
Kabla hujatuma maombi kwenda kwenye chuo chochote ili kujiunga na kozi za cheti basi ni muhimu kwanza kw wewe kuweza kusoma makala hii
Kozi Za Certificate (Cheti)
Kuna viwango takribani 4 katika kiwango cha elimu cha cheti; Viwango hivyo vya elimu ni pamoja na;
- Astashahada ya Msingi (NTA Level 4)
- Cheti cha Ufundi (NTA Level 5)
- Diploma ya Kawaida (NTA Level 6)
- Shahada (Degree Programmes)
Ili kujiunga na ngazi hizo hapo juu za elimu lazima uwe na sifa maalumu, na kumbuka kua sifa za kujiunga na kozi za certificate hubadilika kutoka ngazi moja ya elimu hadi nyingine. Hapa chini tumekuwekea sifa za kujiunga na kozi za certificate (cheti) kwa kila ngazi ya elimu kuanzia NTA LEVELA 4 hadi SHAHADA.
Sifa za kujiunga na kozi za Certificate
Kutokana na utofauti wa sifa kutoka ngazi moja hadi nyingine ya kielimu basi hapa chini tumetenganisha sifa hizo kulingana na ngazi hizo za kielimu;
Astashahada ya Msingi (NTA Level 4)
Ili uweze kujiunga na ngazi ya elimu ya Astashahada ya Msingi basi ni lazima uwe na sifa na vigezo vifuatavyo
1. Elimu ya Kidato Cha NNE
Ili uweze kujiunga na kozi hii ya astashahada ya msingi ni lazima uwe umehitimu elimu ya sekondari kidato cha nne, Pia uwe umepata ufaulu wa masomo manne kiwango cha “D” ukiachilia mbali masomo ya Dini.
2. Cheti cha NVA Level 3
Pia lazima uwe na Cheti cha NVA Level 3 katika fani husika
3. Cheti cha NVA Level 2
Mbali na sifa hizo hapo juu pia ili uweze kujiunga na ngazi hii ya elimu ni lazima uwe na Cheti cha NVA Level 2 hasa kwa wale wanaotaka kujiunga na kozi za uhazili
Cheti cha Ufundi (NTA Level 5)
Ili uweze kujiunga na Cheti cha Ufundi (NTA Level 5) hakikisha unasifa zifuatazo hapa chini;
1. Elimu ya Kidato cha Nne (CSEE)
Kwa yule muhitimu wa kidato cha nne lazima awe na Cheti cha Astashahada cha NTA Level 4 kwenye kozi unayotaka kusomea na cheti hicho kiwe kunatambulika na NACTVET.
2. Elimu ya Kidato cha Sita (ACSEE)
Ili kujiunga na kozi ya cheti cha ufundi basi lazima mwombaji awe na ufaulu japo wa pass moja kwenye masomo yoyote yale isipokua masomo ya kidini
3. Kozi za Ugavi na Ununuzi
Kwa yule mwenye elimu ya kidato cha sita basi awe na ufauli wa pass moja na subsidiary mbili kwenye masomo yoyote yali ukiachilia mbali masomo ya kidini. Sifa hii uhusisha kozi za ugavi na ununuzi peke yake.
4. Kozi za Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu (HR)
Kwa kozi za utawala na usimamizi wa rasilimali watu (HR) mwombaji aliyehitimu kidato cha sita anapaswa awe na ufaulu wa pass moja na pia subsidiary moja kwenye masomo yoyote yale isipokua masomo ya kidini.
Kozi ya Diploma ya Kawaida (NTA Level 6)
Ili uweze kujiunga na Kozi ya diploma ya kawaida ya NTA Alevel 6 ni lazima uwe umaehitimu kidato cha nne na unacheti cha ufundi cha NTA level 5 kwenye kozi unayotaka kuomba na kiwe kinatambulika na NACTVET
Kozi za Shahada (Degree)
Ili kuweza kujiunga na kozi za shahada basi unapaswa kuwa na sifa zifuatazo
- Kwa elimu ya kidato cha sita unapaswa kua na ufaulu wa principal mbili katika masomo yako ya msingi
- Kwa elimu ya Diploma ya kawaida unapaswa kua na GPA inayoanzai 3.0 na kuendelea kwenye kozi unayotaka kuomba.
Muda wa Kozi
Kozi ya Astashahada ya Msingi (NTA Level 4)
-Muda wa kozi hizi ni mwaka mmoja tu wenye mihula miwili.
Kozi ya Cheti cha Ufundi (NTA Level 5)
-Kozi hizi za cheti cha ufundi hudumu kwa muda wa mwakoa mmoja tu ambao pia huwa na mihula miwili.
Kozi ya Diploma ya Kawaida (NTA Level 6)
-Kozi hizi za diploma ya kawaida hudumu kwa muda wa mwakoa mmoja tu ambao pia huwa na mihula miwili.
Kozi ya Shahada (Degree)
-Muda wa kozi hizi ni miaka mitatu.
Kumbuka kama tulivyosema hapo awali sifa na vigezo vya kuweza kujiunga na kozi hizi zinatofautiana kutoka koazi moja hadi kozi nyingine. Hivyo basi kama unataka kujiunga na kozi flani hakikisha unasoma sifa na vicezo vyake kwa kozi hiyo husika.
Machaguzi ya Mhariri;
1. Sifa Za Kujiunga Na Kozi Ya Information Technology (IT)
2. Sifa Za Kujiunga Na Kozi Za Uchumi Tanzania
3. Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Mipango Dodoma