Vilabu Bora Afrika 2025/2026 (CAF Club Ranking)
CAF Orodha Ya Vilabu Bora Afrika 2025/2026 (CAF Club Ranking),Vilabu Bora Afrika 2025/2026 CAF Ranking – CAF Ranking of African Clubs 2025, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetangaza orodha mpya ya vilabu bora Afrika kwa msimu wa 2025/2026, ikionyesha mabadiliko makubwa katika mandhari ya soka barani Afrika. Orodha hii inazingatia utendaji wa vilabu katika mashindano ya kimataifa na ya ndani, hususan Champions League ya Afrika na Confederation Cup.
Al Ahly SC kutoka Misri inaendelea kudumisha nafasi yake kama klabu bora zaidi Afrika, ikifuatiwa kwa karibu na Esperance Tunis.
Orodha ya Vilabu Bora Afrika CAF 2025 Club Ranking
Rank | Club | 2020–21 | 2021–22 | 2022–23 | 2023–24 | 2024–25 | Total |
1 | Al Ahly | 6 | 5 | 6 | 6 | 4 | 78 |
2 | Mamelodi Sundowns | 3 | 3 | 4 | 4 | ≥5 | ≥62 |
3 | Espérance de Tunis | 4 | 3 | 4 | 5 | 3 | 57 |
4 | Simba | 3 | 2 | 3 | 3 | ≥4 | ≥48 |
5 | RS Berkane | 1 | 5 | 0 | 4 | ≥4 | ≥47 |
6 | Pyramids | 3 | 2 | 2 | 1 | ≥5 | ≥42 |
7 | Zamalek | 2 | 2 | 2 | 5 | 2 | 42 |
8 | Wydad AC | 4 | 6 | 5 | 2 | 0 | 39 |
9 | USM Alger | 0 | 0 | 5 | 3 | 2 | 37 |
10 | CR Belouizdad | 3 | 3 | 3 | 2 | 2 | 36 |
11 | Young Africans | 0 | 0 | 4 | 3 | 2 | 34 |
12 | Al-Hilal | 1 | 1 | 2 | 2 | 3 | 32 |
13 | ASEC Mimosas | 0 | 1 | 3 | 3 | 2 | 33 |
14 | TP Mazembe | 2 | 3 | 0.5 | 4 | 1 | 30.5 |
15 | Orlando Pirates | 2 | 4 | 0 | 0 | 4 | 30 |
16 | Raja CA | 5 | 3 | 3 | 0 | 2 | 30 |
17 | Petro de Luanda | 1 | 4 | 2 | 3 | 0 | 27 |
18 | ASFAR Rabat | 0 | 0 | 2 | 0 | 3 | 21 |
19 | Mouloudia Algiers | 3 | 0 | 0 | 0 | 3 | 18 |
20 | Sagrada Esperança | 0 | 1 | 0 | 1 | 2 | 16 |
21 | CS Constantine | 0 | 0 | 0 | 0 | 3 | 15 |
21 | Stellenbosch | 0 | 0 | 0 | 0 | 3 | 15 |
23 | Al-Masry | 0 | 2 | 0 | 0 | 2 | 14 |
23 | Rivers United | 0 | 0 | 2 | 2 | 0 | 14 |
25 | JS Kabylie | 4 | 0 | 3 | 0 | 0 | 13 |
26 | Dreams FC | 0 | 0 | 0 | 3 | 0 | 12 |
27 | Stade Malien | 0 | 0 | 0 | 2 | 0.5 | 10.5 |
28 | Horoya | 2 | 1 | 2 | 0 | 0 | 10 |
29 | Future | 0 | 0 | 0.5 | 2 | 0 | 9.5 |
30 | Étoile du Sahel | 1 | 2 | 0 | 1 | 0 | 9 |
Umuhimu wa Vilabu Bora Afrika
Vilabu bora vya mpira wa miguu barani Afrika vimekua na umuhimu mkubwa katika maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu na jamii kwa ujumla. Hapa chini ni baadhi ya faida za kuwa na virabu bora barani Afrika
- Huvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi
- Huongeza mapato ya serikali kupitia kodi
- Huunganisha watu wa jamii tofauti
- Hukuza vipaji vya vijana na kuwapa nafasi ya kujipatia riziki
- Huimarisha hadhi ya nchi kimataifa
- Huvutia wachezaji bora kutoka nchi mbalimbali
Nafasi ya Simba na Yanga kwenye Orodha Ya Vilabu Bora Afrika 2025
Vilabu vya Tanzania vya Simba na Young Africans (Yanga) vimeendelea kuimarisha nafasi yao katika ramani ya soka barani Afrika. Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, vilabu hivi viwili vikubwa vya Tanzania vimekuwa vikishiriki kwa ufanisi katika mashindano ya kimataifa, hususan Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika.
- Simba iko nafasi ya 4
- Yanga iko nafasi ya 11
Hitimisho
Vilabu hivi vimekuwa mstari wa mbele katika kuboresha viwango vya soka Afrika. Uwekezaji wao katika miundombinu, maendeleo ya vijana, na teknolojia ya kisasa umechangia pakubwa katika mafanikio yao. Kadri soka ya Afrika inavyoendelea kukua, vilabu hivi vitaendelea kuwa mfano wa kuigwa kwa vilabu vingine barani.
Simba itashika nafasi ya kwanza na yanga wakasome sana
Nabado wale al ahly na wenzake watashuka simba achukue namba moja
Waliosema hawachezi waangalie wasije wakamkuta simba amekuwa mithili ya barcelona na huyo mpanzu kila siku kiwango kinapanda
Mliokimbia mwashegeshi rudini make huku mambo yanaenda ni juice na kamnyesho2