Tiketi na Bei ya Viingilio vya Wiki ya Mwananchi 2025
Tiketi na Bei ya Viingilio vya Wiki ya Mwananchi 2025 – Timu ya Yanga imeanza kuuza tiketi za tamasha la kilele cha Wiki ya Mwananchi 2025, litakalofanyika tarehe 12 September 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Hii ni fursa muhimu kwa mashabiki wa Yanga kujumuika pamoja na kusherehekea klabu yao. Tiketi zimeanza kuuzwa katika Makao Makuu ya Klabu Jangwani, maduka ya TTCL nchi nzima, na kupitia mitandao ya simu.
Ikiwa ni maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa 2025/2026 klabu ya Yanga tayari imesha weka hadharani viingilio vitakavyo tumika kwenye sherehe za wiki ya Mwanachini
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram klabu ya yanga imesha weka gharama za viingilio kwa wiki ya mwananchi itakayofanyika siku ya tarehe 12/09/2025.
Tiketi na Bei ya Viingilio vya Wiki ya Mwananchi 2025
Viwango vya Tiketi:
Hapa chini ni mwongozo wa bei za tiketi za sherehe ya Wiki ya Mwananchi
Mzunguko – Tsh 5,000
Orange – Tsh 10,000
Vip C – Tsh 15,000
Vip B – Tsh 30,000
Vip A – Tsh 50,000
Royal – Tsh 300,000
VVIP – Tsh 600,000
Jinsi ya Kununua tiketi za Wiki ya mwananchi kupitia mitandao ya Simu
Maeneo ya Kununua Tiketi:
- Makao Makuu ya Klabu Jangwani: Tiketi zinapatikana kwa urahisi kwa mashabiki wanaoishi karibu na makao makuu ya klabu.
- Maduka ya TTCL Nchi Nzima: Mashabiki wanaweza kupata tiketi kwenye maduka ya TTCL yaliyoenea kote nchini.
- Mitandao ya Simu: Kwa urahisi zaidi, tiketi zinaweza kununuliwa kupitia huduma za mitandao ya simu, kurahisisha upatikanaji wake bila kwenda moja kwa moja kwenye vituo vya mauzo.
Mashabiki wote wa Yanga wanahimizwa kuchukua tiketi mapema ili kuepuka usumbufu na kuhakikisha wanapata nafasi ya kushiriki katika tamasha hili kubwa la Wiki ya Mwananchi 2025.
Leave a Reply