Sifa Za Kujiunga na Kozi ya Nursing Ngazi ya Diploma, Habari kama wewe ni mhitimu wa sekondari na unahitaji kujiunga na kozi ya uuguzi katika ngazi ya diploma basi usiwe na shaka kweni hapa tutaenda kukupa mwongozo wa sifa na vigezo ya kusoma Nursing k atika vyuo mbali mbali vinavyotoa kozi hiyo ya uuguzi.
JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Wakati unafikilia kufanya chaguzi ya chuo cha kusoma kozi ya uuguzi (Nursing) basi ni vyema kufahamu kwanza sifa na vigezo vya msingi vya kujiunga na kozi hiyo kwa ngazi ya diploma Kwa kufanya hivyo itakua na msaada kwako kwa kufanya uamuzi wa kuchagua chuo gani cha kusoma kozi ya uuguzi kwa ngazi ya Diploma
Sifa Za Kujiunga na Kozi ya Nursing Ngazi ya Diploma
Vigezo na sifa za kusoma kozi ya uuguzi (Nursing) kwa ngazi ya Diploma kwa vyuo vingi nchini Tanzania hutofautiana kutoka chuo kimoja kwenda chuo kingine, lakini chuo vingi huwa na mahitaji ya waombaji waliokua na elimu ya sekondari ya kidato cha sita akiwa na ufaulu mzuri wa masomo ya sayansi kama vile kemia, bilojia na fizikia.
Pia zaidi ya kua na elimu ya sekondari ya kidato cha sita yenye ufaulu mzuri waombaji wanatakiwa kuwa na cheti cha ufundi cha mwaka mmoja (NTA Level 5) katika uuguzi au kinacholingana nacho kabla ya kukubaliwa kujiunga na programu ya diploma ya uuguzi.
Diploma ya uuguzi ndio chanzo cha maalifa kwa wanafunzi wanaohitajika kujiunga na ngazi ya degree ya uuguzi inayofanyika kwa muda wa miaka minne.
Orodha ya Vyuo Vinavyotoa Kozi ya Nursing Ngazi ya Diploma
Hapa chini ni baadhi ya vyuo vinavyotoa kozi ya uuguzi (Nursing) ngazi ya Diploma Tanzania
- Chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi Muhimbili,
- Chuo kikuu cha St john cha Tanzania,
- Chuo kikuu cha St. Joseph
- Chuo cha sayansi ya afya Teofilo kisanji.
- Chuo kikuu – Mbeya,
- Chuo Kikuu cha Jimbo la Zanzibar,
- Chuo Kikuu cha Dodoma
- Chuo kikuu cha Zanzibar
Sifa Za Kujiunga na Kozi ya Nursing Ngazi ya Diploma
Hapa chini tunaenda kukuwekea sifa na vigezo vinavyohitajika kwa mwombaji anaetaka kujiunga na kozi ya uuguzi (Nursing) kwa ngazi ya Diploma kwenye chuo chochcote kile
1. Mwombaji anapaswa kua amehitimu elimu ya sekondari kidato cha 6
2. Awe na cheti cha NECTA (ACSEE) chenye ufaulu mzuri wa pass 5 kwenye masomo ya msingi ikiwa ni pamoja na somo la hisabati na kingereza na angalau credit 3 kutoka kwenye masomo ya biologia, kemia na fizikia.
3. Kwa mwombaji wa Diploma ya kawaida ya uuguzi na ukaga ( Ordinary Nursing Diploma) anatakiwa kua na ufaulu wa pass nne kwenye masomo ya msingi ikiwa pamoja na kemia, biolojia na sayansi ya fizikia/uhandisi kwenye cheti cha sekondari (CSEE).
4. Mwombaji mwenye ufaulu wa masomo ya Hisabati ya msingi (Basic Mathematics) na lugha ya kingereza huchukuliwa kama vigezo vya nyongeza.
5. Pia waombaji waliohitimu kozi ya ufundi (NTA Level 5) katika uuguzi na ukunga kutoka taasisi yoyote inayotambuliwa na NACTEVET wanaweza kujiunga na kozi hii ya uuguzi kwa ngazi ya Diploma
Mapendekezo ya mhariri:
1. Vigezo Na Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Mweka
2. Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Diplomasia
3. Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Diplomasia
4. Sifa za Kujiunga Archbishop Mihayo University College of Tabora
5. Vigezo Na Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Ardhi Dar es Salaam
6. Jinsi Ya Kuhakiki Bima Ya Gari (Car Insurance Validity Check In Tanzania)