Wachezaji wanaolipwa pesa nyingi Tanzania 2024, Habari mwanamichezo wa Habarika24, karibu katika makala hii fupi itakayoenda kukuonyesha orodha ya wachezaji 10 wanaolipwa mishahara mikubwa katika ligi kuu ya NBC kwa mwaka 2024.
Kama unashahuku ya kutaka kujia ni wachezaji gani na wanatoka klabu gani wanalipwa pesa ndefu zaidi kwenye ligi kuu ya NBC basi makala hii itakupa kila kitu unachotamani kukifahamu kwa msimu wa 2024.
Ligi kuu ya NBC imekua ni miongoni mwa ligi bora zaidi Afrika mashariki na Afrika kwa ujumnla wake kwani kwenye ubora wa viwango vya CAF ligi ya Tanzania (NBC Premier League) inashika nafasi ya 5 kwa ubora barani Afrika.
Hii ni kutokana na uwekezaji unaofanywa katika klabu zinazoshiriki katika ligi hiyo. Mfano kwa klabu kama Yanga, Simba na Azam wamewekeza pesa nyingi sana katika vilabu vyao na hivyo kuwavutia wachezaji wengi wazuri wa kimataifa kwa kuwalipa vizuri. Wamekua wakitoa mishahara mizuri kwa wachezaji hivyo kufanya wachezaji wenye uwezo mkubwa kutamani kucheza katika ligi hii.
Kwa mujibu wa chanzo chetu hii ni orodha ya Wachezaji 10 wanaolipwa Mishahara mikubwa Ligi Kuu ya NBC.
Wachezaji wanaolipwa pesa nyingi Tanzania 2024
Nafsi | Jina la Mchezaji | Kiasi Anacholipwa | Klabu Anayocheza |
1 | Stephen Aziz Ki | 30M | Young Africans |
2 | Clatous Chama | 28M | Simba SC |
3 | Ali Ahmada | 25M | Azam FC |
4 | Feisal Salum | 23M | Azam FC |
Orodha ya Wachezaji Wengine Wanaolipwa Mishahara Mizuri zaidi Tanzania
Ukiachilia mbali wachezaji wa nne tuliowaweka kwenye orodha hapo juu pia katika ligi ya NBC kuna wachezaji wengine wengi tu wanaolipwa pesa nyingi zaidi kama mishahara yao kutokana na vipaji vyao vya uchezaji.
Hapa chini ni orodha ya wachezaji wengine wanaolipwa pesa nyingi zaidi katika klabu zao
- Luis Miquisone
- Pacome Zouzoua
- Saidoo Ntibanzokiza
- Henock Inonga
- Fabrice Ngoma
- Djigui Diarra
- Ayoub Lakred
- Kibu Denis
- Maxi Mzengeli
Ukiangalia vizuri kutoka kwenye orodha hiyo hapo juu utaona kua vilabu kama Simba SC, Yanga SC na Azam FC ndio vinavyo ongoza kwa kulipa mishahara mizuri zaidi kwa wachezaji wake huku ligi kuu ya NBC ikiwa na ushiriki wa timu 16.
Soma Pia;
>>JINSI ya Kutumia Kadi Ya GUSA AzamPesa
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku