweza kutembela ATM mashine ya NBC akiwa na kadi yake ya banki ya NBC. Kwenye mashine ya ATM ya NBC mteja ataingiza kadi na itahitaji mteza aingize neno siri lake (nywira) kisha utachagua chaguzi la kutoa pesa utaweka kiasi na kuthibisha na pesa zitatoka kwenye akaunti yako.
Njia ya Wakala
Hii pia ni njia ambayo mteja wa NBC anaweza kuitumia ili kuweza kutoa pesa kutoka kwenye akaunti yake. Mteja wa NBC itampasa kutembelea kwa wakala yoyote yule akiwa na kadi yake ya NBC au sim benki ya NBC. kwa kufanya hivyo basi anaweza kutoa kiasi akitakacho cha pesa kutoka kwenye akaunti yake ya NBC Bank.
Mawasiliano ya NBC
Kama unatatizo lolote juu ya kuangalia salio la akaunti yako ya NBC au kuhusu huduma za NBC basi basi tumia mawasiliano haya hapa chini kuweza kuwafikia wahusika;
- +255 76 898 4000,
- +255 22 219 3000
- 0800711177
Mawasiliano ya namba zote hizo hapo juu ni bure kabisa.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Kozi za Diploma na Ada Za Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA)
2. Ada na Kozi Zitolewazo Na Chuo Kikuu Cha Sokoine SUA
3. Orodha ya Shule za Sekondari Mkoa wa Njombe
4. Orodha ya Shule za Sekondari Mkoa wa Rukwa
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku