Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Diplomasia 2025/2026
Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Diplomasia,Habari, karibu katika makala hii ambayo kwa kina zaidi itaenda kukuonyesha sifa na vigezo vya kujiunga na chuo cha diplomasia.
Historia ya Chuo Cha Dipolamsia Kurasini,Dar es Salaam
Chuo cha diplomasia kilianzishwa mwaka 1978 ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano yaliyofanywa kati ya serikali ya Tanzania na ile ya Msumbiji
Chuo hiki cha diplomasia ni moja ya vyuo bora zaidi nchini Tanzania, kinapatika jijini Dar es Salaam kurasi.Chuo cha diplomasia cha mahusiano ya kigeni kilichopo Tanzania na Msumbiji pia kinatambulika kama chuo cha mahusiano cha kigeni CFR),
Lengo kuu la chuo cha Diplomasia cha Tanzania na Msumbiji ni kukuza maendeleo, maarifa na uelewa wa changamoto za uhusiano ya kimataifa katika viwango vya kikanda na kimataifa vya kufanya mazoezi na kukuza wataalamu, pamoja na umma kwa ujumla.
Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Diplomasia
Kozi Zitilewazo Na Chuo Cha Diplomasi
Chuo cha diplomasia kinatoa kozi mbalimbali za kawaida zinazozingatia mfumo wa Tuzo za Kitaifa za Kiufundi (NTA).
Pia chuo kinatoa kozi za muda mfupi kulingana na mahitaji ya wanafunzi.
Ikiwa wewe ni miongoni mwa maelfu wanaofikilia kujiunga na kozi zitolewazo na chuo cha diplomasia basi huna budi kufahanu sifa na vigezo vinavyohutajika ili kuweza kujiunga na chuo hiki cha mahusiano ya kigeni Cha CFR.
Makala hii itaenda kukuchambulia sifa kwa kila kozi itolewayo na chuo cha diplomasia cha Tanzania na Msumbiji
Sifa Za Kujiunga Na Kozi ya Basic Technician Ngazi ya Certificate
Kama wewe ni mwombaji wa kozi ya kozi ya Ufundi ngazi ya cheti (Basic Technician Certificate) katika chuo cha diplomasia basi lazima ukidhi sifa zifuatazo:
-Mwombaji anapaswa awe amehitimi kidato cha nne na kupata ufaulu wa angalau masomo manne,ukiondoa masomo ya dini.
-Mwombaji anapaswa awe na sifa za ngazi ya NTA Level 3 kutoka taasisi inayotambulika
Sifa Za Kujiunga na Kozi Ya Ordinary Diploma in International Relations and Diplomacy
Ili kujiunga na kozi ya diploma ya kawaida kwenye mahusiano ya kimataifa na diplomasia mwombaji inampasa awe na vigezo vifuatavyo
– Mwombaji mwenye sifa za kujiunga moja kwa moja anapaswa awe amehitimu kidato cha nne na ufaulu wa prinsipo 1 na pass 1, pia awe na credit pass kwenye masomo 3
– Waombaji wenye sifa za kujiunga wanatakiwa kua na cheti cha Ufundi Stadi (NTA level 4) kutoka taasisi yoyote inayotambuliwa na NACTE chenye angalau daraja la pili au wastani wa B na kuendelea.
Sifa Za Kujiunga na Kozi ya Higher Diploma /(NTA Level 7) Bachelor Degree in International Relations and Diplomacy (NTA Level 8)
– Mwombaji wa Moja kwa Moja anapaswa kua na Cheti cha elimu ya kidato cha sita (ACSEE) chenye ufaulu wa principle Pass 2 (4.0point) ukitoa masomo ya dini, kikiwa na credit pass ya masomo 3.
– Mwombaji mwenye Sifa za moja kwa moja anapaswa kua na diploma ya kawaida( Ordinary Diploma) kwenye mahusiano ya kimataifa na diplomasia( NTA Level 6) au fani inayohusiana nayo kutoka taasisi yoyote inayotambuliwa na NACTE yenye angalau daraja la PILI au GPA ya 3.0 na kuendelea.
Sifa za Kujiunga na Kozi ya Bachelor Degree IN International Relations and Diplomacy
– Mwombaji wa moja kwa moja anapaswa awe amehitimu stashahada Ya Juu ya Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia ( Diploma in international relations and Diplomacy) kwa ufaulu anaweza kuendelea na Shahada ya Kwanza katika Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia (kiwango cha NTA 8).
Sifa za Kujiunga na Kozi ya Postgraduate Diploma in Management of Foreign Relations
– Mwombaji wa moja kwa moja anapaswa kua na shahada ya kwanza au inayolinga nayo kutoka taasisi inayotambulika yenye GPA isiyopungua 2.0; au Diploma ya Sawa na Stashahada ya Juu kutoka kwa taasisi inayotambulika yenye daraja isiyopungua ‘B’;
Sifa za Kujijnga na Kozi ya Postgraduate Diploma in Economic Diplomacy
-Mwombaji wa moja kwa moja anapaswa kua na Shahada ya kwanza au inayolingana nayo kutoka taasisi inayotambulika yenye GPA isiyopungua 2.0; au Sifa Sawa na Diploma ya juu kutoka katika taasisi inayotambulika isiyopungua wastani wa daraja ‘B’
Sifa za Kujiunga na Kozi ya Postgraduate Diploma in Peace and Conflict Management
– Mwombaji anapswa kua na Shahada ya kwanza au inayolingana nayo kutoka kwa taasisi inayotambulika yenye GPA isiyopungua 2.0; au
– Mwombaji anapaswa kua na Diploma ya Juu kutoka katika taasisi inayotambulika isiyopungua wastani wa daraja ‘B’.
Sifa Za Kujiunga na Kozi ya Master’s Degree in Strategic Governance
– Mwombaji wa moja kwa moja anatakiwa kua na Shahada ya kwanza au inayolingana nayo kutoka taasisi inayotambulika yenye GPA isiyopungua 2.7;
– Mwombaji anapswa kua na Stashahada ya Juu isiyopungua wastani wa daraja ‘B’ kutoka katika taasisi inayotambulika.
NB: Mahitaji ya ziada yanaweza kuhitajika, kama vile ujuzi katika lugha ya Kiingereza
Mapendekezo ya mhariri:
Sifa za Kujiunga Archbishop Mihayo University College of Tabora
Vigezo Na Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Ardhi Dar es Salaam
Sifa Za Kujiunga Na Arusha Technical College
Sifa Za Kujiunga Na Chuo cha ardhi Tabora ARITA 2024/2025
Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha DUCE Entry Requirements