Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anawajulisha waombaji kazi wote wa kada ya MARINE ENGINEER II, DECK OFFICER II, ONBOARD ATTENDANT II, ORDINARY SAILOR II, MOTORMAN II ambazo mwajiri wake ni Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) kuwa kuna mabadiliko ya ratiba ya usaili wa vitendo.
Usaili wa vitendo utafanyika tarehe 31 Julai,2025 badala ya tarehe 30 Julai,2025. Aidha, eneo na muda wa usaili utabaki kama ulivyotolewa kwenye tangazo la awali la kuitwa kwenye usaili.