
Orodha ya Vyuo Vinavyotoa Kozi ya Maabara na Matibabu (Medical Laboratory) Ngazi ya Diploma na Degree
- Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
- Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afya na Sayansi Shirikishi
- Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala nchini Tanzania
- Kilimanjaro Christian medical university college
- Muslim university of Morogoro
- Ruaha catholic university (RUCU)
- St john’s university of Tanzania
- St. Francis chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi
- Chuo kikuu cha jimbo la Zanzibar
Sifa za Kujiunga na Medical Laboratory Ngazi ya Diploma na Degree
ili uweze kujunga na chuo chochote kile kinachotoa kozi ya matibabu ya maabara (medical laboratory) kwa ngazi ya Diploma ni lazima mwombaji awe na sifa zifuatazo
– Mwombaji awe amehitimu elimu ya sekondari kidato cha Sita
– Awe na ufaulu mzuri kwenye mtihani wa mwisho na kutunukiwa cheti cha ACSEE kwenye masomo ya kemia, biolojia na fizikia.
– Kwa baadhi ya vyuo huitaji mwombaji awe na uwelewa wa kuongea na kuandika kingereza vizuri
– Mwombaji awe amehitimu Cheti cha Ufundi cha mwaka mmoja (NTA Level 5) katika Maabara ya Tiba au cheti kinacholingana nacho.
Sifa za kujiunga na Kozi ya Maabara ya Matibabu Ngazi ya Diploma ya Kawaida
– Mwombaji anapswa kua na ufaulu wa chini wa pass 4 kutoka masomo ya msingi ikiwa ni pamoja na kemia, biolojia, na sayansi ya fizikia/uhandisi katika cheti chako cha mtihani wa elimu ya sekondari (CSEE).
– Kufaulu katika hisabati ya msingi ( basic mathematics) na lugha ya Kiingereza ni faida iliyoongezwa.
Sifa za kujiunga na Kozi ya Sayansi ya Maabara ya Tiba (BMLS) Ngazi ya Shahada ya Kwanza (Bachelor’s Degree)
Ili kupokelewa katika Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Maabara ya Tiba (BMLS mwombaji anapaswa kua na sifa zifuatazo;
– Anatakiwa kuwa na ufaulu wa credit 3 katika masomo ya Fizikia, Kemia na pointi 6 katika cheti chake cha mtihani wa elimu ya sekondari; yaani mwombaji awe na angalau daraja C katika Kemia na angalau daraja D katika Biolojia na daraja E katika Fizikia.
Mapendekezo ya mhariri:
1. Sifa za Kujiunga Archbishop Mihayo University College of Tabora
2. Vigezo Na Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Ardhi Dar es Salaam
3. Sifa Za Kujiunga Na Arusha Technical College
4. Sifa Za Kujiunga Na Chuo cha ardhi Tabora ARITA 2024/2025