Tetesi za Usajili Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2025/2026

Tetesi za Usajili Ligi Kuu NBC Tanzania Bara

Tetesi za Usajili Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2025/2026

Hapa tutaenda kuangali tetesi za usajili kwa baadhi ya vilabu vikubwa vinavyoshiriki katika ligi kuu ya NBC kwa msimu wa 2025/2026

Klabu ya Yanga

  • Yanga SC imefikiahatua za mwishoni katika kukamilisha usajili wa mchezaji Offen Chikola anae cheza nafasi ya Kiungo Mshambuliaji akiwa na Umri wa miaka 26 kutokea klabu ya Tabora Utd Kwa mkataba wa miaka 2.
  •  Yanga Sc inafanya mawasiliano Kiungo Mshambuliaji raia wa Gambia Gibril Sillah Sillah mwenye Umri wa miaka 26 ambaye kwa sasa yupo huru baada ya kumaliza mkataba wake kwenye klabu ya Azam FC kwaajili ya kunasa saini yake kwa msimu wa2025/2026.
  • Yanga Sc imekamilisha usajili wa Kiungo mkabaji, Abdulnassir Mohammed Abdallah Kutoka Mlandege FC kwa mkataba wa miaka mitatu.
  • Yanga Sc imekamilisha usajili wa Mchezaji Aboubakar Nidhar Othman (Ninju ) aliyekuwa kwa mkopo JKU SC ya Zanznibar akitokea timu ya vijana ya Azam FC, Ninju (17).
  • Uongozi wa klabu ya Young Africans umeachana na kiungo aliyekuwa anaitumikia Klabu hiyo kwa mkopo akitokea Singida Black Stars Aziz Andambwile baada ya mkataba wake kuisha.

Klabu ya Simba

  • Mshambuliaji Cyprian Kipenye na Kiungo Morice Abraham ni majina pekee aliyoyapitisha Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba SC, Fadlu Davies baada ya kuwafuatilia kwenye majaribio klabuni hapo.

Klabu ya Azam FC

  • Klabu ya Azam  Imekamilisha Usajili wa Golikipa, Aishi Salum Manula Mwenye Umri wa Miaka 29 Kwa Mkataba wa Miaka Miwili kutoka Simba SC kwa uhamisho huru baada ya mkataba wake na Simba Kumalizika.
  • Klabu ya Azam FC imekamilisha usajili wa mlinzi, Lameck Lawi Kutoka Coastal Union ya mkoani Tanga.
  • Klabu ya Azam FC imekamilisha Usajili wa Kocha, Florent Ibenge mwenye Umri wa miaka 63 Kutoka Al Hilal SC ya Sudan.
  • Klabu ya Azam Imekamilisha Usajili wa Kiungo Mkabaji, Himid Mao mwenye Umri wa miaka 32 kutoka Ghazl El Mahalla ya Misri.

Klabu ya Tabora United

  • Klabu ya Tabora United ipo kwenye hatua za mwisho Kukamilisha Usajili wa Golikipa wa timu ya Taifa ya Ghana, Frederick Asare mwenye Umri wa miaka 26 Kutoka Asante Koto kama Mchezaji huru

Klabu ya Dodoma Jiji

  • Klabu ya Dodoma Jiji imekamilisha Usajili wa Mshambuliaji, Andrew Simchimba Kutoka Geita Gold FC.
  • Mashambaliaji huyo wa zamani wa vilabu vya KMC, Azam Fc na Ihefu Fc msimu uliopita alifanukiwa kufunga jumla ya Mabao 18 ya NBC Championship.
  • Klabu ya Dodoma Jiji imekamilisha usajili wa aliyewahi kuwa kocha wa Tabora United, Anicet kiazayidi ikiipiku coastal Unioni baada ya kuweka donge nono zaidi yao.

Klabu ya Mashujaa FC

  • Klabu ya Mashujaa FC ya Mkoani Kigoma imekamilisha Usajili wa aliyekuwa Mlinzi wa Kati wa Kagera Sugar FC ya Kagera, Mohamed Mussa Kwa Mkataba wa miaka miwili.

Klabu ya Singida Black

  • Klabu ya Singida Black Stars imekamilisha Usajili wa aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Klabu Yanga, Miguel Gamondi Kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Klabu ya Pamba Jiji FC

  • Klabu ya Pamba Jiji FC Imekamilisha Usajili wa Mshambuliaji, Abdallah Idd Pina kutoka Mlandege FC ya Zanzibar Kwa uhamisho huru baada ya kumaliza mkataba wake na Mlandege FC.

Wanaondoka Ligikuu ya NBC

  • Klabu ya Ismaily Sc ya Misri imekamilisha Usajili wa aliyekuwa kocha wa Yanga Sc, Miloud Hamdi kama Kocha Mkuu.
  • Klabu ya Hassania d’Agadir ya Morocco ipo kwenye hatua za mwisho Kukamilisha Usajili wa aliyekuwa Kiungo mkabaji wa Simba SC, Fabric Ngoma mwenye Umri wa miaka 31.
  • Wengine ni Kennedy Musonda ambaye tayari ameshaondoka nchini Tanzania, Wakati Winga wao Jonathan Ikangolombo akiwa kwenye mazungumzo juu ya hatma yake ya kutolewa kwa mkopo ama kuvunjwa kwa kandarasi yake
  • Mlinda lango, Abubakar Khomeiny pia nae hatokuwa sehemu ya kikosi hicho kuelekea msimu ujao wa 2025/2026.

etesi za usajili ligi kuu NBC Tanzania Bara 2025/2026 zinaashiria ushindani mkali sokoni na juhudi za klabu kuimarisha vikosi. Yanga, Simba, Azam, Singida BS na Mtibwa Sugar zinashindana kwa ajili ya saini za wachezaji wenye umahiri. Mashabiki wanatarajia kuona vikosi vikali vinavyochanganya uwezo wa ndani na nje. Endelea kufuatilia mwongozo wetu kwa kila taarifa mpya na uhakika.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FQA)

Q1: Dirisha kubwa na dogo ya usajili ni lini?
A: Dirisha kubwa limefunguliwa kabla ya Agosti 15, 2024; dirisha dogo linafikia Jan 2025 .

Q2: Mtibwa Sugar itaonekana namna gani msimu huu?
A: Baada ya kupanda, Mtibwa Sugar ina mpango wa kuongeza nguvu kwa wachezaji wapya kuelekea ligi kuu .

Q3: Je, klabu kubwa zinawekeza vipi?
A: Simba, Yanga na Azam zinaendelea kuwania wachezaji kama Fei Toto na Diarra, kushindana sokoni .

Q4: Nani mwaminifu kati ya Singida BS?
A: Benson Mang’olo ameondoka, lakini Singida inalenga kupata mshambuliaji kama Stephen Amankona mwenye rekodi nzuri .

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!