Simba Sc vs Singida Black Stars Nusu Fainali CRDB Federation CUP 31 Mei 2025
Baada ya kumalizana na michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika wekundu wa msimbazi Simba Sc tarehe 31 Mei inaenda kutupa karata yake katika mchezo wa nusu fainali ya CRDB Federation Cup.
Nusu fainali hii ya CRDB Federation Cup itawakutanisha wababe hawa wawili wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara Simba Sc vs Singida Black Stars baada ya mchezo wa ligi kuu kati ya miamba hawa 2 utakaofanyika tarehe 28 Mei 2025.
Maelezo Muhimu ya Mchezo Huu Wa Nusu Fainali CRDB Federation Cup
Ligi: CRDB Federation Cup
Hatua: Nusu Fainali
Timu: Simba Sc vs Singida Black Stars
Uwanja: Tanzanite Kwaraa, Manyara
Muda: 15:30 Mchana
Mchezo huu utakua mchezobwa ushindani sana na atakae shinda katika mechi hii atajiungana na klabu ya Yanga katika hatua ya Fainali ya CRDB Federation Cup kwa msimu huu wa 2024/2025.
Matarajio ya Mashabiki
Mashabiki wa soka nchini Tanzania wanatazania kuona mchezo wa kuvutia na huku wengi wakitarajia kuona hasira za mnyama simba baada ya kujeruhiwa kwa kukosa ubingwa wa kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kupingwa na klabu ya RS Berkane.
Mashabiki wa Yanga pia wanausubilia kwa hamu ya kutosha mchezo huu ili kuona mtaninwao nini atafanya na kama ataweza kukata tiketi ya fainali mbele ya wababe wa nafasi ya 3 katika ligi kuu ya NBC Tanzania bara.
Kulekea mchezo huu Kisiwa24 blog tutakuletea taarifa zote za msingi hata siku ya mchezo ikiwa ni pamoja na,
-Kikosi cha Simba kitakachocheza na Sigida black Stars Nusu Fainali CRDB Federation Cup
– Live Matokeo ya Simba vs Singida Black Stars Fainali CRDB Federation Cup.
Hivyo usiache kutembelea kwenye site yetu upamde wa Michezo ili kuweza kupata taarifa zote kuhusu mchezo huu wa nusu fainali ya CRDB Federation Cup kati ya Simba Sc vs Singida Black Stars 31 Mei 2025